dumejm
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,180
- 853
Madini
Mara nyingi tunachanganya biashara, kazi na kujiajiri.
Iko hivi:
1. Mfanyakazi ni Mtu aliye ajiriwa au amejiajiri awe mchuuzi au mjasiriamali. Utakuwa mfanyakazi kama kipato chako kinategemea uwepo wako sehemu ya kazi.
2. Mfanyabiashara ni mtu ambaye amejenga taasisi ambayo mara nyingi ni kampuni, yenye mifumo na utaratibu rasmi wa uendeshaji wake. Hapa mwenye kampuni anaweza kupata faida hata kama hafanyi kazi. Kwa sababu kuna watu wanamfanyia kazi.
Tofauti na kazi, biashara inaingiza pesa hata bila mmiliki kuwepo au kuhusika. Mara nyingi mmiliki akishaweka mifumo madhubuti anakaa pembeni na ana oversee kwa juu pale na kuweka mikakati zaidi..
Biashara inaweza kurithishwa lakini lazi haiwezi kurithishwa. Ukiwa CEO wa kampuni kubwa hata kama unalipwa ma billion uki retire au kufa ndo mwisho wa mabilioni yako. Watoto au familia yako haiwezi kurithi kazi yako.
Utajiri unakuja pale ambapo mtu anakuwa na biashara (portifolio) zaidi ya moja. Umeshaweka mipango yako wewe unapata gawio tu, huku ukiendelea kula bata.
Infact mtoa mada ana point, kwa sababu watu wengi wanaojiita wafanyabiashara ni wafanyakazi waliojiajiri. Wabongo hatuna utamaduni wa kuweka mifumo na utaratibu wa usimamizi wa biashara zetu kiasi kwamba muhusika mkuu akiondoka na biashara inakufa.