Hakuna Timu ya kuifunga Simba SC, Kituo kinachofuata ni Iringa, Kila timu ishinde mechi zake!

Hakuna Timu ya kuifunga Simba SC, Kituo kinachofuata ni Iringa, Kila timu ishinde mechi zake!

Ligi Kuu ya Tanzania kwa mzunguko huu wa lala salama, hakuna Klabu ya mpira yenye uwezo wa kuifunga Simba SC kutokana ubora wa kikosi.

••Watafanya Nini Sasa Uwezo Hamna

Simba SC imekuwa ikitandaza gozi la ng'ombe vema kabisa kwa viwango vya juu, huku wakipiga pasi za maana zilizothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) na kusababisha Simba SC kupata matokeo chanya.

Klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi wao wanachokifanya ni kutiririka tu kwenye mtelemko wa kuzoa pointi tatu kila mchezo, Yanga kachukua kidude 1-0 Uwanja wa Taifa, African Lyon kagaragazwa 3-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Azam FC kachapwa 3-1 Uwanja wa Taifa, klabu ambazo kidogo zilikuwa zikitegemewa kuleta upinzani wa kupata walau sare, kwa mukhadha huo hakuna kwa sasa timu ambayo itaifunga Simba SC kwenye TPL.


••Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Katika mwendelezo wa kukusanya pointi tatu tatu kila sehemu, kwa sasa kituo kinachofuta ni Ipogolo mkoani Iringa ambapo Lipuli watalazimika kushuka katika eneo lao nakuacha pointi tatu huku safari ya Watakatifu Simba ikiendelea.

Klabu ya Simba imeondoka leo kuelekea mkoani Morogoro ambapo leo jioni watafanya mazoezi kisha kesho asubuhi wataanza safari kuelekea mkoani Iringa ambako Jumanne itakipiga na Wanapaluhengo Lipuli FC.

Niiii Ghazwat kwa niaba ya sembo OKW BOBAN SUNZU Shunie King Ngwaba Sapta Sapta Tui tunawaambia watani zetu Sibonike Mwana Mtoka Pabaya Shadeeya Prince Kunta Kila timu ishinde mechi zake..!View attachment 1030312View attachment 1030313View attachment 1030314

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni nani eti mpaka nikubishie
 
Mentality ya Simba kwa mashabiki Hadi wachezaji kuwa hatufungwi tukiwa kwa Mkapa na wageni wanajua wakija machinjioni pale hawatoki nakukumbusha tuu Mwaka 2003 wakati Simba tupo makundi ya klabu bingwa kipindi kile makundi ilikua ngazi ya nane Bora Simba alishinda mechi 2 za nyumbani na Moja tulitoa sare na Ismailia refa alikataa goli la wazi la Emmanuel Gabriel Batistuta,tukamaliza na points 7 Enyimba alienda kuwa bingwa lakini aliacha points 3 hapa uwanja wa Uhuru almaarufu "shamba la Bibi" mwaka huu makosa hayajirudii kwa Mkapa hatoki mtuView attachment 1030349

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka hilo goli mkuu.
Mipango ni kuhakikisha Soura anakula kibano kwake baasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom