hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
Kaka ,Mimi najibu hoja wewe unasema nipo kushindana ,kwanini ....au unataka nikubaliane na unachosema hata kama naona ni uongo?Halafu Rudi Kasome Mimi Nilisema Dini au Nilisema Ibada..
Na ndo maana Nilikuuliza mara Mbili Unajua Tofauti ya Dini na Ibada..
sijadokoa Nilivyovitoa Ndo Msingi hasa wa Dini Hizi mbili yoyote asiye swali kati ya Dini Hizi mbili Huesabika Kuwa hafanyi Ibada..
yoyote asiyesoma Talmud na Hadithi huhesabika Ni mtu asiyejua Dini..Yoyote asiyefanya wudhu na Netilat hana Utukufu..
mwanzoni Nilikuambia Kuwa Unapoingia kwenye Mijadala Jitahidi Usitafute Kushinda Lengo Liwe ni Kuelimika Ila kama Ukitafuta Kushinda Utatoka Kappa Katika kuelewa baadhi ya Vitu..
mimi Huwa naingia Kwenye Mijadala lengo ni Kupata Elimu nisiyo nayo..
viko Vitu vingi sana Nimeweka Vichache kwa sababu ya Ugumu wa Kuviandika Vyote na Najua Pia nikiandika Viti vingi hitaweza kusoma..
kuna Hadithi halafu Kuna Sunna..
Kama kweli wewe Ni Ulikuwa Mwislamu utaweza Kutofautisha Kati ya Hadithi na Sunna..
Na Sikuweka Talmud peke yake soma Ili.Kuelewa Sio Kusoma Ili kujibu Hoja Zangu uonekane kwanmba umeweza kuziwekea Pingamizi..
kumbuka Sijaweka Shofar peke yake Nimekuwekea Mpaka Shema Yisrael!
Eleza Kuhusu Hiyo ambayo Nimekuwekea Mpaka Video..
Na kwa bahati nzuri nimeweka mpaka Maneno ya Imani na Nimeonyesha yanatoka kitabu gani..
hapa ndo naamini Unasoma Ili upate njia ya kujibu..
Na Ningependa Usome zaidi Kuhusu Shofar Inaonekana Huna Elimu nayo kabisa..
Wudhu sio Kusali tu Mkuu..
wudhu hata Ukiataka Kula unatakiwa utie Udhu..
kulingana na Maandiko kabla hujachangia Hoja Ijue kwanza hoja
Kuoga Janaba ni ibada ya Kila siku 🤣🤣🤣
kaka Jitahidi Usome Ndo kitu pekee Kitakuokoa
maana Ninaamini hata Unachokiandika Hukujui vizuri ..
ILa mwanzoni ulisema Kuwa Swala ya wayahudi hakuna Kusujudu 🤣🤣
Mi naona Najenga Hoja na Mtu asiye Jua hata Anazungumza kuhusu Nini
Sheria ya Kosher na Sheria za Halal hazitofautiani hata Kidogo zote zina Msingi wa Kutoka kwenye Mambo ya Walawi 7 😁😁
Sunna Sio Ibada sunna Ni Sehemu ya Fasihi na Ni chanzo cha Sheria ya Fiqhi za Kiislamu kama Ilivyo Halakha na Agaddah kwa Talmud
Kasome kuhusu Shema Yisrael na Shofar Vizuri utajijibu swali hilo
Itoshe Kusema Kasome Dini Moja moja kabla ya Kuja hadharani na kuichambua Dini Hiyo..
Kuhusu Uyahudi Ndugu yangu Huuujui na Kuhusu uislamu Pia Huujui
Naomba Niwasilishe Kalamu
Biashara ya kuanza kuniambia Uyahudi , uislamu siujui hayo ndio mashindano unayotaka ,mimi nimejikita kwenye kujibu na kujenga hoja , wewe ndio unaonekana unataka kushindana ,maana Hadi unasema Uyahudi , uislamu siujui ni dhahiri umeanza kuishiwa hoja, wewe jikite kwenye mada tu ,
Dini na ibada ni vipengele vinavyohusiana lakini vinatofautiana. Dini ni mfumo wa mafundisho, maadili, na sheria zinazoongoza maisha ya mtu, wakati ibada ni vitendo vya kumtumikia Mungu. Biblia inasema, "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye ni lazima wamwabudu kwa roho na kweli" (Yohana 4:24), na Qur'an inasema, "Enyi watu, ibaduni Mola wenu aliyeumba mbingu na ardhi..." (Al-Baqara 2:21). Hii inaonyesha kwamba ibada ni sehemu ya dini, lakini dini inahusisha mafundisho na miongozo zaidi ya ibada pekee.
Hadithi na Sunna ni vipengele vinavyohusiana na mafundisho ya Mtume Muhammad, lakini ni muhimu kutambua kuwa Hadithi na Sunna siyo msingi pekee wa dini ya Kiislamu. Qur'an inaeleza, "Na hakika wewe (Mtume) uko katika tabia ya juu kabisa" (Al-Qalam 68:4), lakini mafundisho ya Qur'an ndio msingi wa dini. Katika Biblia, Kristo alisema: "Neno la Mungu ni kweli" (Yohana 17:17), hivyo Biblia ndiyo msingi wa mafundisho ya Wakristo na sio Hadithi pekee.
Shema Yisrael ni kauli kuu ya imani ya Wayahudi, lakini haiwezi kuwa msingi wa imani ya Waislamu. Biblia inasema, "Sikiza, Ee Israeli; Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja" (Kumbukumbu la Torati 6:4), lakini Waislamu wanatambua Shahada kama kauli kuu ya imani yao, ambayo inasema, "La ilaha illallah, Muhammadur rasulullah" (Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake). Hii inaonyesha tofauti ya msingi katika imani zao.
Wudhu ni ibada ya kutakasika kwa Waislamu, kama ilivyoelezwa katika Qur'an (Al-Ma'idah 5:6), ambapo inasisitiza umuhimu wa kutakasika kabla ya ibada. Hata hivyo, Biblia inasisitiza kutakasika kwa moyo na roho, kama inavyoonyeshwa katika Zaburi 51:10: "Nipatie moyo safi, Ee Mungu, na roho mpya iliyo thabiti ndani yangu." Hii inaonyesha kuwa katika Biblia, kutakasika ni jambo la kiroho zaidi kuliko kitendo cha nje kama ilivyo kwa Waislamu.
Sheria za Kosher na Halal zinatokana na sheria za dini hizi, lakini kuna tofauti kubwa katika utekelezaji wao. Katika Biblia, Walawi 11 inatoa sheria kuhusu chakula kilichokubalika kwa Wayahudi, kama vile marufuku ya kula nyama ya nguruwe, wakati Qur'an pia inaweka sheria kuhusu chakula kilichohalalishwa (Al-Baqara 2:173), lakini Sheria ya Kiislamu inajumuisha miongozo mingine ya kimaisha zaidi. Hivyo, ingawa kuna mfanano, kila dini ina mfumo wake wa kisheria na maadili.