Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden

Hujaelewa kabisa! Hapa historia haihitajiki! Tunaangalia tukio ambalo limetokea. Na shida siyo Rais Samia au viongozi wa Africa kupanda basi. Kinachojadiliwa ni ngozi nyeusi na nyeupe! Ngozi nyeupe wamepandishwa gari maalumu na wengine kuingia na misafara! Niambia kiongozi gani wa Africa alipanda gari maalum achilia mbali msafara! Ni dhahiri ubaguzi haujaisha duniani na waliobaguliwa siyo marais wetu tu bali waafrika wote! Hicho ndiyo kitu tulichojifunza na kituwezeshe kuwa na mtizamo mpya kuhusu dunia. Mimi siyo mwandishi. Nadhani wewe kama mwandishi unahitaji kutulia na kufikiria nje ya box kabla hujakurupuka kuandika kitu chochote.
 
Hiyo kuona rais wetu kutokufurahia ni interpretation yako. Hakuna aliyelazimishwa kwenda msibani na taratibu za usafiri ziliwekwa wazi. Pili, umeshaambiwa tuna ushamba ndiyo maana kila kiongozi atasafiri na gari peke yake, maana anaona ndiyo ukubwa. Wakati wa mwalimu wabunge walipanda mabasi toka Dar kwenda Dodoma.
 
Pascal Nafikiri maneno - 'ubaguzi wa rangi' unayajua! Na pia katika hoja yako, umetoa mfano wa South Africa, sasa kilichotokea Uingereza ni hicho! Je! Waandaaji wa shughuli za mazishi walitumia kigezo gani kuwaweka waafrika basi moja? - was it country initial alphabet au It's leader's name initial alphabet! Kwanini hakuna race nyingine kwenye bus? Tuliokaa South Africa, tuna fahamu sana mpangilio huo - mnapo jikuta weusi, wahindi, wazungu etc mmepangwa wenyewe kwa wenyewe! Kwa mfano, waafrika watatu hamjuani, mmekata tiketi ya ndege kutoka Johannesburg kwenda Capetown na mme nunua ticket siku tofauti! Siku ya safari mnajikuta mmepangiwa kukaa pamoja zile siti tatu! Usiwatetee - waafrika walibaguliwa! Mimi sina tatizo na bus, nina tatizo na ubaguzi wa hali ya juu!
 
Kwanini sasa siku hizi Sasa hawapandi?
 

Kunywa bia au soda ntalipa Ngosha.Umenena vyema hawezi kutuita wajinga kwa kutoa maoni yetu.
 
Hii issue sasa inahusishwa na kutumbuliwa kwa MFA Balozi Mulamula, naendelea kusisitiza Rais Samia ni simple, humble na down to earth kama nilivyo muelezea hapa
Mkuu Sexless , kwanza naungana na wewe kwenye the quest for information, we are living in a world of information Science, akiteua atoe sababu na akitumbua pia atoe sababu. Kwa vile hatujahi ku demand rais atoe sababu za kumteua fulani, siku akitumbua pia hatuna justification ya ku demand kupewa sababu!.

Nimekuleta hapa ili kukujulisha kuwa huyu Mama ni very humble and down to earth, hivyo hana tatizo kabisa na ile issue ya London bus kama nilivyo eleza hapa Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…