Hakuna ubaguzi wa rangi wala mfumo dume, Democrats wameshindwa kihalali kwasababu wameiharibu mno marekani na wangeharibu zaidi wangeshinda

Hakuna ubaguzi wa rangi wala mfumo dume, Democrats wameshindwa kihalali kwasababu wameiharibu mno marekani na wangeharibu zaidi wangeshinda

Hapo uliposema Marekani kuna ukosefu wa ajira ni Uongo.
Marekani kuna kazi nyingi za kubeba box, kusimamia stoo za amazon, kulea wazee, n.k.

Wamarekani wengi walipata kazi nyingi viwandani zenye malipo ya kati awamu ya Trump lakini viwanda vingi vilifungwa kwenye awamu ya Biden
 
Wewe na wanaokuunga mkono mnasikiliza sana uwongo na propaganda za Trump na watu wake; ni haki yenu mfurahia matokeo.

Trump aliingia madarakani wakati uchumi wa marekani unakua kwa 2.9%, unemployement ilikuwa imeungua kutoka 14% hadi kufikia 4.1% na infalation ilikuwa 1.3%. Aliishi kwa momenmtum ya uchumi huo aliorithi ingawa GDP yake ilikuwa inatelemka. Ilipokuja hali inayotaka uongozi wake, akaboronga na kuanguasha uchumi hadi GDP ikafikia -2.21%, unemployement ikawa 15%. Biden akarithi mzigo ambao ameurekebisha hadi sasa hivi uchumi unakuwa kwa 2.8% tena, uneplyment iko 4.1% na inflation ni 2.4%. lakini Trump amekuwa anajisisfia sana kuwa anajua kuongoza uchumi wakati hakuna kitu.

Sasa hivi Trump anarithi uchumi ulioimarika ahalafu atajisifia sana, na watu kama wewe ambao hawako informed.
watachukua uwongio huo na kuufanya kuwa kweli. Utasikia eti crime is too high because of Biden lakini FBI wanakuambia kuwa mwaka 2019 (wakati wa Trump) violent crimes zilikuwa 1,745,570, lakini mwaka 2023 (wakati wa Biden) violent crimes zilipungua na kufikia 1,343,180. Lakini Trump anapiga uwongo kuwa crime is everywehere kama Marekani sasa hivi ni nchi ya hatari sana, halafu watu kama wewe mnakubaliana naye.

Marekani ina watu wengi ambao hawako informed, hivyo Trump kushinda na halali yake.
Kipindi ambacho Obama anamaliza muhula wake, uchumi ulikuwa umedorola, aliwaambia wapiga kura Inahutajika muujiza kuufufua uchumi lakini Trump alimshangaza, aliimarisha sana uchumi kwasababu alipunguza sana kodi na kuchochea biashara mpya kufunguliwa, kulikuwa na oppurtunity zones za wamarekani weusi wanafanya biashara kwa kodi kiduchu, Makampuni mengi yenye viwanda China yalirudi Marekani na kuwapa ajira wamarekani, Trump aliwachapa Tarrifs wachina Marekani iliingiza mabilioni ya dola kwenye bidhaa zinazotoka China, n.k.

Uchumi wa sasa wa Marekani kodi zimepandishwa, kodi zinatandikwa hadi kwenye tips na overtime, mfumuko wa bei ni jambo linalowaumiza sana wamarekani awamu hii, watu waliozoea kufanya kazi 1 wanafanya kazi mbili kupambana na mfumuko wa bei, Kazi nyng zimehamia nje ya nchi kwasababu viwanda vingi vimehama,
 
Duh! Ilitakiwa Trump aapishwe usiku huu huu na sio kusubiri hadi January, 2025!

Kama hali ndio hiyo wanastahili kabisa kufuata precedence waliyoacha Kivuitu na Kibaki.
Wenzetu hawana mihemko.
 
Kwa ile idadi ya wahamiaji haramu kujaa Marekani, bila shaka uhalifu lazima uwe juu. Hata Tanzania hatuwezi kufanya upuuzi wa kumruhusu kila mtu ajiingize tu nchini bila kibali wala uhalali.

Trump yuko sahihi, ndiyo maana amerejea Jumba Juepe.
Siyo kweli mzee wangu; in fact wahamiaji ndio wanaofuata sheria sana kwa kuogopwa kudakwa
 
We ndio mungo Tena mpumbavu wa kitumbikwela
Kwa lugha yako, inaonyesha na wewe ni mmoja wale Poorly educated kwa vile hata huwezi kutetea hoja yako ila unataka kulazimisha tu. Huenda na wewe uliandamana January 6 kwani waliondamana siku ile wote walikuwa ni poorly educated.
 
Si wanasemaga marekani inaongozwa na mfumo siyo mtu?? Au huwa ni uongo wa majinga Chadema?

Iweje Trump aongoze kivyake na Biden kivyake?
Kuna ukwel flan ndan yake

Marais waliopita wakiwemo waliotoka chama cha Trump kuna mambo walifanana na marais wa Democrats mfano kuanzisha na kufadhili vita, Bush alizivamia Afghanistan na Iraq, Obama alitoa mkongoto wa nguvu Libya, Biden na yeye anafadhili mno vita ya Ukraine na upande mwengine kawaimarisha sana Iran, Ni biashara za Silaha hizi, Marekani ndie Kinara, Kuna maslah mengine hufaidika ikiwemo kuchota rasilimali kama mafuta wakati vita zinaendelea.

Trump yupo tofauti sana ni mpenda amani ndio maana dunia ilitulia zaidi awamu yake, Al Qaeda na Isis waliufyata !! Putin alitulia, Iran ilifulia, hizi fujo zimeanza baada ya yeye kuondoka

Ndio maana wamejarbu mara mbili kum shoot, yupo tofauti na wenzake.
 
Siyo kweli mzee wangu; in fact wahamiaji ndio wanaofuata sheria sana kwa kuogopwa kudakwa
wahamiaji halali waliofata utaratibu wa kupata visa ndio wanafuata sana sheria

Hawa maharamia wengi wanawake na watoto ni mali za magenge wanavushwa kufanya biashara ya ngono, Wanaume kuna kundi kubwa la wahalifu waliokimbia nchi zao, kuvusha madawa ya kulevya, kuongeza nguvu kwenye magenge ya kihaliifu, n.k.
 
Unarudia maneno ya Trump kama wimbo. Sijui unapata wapi habari lakini ni wazi hauko informed kabisa

1730920393898.png

Soma paper kamili hapa
 
Attachments

Unarudia maneno ya Trump kama wimbo. Sijui unapata wapi habari lakini ni wazi hauko informed kabisa

View attachment 3145566

Soma paper kamili hapa
Maharamia hawapendi kuishi Texas kwasababu ni jimbo la Republicans, kuna sheria kali sana za uhalifu na ni jimbo linalosifika kwa wakazi wake kujilinda na bunduki.

Maharamia wanapenda zaidi kwenda majimbo ya Democrats mfano california wameruhusu sheria ukiiba vitu cisivyozidi dola 950 (zaidi ya shilingi milioni 2) hakuna jela, Chicago, Newyork, n.k. kuna sheria dhaifu za kuwalinda wahalifu hasa maharamia
 
Kilichopigiwa kura zaidi ni sera ya kuilinda Marekani, Sera za Democrats zimeiharibu sana Marekani,

Haya ni baadhi ya mambo waliyofanya Bidden na Haris kwenye awamu yao, Trump kashinda kwasababu kaapa anaenda kuyafuta na kuyarekebisha.

Mfumuko wa bei na maisha kuwa juu, vyuma vimekaza Marekani, watu wengi uchumi daraja la chini la kati waliofanya kazi 1 kukidho mahitaji yao lakini awamu hii wanafanya kazi 2, Wamarekani wengi hawakuwa tayari kumpa kura Harris kwasababu angefanya maisha yawe magumu zaidi kiuchumi, Vitu vya muhimu kama chakula, mafuta, umeme, Kodi za nyumba n.k vimepanda mno gharama, Ndio sababu ya wanawake wengi wanaoshinda nyumbani wakiwa na uhakika wa kupokea pesa za matunzo na pesa za malezi ya mtoto wamempigia kura Harris lakini wanaume na wanawake wengi wanaojitafutia pesa wamemchagua Trumo

Ongezeko la kodi na kuwatoza kodi wafanyakazi kwenye Tips na overtime, Kwa marekani ni utamaduni uliozoeleka ukiuhudumiwa na watu kama waiter unatoa tip, hii huwa inapigwa kodi, Overtime masaa ya ziada kazini yanapigwa kodi.

Kuruhusu wanaume kubadili jinsia na kuishi kwenye hostel za wanafunzi wa kike, kuoga nao kwenye mabafu, kwenye michezo, n.k. michezoni wanaume wamevunja rekodi nyingi,

Kuruhusu maharamia milioni 20 kuingia Marekani, Siku ya kwanza Biden kuingia ofisini alifuta sheria nyingi za Trump zilizozuia maharamia kuingia nchini, Matokeo yake mipaka ikawa wazi, magenge ya kihalifu yamesafirisha wanawake na watoto wengi sana kuwatumikisha kwenye biashara ya ngono, wahalifu kuanzia wauaji, wabakaji, majambazi, n.k. wanatoroka nchi zao kwenda Marekani, Uhalifu umezidi mno Marekani, magenge ya Venezuela yameanza kuchukua kimabavu apartments.

Kupunguza support kwa Israel mshrika mkuu wa Marekani, Kamala alionyesha dalili za wazi kuwavumilia waandamaji wa Hamas kwa kuwaruhusu kufunga barabara, kuweka kambi vyuoni, n.k. Netanyahu alihutubia bunge la Marekani bila ya uwepo wa Kamala na Biden licha ya wabunge wa Democrats kuhudhuria, Mipango ya Israel kuishambulia Iran ilivujishwa, n.k.

Kuruhusu watoto kubadili jinsia bila ridhaa ya wazazi, hii ilifanya wazazi kupoteza controll ya watoto wanaoshawishika kirahisi

Kufundisha watoto wadogo elimu ya viungo vya uzazi, ikiwemo sex, masturbation, n.k.

Kuruhusu wanawake kufanya late term abortion, kuharibu mimba iliyofikia miezi 9
Sisi huku ketu wananchi hawawezi kuchambua mambo ili wafanye uchaguzi sahihi. Wameshikwa akili na huchagua chama badala ya mtu!
 
Wewe na wanaokuunga mkono mnasikiliza sana uwongo na propaganda za Trump na watu wake; ni haki yenu mfurahia matokeo.

Trump aliingia madarakani wakati uchumi wa marekani unakua kwa 2.9%, unemployement ilikuwa imeungua kutoka 14% hadi kufikia 4.1% na infalation ilikuwa 1.3%. Aliishi kwa momenmtum ya uchumi huo aliorithi ingawa GDP yake ilikuwa inatelemka. Ilipokuja hali inayotaka uongozi wake, akaboronga na kuanguasha uchumi hadi GDP ikafikia -2.21%, unemployement ikawa 15%. Biden akarithi mzigo ambao ameurekebisha hadi sasa hivi uchumi unakuwa kwa 2.8% tena, uneplyment iko 4.1% na inflation ni 2.4%. lakini Trump amekuwa anajisisfia sana kuwa anajua kuongoza uchumi wakati hakuna kitu.

Sasa hivi Trump anarithi uchumi ulioimarika ahalafu atajisifia sana, na watu kama wewe ambao hawako informed.
watachukua uwongio huo na kuufanya kuwa kweli. Utasikia eti crime is too high because of Biden lakini FBI wanakuambia kuwa mwaka 2019 (wakati wa Trump) violent crimes zilikuwa 1,745,570, lakini mwaka 2023 (wakati wa Biden) violent crimes zilipungua na kufikia 1,343,180. Lakini Trump anapiga uwongo kuwa crime is everywehere kama Marekani sasa hivi ni nchi ya hatari sana, halafu watu kama wewe mnakubaliana naye.

Marekani ina watu wengi ambao hawako informed, hivyo Trump kushinda na halali yake.
Kwamba wewe ndio unaweza kua upo well informed kuliko Americans waliopiga KURA? Naweza kukubaliana na wewe kuhusu takwimu za crime zilizo tolewa na FBI kwa most of citizens wanaweza kua hawana taarifa za kutosha but kuhusu uchumi, unemployment, ugumu wa maisha, inflation nk hivo hata kipofu anaviona, havihitaji wana siasa kukuelezea.
 
Reply

Kwanza elewa kuwa nimesihi marekani takriban miaka 35 sasa kwa hiyo usidhani kuwa siijui marekani. Kuna wamarekani wengi sana waliopiga kura waliozaliwa baada ya mimi kuwapo marekani hivyo watakuwa hawaijui marekani kuliko mimi.

Kuhusu data za uchumi zipo wazi na hutolewa kila mwisho wa mwezi. Sasa kama mtu huwa hasikilizi data official anasubiri kusimuliwa ndio hupotezwa. Bureau of Labor Statistics (BLS) and the Bureau of Economic Analysis (BEA) hutoa data kila mwezi; kama huwa huzipati basi usiseme kuwa hazipo. Namba nilizokwoti hapo zimetoka huko.

Watu wasiokuwa informed hukubali lolote hasa muongeazji akirudia rudia mara nyingi sana. Trump ana sifa ya kurudia uwongo mara nyingi sana, kwa hiyo watu ambao hawako informed huwa victim wake haraka sana; na wamarekani wengi hawako informed. Kuna survey iliyotoka mwaka 2018 ilikionyesha kuwa wasikilizaji wa Fox News hawako informed kabisa; kwa hiyo ukizingatia kuwa Fox News ndiyo inayotazamwa na watu wengi sana marekani utaelewa nasema nini

Ukiangalia kura nyingi alizopata Trump ni za watu wa vijijini na miji miodgo midogo ambako watu hawako informed sana. Mpka wanafikia kukubali kuwa eti Biden alituma watu wakumwue Trump, jambo ambalo mtu yeyote mwenye akilio asingekubaliana nao.
 
Kipindi ambacho Obama anamaliza muhula wake, uchumi ulikuwa umedorola, aliwaambia wapiga kura Inahutajika muujiza kuufufua uchumi lakini Trump alimshangaza, aliimarisha sana uchumi kwasababu alipunguza sana kodi na kuchochea biashara mpya kufunguliwa, kulikuwa na oppurtunity zones za wamarekani weusi wanafanya biashara kwa kodi kiduchu, Makampuni mengi yenye viwanda China yalirudi Marekani na kuwapa ajira wamarekani, Trump aliwachapa Tarrifs wachina Marekani iliingiza mabilioni ya dola kwenye bidhaa zinazotoka China, n.k.

Uchumi wa sasa wa Marekani kodi zimepandishwa, kodi zinatandikwa hadi kwenye tips na overtime, mfumuko wa bei ni jambo linalowaumiza sana wamarekani awamu hii, watu waliozoea kufanya kazi 1 wanafanya kazi mbili kupambana na mfumuko wa bei, Kazi nyng zimehamia nje ya nchi kwasababu viwanda vingi vimehama,
Na wewe hauko informed kabisa kwa vile hujui kuwa Obama aliingia madarakani mwaka 2008 wakati uchumi umeanguka kabisa. angalia data za uchumi wakati Obama anaingia madarakani na wakati anaondoka ndipo uwe autohritative enough kujadili jambo hilo. Kwa miaka zaidi ya 30 niliyoishi marekani ni kwamba nilipoinga marekani nilikutana na matatizo yaliyoachwa na George Bush Snr. baada ya miaka minane ya Clintoni, bajeti ya serikali ikawa na surplus. Akaja George Bush Jr akairudisha nchi kwenya janga kabisa. Obama alaja kuimarisha tena uchumi kutoka kwenye korongo kubwa mwaka 2008 lakini baada ya Obama akaja Trump na kurudisha uchumi kwenye korongo tena chini ya miaka miine tu. Biden kaunyanua tena, ngoja tusubiri yajayo.

View: https://www.youtube.com/watch?v=FqhjkxdMEX8
 
Wewe na wanaokuunga mkono mnasikiliza sana uwongo na propaganda za Trump na watu wake; ni haki yenu mfurahia matokeo.

Trump aliingia madarakani wakati uchumi wa marekani unakua kwa 2.9%, unemployement ilikuwa imeungua kutoka 14% hadi kufikia 4.1% na infalation ilikuwa 1.3%. Aliishi kwa momenmtum ya uchumi huo aliorithi ingawa GDP yake ilikuwa inatelemka. Ilipokuja hali inayotaka uongozi wake, akaboronga na kuanguasha uchumi hadi GDP ikafikia -2.21%, unemployement ikawa 15%. Biden akarithi mzigo ambao ameurekebisha hadi sasa hivi uchumi unakuwa kwa 2.8% tena, uneplyment iko 4.1% na inflation ni 2.4%. lakini Trump amekuwa anajisisfia sana kuwa anajua kuongoza uchumi wakati hakuna kitu.

Sasa hivi Trump anarithi uchumi ulioimarika ahalafu atajisifia sana, na watu kama wewe ambao hawako informed.
watachukua uwongio huo na kuufanya kuwa kweli. Utasikia eti crime is too high because of Biden lakini FBI wanakuambia kuwa mwaka 2019 (wakati wa Trump) violent crimes zilikuwa 1,745,570, lakini mwaka 2023 (wakati wa Biden) violent crimes zilipungua na kufikia 1,343,180. Lakini Trump anapiga uwongo kuwa crime is everywehere kama Marekani sasa hivi ni nchi ya hatari sana, halafu watu kama wewe mnakubaliana naye.

Marekani ina watu wengi ambao hawako informed, hivyo Trump kushinda na halali yake.
Wewe hapo unajiona una akili na kuita anachokisema Trump ni propaganda??? Halafu tukikuliza hizi data zako wewe umetoa wapi au chanzo Chake ni nini utataja WP(Washington Post),NY times na liberal media outlets zingine ambazo nyingi ni pro-government na Tena hizo liberal medias zimekuwa zikiwapeni nyie wafuasi wa Kamala ill-informations.

Hebu tembelea kwenye forums mbali mbali uone wamerakani wanavyoongelea suala la uchumi na ajira kwa miaka minne ya Biden na jinsi wanavyofurahi Trump kushinda.

Umejaribu hata kujiuliza ni kwanini licha ya kashifa mbaya zinazomuandama Trump lakini wamarekani Bado wamemchagua Trump Tena kwa kishindo??? Kwa sababu wanajionea jinsi gani nchi yao ilivyoharibika kwa huu muda wa hii miaka minne karibu kwenye angle zote... Sera za Democrats zinatishia kupungua kwa nguvu kazi Marekani siku za mbeleni kwa maana ya low fertility rate, imagine eti leo hii Kila mwanamke awe na ruksa ya kutoa mimba muda wowote anaojiskia Tena Bure kwenye hospital yeyote ile....nini kitatokea?? Watu si watakuwa wanatoa tu mimba kiholela holela, mtu anahitaji mtoto wa kike amegundua mimba aliyobeba ni ya mtoto wa kiume anaenda anaichomoa.

Biden mpaka kufikia mwezi July mwaka huu alikuwa ameshatoa msaada wenye thamani ya dollar za kimarekani zaidi ya $174b kwa serikali ya Ukraine kwenye vita inayoendelea na mrusi na hizi zote ni pesa za walipa Kodi wa Marekani na wamepiga sana kelele kuhusu kutoa hiyo misaada maana hata wao Wana matatizo yao huko nchini kwao ikiwemo upungufu wa ajira... lakini Biden anasitiza tu "we will never back down to assist Ukraine".

Kwa ufupi tu serikali ya Biden imewaudhi sana wamerakani na wameona kabisa kumchagua Kamala ni kuendeleza matatizo Yale Yale ya Bidden Tena Kamala ndio uongozi wake ungeweza kuwa wa ovyo sana kuliko hata wa Bidden.

#TRUMP WILL FIX IT
#TRUMP2024
 
Marekani kuna kazi nyingi za kubeba box, kusimamia stoo za amazon, kulea wazee, n.k.

Wamarekani wengi walipata kazi nyingi viwandani zenye malipo ya kati awamu ya Trump lakini viwanda vingi vilifungwa kwenye awamu ya Biden
Unajua Kuna watu wakiskia neno "hakuna ajira" basi tafsiri yao ni kwamba sehemu hiyo haina shughuli yoyote ya kumuingizia mtu kipato, na kama shughuli za kuingiza kipato zinapatikana basi eneo Hilo halina ukosefu wa ajira.

Anyway Marekani Inakabiriwa na tatizo la ajira lakini Lina shughuli nyingi sana za kumuingizia mtu kipato ambazo ni menial jobs.
 
Back
Top Bottom