Hakuna Tume Huru, hakuna uchaguzi utakaokubalika nchini Waziri Selemani Jafo awajibike kwa kuharibu uchaguzi

Zito hapo wa kujiuzuru ni Waziri kamili na huyo msaidizi wake ni kwa uwajibikaji tuu! lakini naona mnamruka kumuongelea huyo waziri kamili wa wizara hiyo.

In that first place sikujua kwanini hiyo wizara ilitoka kwa waziri mkuu mpaka huko iliko, kumbe ni kwa mkakati mfu huu!
 
Solution itapatikana kwa kufanya maamuzi magumu kama inavyofanyika katika mataifa mengine.Magu na CCM ni maadui wa demokrasia hivyo ni lazima zitumike mbinu/njia za kuwalazimisha waheshimu demokrasia na si vinginevyo.

Tusijidanganye!!!
 
Wapinzani walinusa dalili za kushindwa

Wakaamua kijiondoa kukwepa aibu

Hivi kwa uchapakazi wa Magufuli kuna mtu ana muda wa kusikiliza Wapinzani?
Hizo kazi unazodai huyo haramia anafanya anamfanyiaga mama ako nn ndomana mwezetu unaziona nakufaidika nazo,mana kilasiku unaziona mana zipondani ya kutazenu zanyumba ndomana imekua rahisi uzione
 
MSIMAMO WA ACT-WAZALENDO;

“HAKUNA TUME HURU, HAKUNA UCHAGUZI UTAKAOKUBALIKA NCHINI” WAZIRI SELEMANI JAFO AWAJIBIKE KWA KUHARIBU UCHAGUZI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa leo Tarehe 11/11/2019

1. Mchakato wote wa Uchaguzi uanze upya: Lazima yote yaliyofanyika chini ya utaratibu wa sasa yafutwe, uchaguzi uahirishwe na mchakato wa uchaguzi uanze upya.

2. Wasimamizi wa Uchaguzi wote walioharibu mchakato wa uchaguzi huu wawajibishwe ili kukomesha tabia hii inayoharisha amani ya nchi.

3. Zitungwe Kanuni Mpya za Uchaguzi kwa maridhiano na makubaliano na Wadau wote hususani vyama vya siasa.

4. Iundwe Kamati Huru ya kusimamia Uchaguzi: Lazima maamuzi katika hatua zote za Uchaguzi yawe ya maridhiano na makubaliano ya vyama sio TAMISEMI, ambao hawana uhuru, uwazi na wala uwezo wa kutenda haki.

5. Waziri Selemani Jafo aitishe kikao cha pamoja cha vyama vyote vya siasa ili kukubaliana juu ya namna ya kusonga mbele Kwa utekelezaji wa mapendekezo yetu hayo. Kinyume na hivyo sisi ACT Wazalendo hatutashiriki Uchaguzi huu wa Tarehe 24 Novemba, 2019.

6. Kutokana na O-TAMISEMI kuwa Wizara iliyopo chini ya OFISI YA RAIS, tunamtaka Rais Magufuli afikirie upya kuiondoa ofisi hii Ikulu na kuirejesha kwa Waziri Mkuu kama ilivyokuwa awali ili ‘TAASISI YA URAIS IEPUKANE NA KASHFA ZA UHARIBIFU WA DEMOKRASIA NCHINI’

7. Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya Siasa kutokubali hadaa ya Waziri Jafo na kutumia nafasi hii kuwa pamoja kudai Tume Huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi wa mwaka 2020 usiwe na dosari tulizoshuhudia sasa. Bila Tume Huru ya Uchaguzi pasiwe na Uchaguzi wowote nchini. Viongozi wa Kitaifa wa vyama watoke na tamko la pamoja kutaka TUME HURU YA UCHAGUZI.

HITIMISHO

Ndugu wanahabari, ni wazi mchakato wa uchaguzi huu wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, hauwezi kuendelea kwa haki hasa baada ya wananchi kuonyesha hisia zao za kuichoka CCM katika hatua za awali katika uandikishaji wapiga kura. Serikali ya CCM itaendelea na gilba zake kuhakikisha inapoka demokrasia ili kujihalalishia ushindi kwa kutumia mabavu ya dola na mtandao mpana uliowekwa kwa kazi hiyo. Ndio maana vitisho vya waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola na DCI Robert Boaz vinaendelea kila uchao.

Tunaendelea kusisitiza msimamo wetu wa kujitoa kwenye uchaguzi na kuwataka wanachama wetu wote nchi nzima kuendelea kutekeleza agizo la Chama la kuandika barua za kujitoa kwenye uchaguzi. Aidha tunatoa wito kwa wanachama wetu kubaini wagombea bandia wa CCM waliopewa fomu kwa kugushi mihuri na barua za utambulisho maeneo kadhaa nchini ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.”
….
Joran Bashange
MWENYEKITI WA KAMATI YA KAMPENI NA UCHAGUZI TAIFA.
Ugonjwa was moyo unakufuata.
Maana unachosema na ukweli ni tofauti.
Process zote zinaendelea.
 
MWISHO WA SIKU SISI WATANZANIA BADO HATUJACHOKA NA UGUMU WA MAISHA. MTUACHE TUKICHOKA TUTAAMUA WENYEWE BILA KUPITIA VYAMA VYENU VYA SIASA. KWA SASA TUNAWATAZAMA MNAVYOJIKUNA WENYEWE HUKU MKILIPANA RUZUKU NA PISHO ZA VIKAO
 
Wapinzani walinusa dalili za kushindwa

Wakaamua kijiondoa kukwepa aibu

Hivi kwa uchapakazi wa Magufuli kuna mtu ana muda wa kusikiliza Wapinzani?
Watetezi wa CCM mitandaoni ni wapumbavu
 
Huyu mzushi ambaye hata aibu hana.
 
"You give them an inch they ask for a mile"
 
Huyu Zitto Wananchi tumechoka na siasa zake za ulaghai

Kuna kijana anayekubalika kigoma yote amerudi Ccm leo ,huyu Ndio mrithi wa Zitto sasa
Wewe jamaa Unafanya kazi saa ngapi? Au hii kutetea chama Tawala ndio ajira yako hapa?
 
Wapinzani walinusa dalili za kushindwa

Wakaamua kijiondoa kukwepa aibu

Hivi kwa uchapakazi wa Magufuli kuna mtu ana muda wa kusikiliza Wapinzani?
Nyie wajinga sana kama anachapa kazi kwa nini watendaji wajifiche na kufunga ofisi?
 
Zitto wewe ni mnafiki na mchochezi mmoja hapa Nchini
wewe na wanavyama wenzia tayari mshagomea uchaguzi sasa mnalalamikia nini
gomeeni nchini
 
Huyu Zitto Wananchi tumechoka na siasa zake za ulaghai

Kuna kijana anayekubalika kigoma yote amerudi Ccm leo ,huyu Ndio mrithi wa Zitto sasa
Buku 7 unazopata unazotendea haki, kazi unayoifanya siyo mchezo japo ni ya kitoto sana.
 
MSIMAMO WA ACT-WAZALENDO;

“HAKUNA TUME HURU, HAKUNA UCHAGUZI UTAKAOKUBALIKA NCHINI” WAZIRI SELEMANI JAFO AWAJIBIKE KWA KUHARIBU UCHAGUZI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa leo Tarehe 11/11/2019

1. Mchakato wote wa Uchaguzi uanze upya: Lazima yote yaliyofanyika chini ya utaratibu wa sasa yafutwe, uchaguzi uahirishwe na mchakato wa uchaguzi uanze upya.

2. Wasimamizi wa Uchaguzi wote walioharibu mchakato wa uchaguzi huu wawajibishwe ili kukomesha tabia hii inayoharisha amani ya nchi.

3. Zitungwe Kanuni Mpya za Uchaguzi kwa maridhiano na makubaliano na Wadau wote hususani vyama vya siasa.

4. Iundwe Kamati Huru ya kusimamia Uchaguzi: Lazima maamuzi katika hatua zote za Uchaguzi yawe ya maridhiano na makubaliano ya vyama sio TAMISEMI, ambao hawana uhuru, uwazi na wala uwezo wa kutenda haki.

5. Waziri Selemani Jafo aitishe kikao cha pamoja cha vyama vyote vya siasa ili kukubaliana juu ya namna ya kusonga mbele Kwa utekelezaji wa mapendekezo yetu hayo. Kinyume na hivyo sisi ACT Wazalendo hatutashiriki Uchaguzi huu wa Tarehe 24 Novemba, 2019.

6. Kutokana na O-TAMISEMI kuwa Wizara iliyopo chini ya OFISI YA RAIS, tunamtaka Rais Magufuli afikirie upya kuiondoa ofisi hii Ikulu na kuirejesha kwa Waziri Mkuu kama ilivyokuwa awali ili ‘TAASISI YA URAIS IEPUKANE NA KASHFA ZA UHARIBIFU WA DEMOKRASIA NCHINI’

7. Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya Siasa kutokubali hadaa ya Waziri Jafo na kutumia nafasi hii kuwa pamoja kudai Tume Huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi wa mwaka 2020 usiwe na dosari tulizoshuhudia sasa. Bila Tume Huru ya Uchaguzi pasiwe na Uchaguzi wowote nchini. Viongozi wa Kitaifa wa vyama watoke na tamko la pamoja kutaka TUME HURU YA UCHAGUZI.

HITIMISHO

Ndugu wanahabari, ni wazi mchakato wa uchaguzi huu wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, hauwezi kuendelea kwa haki hasa baada ya wananchi kuonyesha hisia zao za kuichoka CCM katika hatua za awali katika uandikishaji wapiga kura. Serikali ya CCM itaendelea na gilba zake kuhakikisha inapoka demokrasia ili kujihalalishia ushindi kwa kutumia mabavu ya dola na mtandao mpana uliowekwa kwa kazi hiyo. Ndio maana vitisho vya waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola na DCI Robert Boaz vinaendelea kila uchao.

Tunaendelea kusisitiza msimamo wetu wa kujitoa kwenye uchaguzi na kuwataka wanachama wetu wote nchi nzima kuendelea kutekeleza agizo la Chama la kuandika barua za kujitoa kwenye uchaguzi. Aidha tunatoa wito kwa wanachama wetu kubaini wagombea bandia wa CCM waliopewa fomu kwa kugushi mihuri na barua za utambulisho maeneo kadhaa nchini ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.”
….
Joran Bashange
MWENYEKITI WA KAMATI YA KAMPENI NA UCHAGUZI TAIFA.
Tume Huru mliikataa Bunge maalum la Katiba mkatoka wote kwa ujinga CCM wakaipitisha
Kwa sasa ni bora mkadai Katiba pendekezwa ambayo ipo kwenye makabati ya Ikulu ipigiwe kura ya ndiyo au hapana hiyo ndiyo salama yenu.
Huko mtapata Tume Huru vinginevyo kaeni kimya hatutaki ngonjera zenu.
 
Ndugu Zitto. Tume huru kwa sasa ni kama Ndoto ya Alinacha
 
Kwa mara ya kwanza ninashuhudia nadharia ya refa, goalkeeper na striker akiwa ni mtu mmoja tu, huhitaji mtaalamu wa mchezo kujua matokeo yatakuwaje!!!
 
Back
Top Bottom