Hakuna ubishi, bila biblia, hakuna uislam. Kama ukristo ungedukua na kukopi na kupaste quran, hali ingekuwaje?

Kaka ,Mimi najibu hoja wewe unasema nipo kushindana ,kwanini ....au unataka nikubaliane na unachosema hata kama naona ni uongo?

Biashara ya kuanza kuniambia Uyahudi , uislamu siujui hayo ndio mashindano unayotaka ,mimi nimejikita kwenye kujibu na kujenga hoja , wewe ndio unaonekana unataka kushindana ,maana Hadi unasema Uyahudi , uislamu siujui ni dhahiri umeanza kuishiwa hoja, wewe jikite kwenye mada tu ,

Dini na ibada ni vipengele vinavyohusiana lakini vinatofautiana. Dini ni mfumo wa mafundisho, maadili, na sheria zinazoongoza maisha ya mtu, wakati ibada ni vitendo vya kumtumikia Mungu. Biblia inasema, "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye ni lazima wamwabudu kwa roho na kweli" (Yohana 4:24), na Qur'an inasema, "Enyi watu, ibaduni Mola wenu aliyeumba mbingu na ardhi..." (Al-Baqara 2:21). Hii inaonyesha kwamba ibada ni sehemu ya dini, lakini dini inahusisha mafundisho na miongozo zaidi ya ibada pekee.

Hadithi na Sunna ni vipengele vinavyohusiana na mafundisho ya Mtume Muhammad, lakini ni muhimu kutambua kuwa Hadithi na Sunna siyo msingi pekee wa dini ya Kiislamu. Qur'an inaeleza, "Na hakika wewe (Mtume) uko katika tabia ya juu kabisa" (Al-Qalam 68:4), lakini mafundisho ya Qur'an ndio msingi wa dini. Katika Biblia, Kristo alisema: "Neno la Mungu ni kweli" (Yohana 17:17), hivyo Biblia ndiyo msingi wa mafundisho ya Wakristo na sio Hadithi pekee.

Shema Yisrael ni kauli kuu ya imani ya Wayahudi, lakini haiwezi kuwa msingi wa imani ya Waislamu. Biblia inasema, "Sikiza, Ee Israeli; Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja" (Kumbukumbu la Torati 6:4), lakini Waislamu wanatambua Shahada kama kauli kuu ya imani yao, ambayo inasema, "La ilaha illallah, Muhammadur rasulullah" (Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake). Hii inaonyesha tofauti ya msingi katika imani zao.

Wudhu ni ibada ya kutakasika kwa Waislamu, kama ilivyoelezwa katika Qur'an (Al-Ma'idah 5:6), ambapo inasisitiza umuhimu wa kutakasika kabla ya ibada. Hata hivyo, Biblia inasisitiza kutakasika kwa moyo na roho, kama inavyoonyeshwa katika Zaburi 51:10: "Nipatie moyo safi, Ee Mungu, na roho mpya iliyo thabiti ndani yangu." Hii inaonyesha kuwa katika Biblia, kutakasika ni jambo la kiroho zaidi kuliko kitendo cha nje kama ilivyo kwa Waislamu.

Sheria za Kosher na Halal zinatokana na sheria za dini hizi, lakini kuna tofauti kubwa katika utekelezaji wao. Katika Biblia, Walawi 11 inatoa sheria kuhusu chakula kilichokubalika kwa Wayahudi, kama vile marufuku ya kula nyama ya nguruwe, wakati Qur'an pia inaweka sheria kuhusu chakula kilichohalalishwa (Al-Baqara 2:173), lakini Sheria ya Kiislamu inajumuisha miongozo mingine ya kimaisha zaidi. Hivyo, ingawa kuna mfanano, kila dini ina mfumo wake wa kisheria na maadili.
 
Unasema kwa Waislamu Shabbat ni ijumaaa au nimesoma vibaya?
Sijasema Hichi kitu Nimekuambia Kuwa Maandiko ya Kiislamu ikiwemo Qurab Yanathibitisha uwepo wa Siku ya Sabato ama shabbat ambayo wayahudi Walikuwa nayo ila waliihalifu..

Nikakujibu swali lako la kwanini Hawaifati hiyo shabbati kuwa na wao walipewa Maamrisho yao ya Kufata siku ya Jumu'a ..
unajua hata maana ya Jumu'a?

mana yake Ni jumuiko So jumuua ni Jumuiko ama Kutaniko Limetokana na neno Jamaa yaani Kusanyiko

Yote haya sijayasema
Ilo unapswa wewe kusema kwakuwa nimekwisha kukujibu inafanana pote sasa wewe nionyeshe ambapo haifanani mbona ni Simple ..

Nimetoa aya na Sura isome Imeandika Vizuri sana
maswali haya yote nimeshayajibu kama unafatilia ilibidi uulize maswali yenye Msingi
Itoshe Kusema Hamis Unasafari Kubwa sana ya Kusoma Dini..
Jitahidi sana Usome dini..

Kabla ya Kusema dini hii Haifai Jitahidi Uisome sana..
Nina bahati ya Kusoma Atleast Dini Tatu..Uislamu, Ukristo (Theology yangu safi) na Uyahudi (Yeshiva)..
Japo Bado ni mwanafunzi wa Hizi dini Ila pia nasoma na dini nyingine nyingi kwa Miaka 8 sasa..

ELimu haiji hivi hivi umiza Kichwa..
...

Nitajibu maswali Yako baadhi..

Kwamba Utofauti wa Dini na Ibada..
Dini Ni mfumo Mzima wa Maisha wote Ni kama ka ratiba Fulani kuanzia unapoamka mpaka unapolala..

Ila Ibada ni Matendo unayofanya ili Kutimiza Dini yako..


Kitu ambacho nimegundua Ni Kwamba Unatumia AI kunijibu maswali yangu na unafanya hivyo Kutengeneza Maswali.. Thats why maswali yako yanajirudia halafu yanakosa Umaana wa kuuliza...
Unakuta swali.limekwisha jibiwa Kwenye Post ya Nyuma unarudia hilo hilo..

MImi naomba Nilushukuru Pale utakapoanza Kutumia Akili yako binafsi kutafakari kila swali na Kila kitu unachoandika Tutaanza Kuongea au Utanitag
 
Wewe hutaki kujibu maswali yangu ,ninachoona unalalamika tu, Mimi natumia biblia na elimu niliyoipata kwenye uislamu ,

Dini ya kiislamu inafanana na Uyahudi sehemu ndogo tu Tena kwa sababu ya tamaduni za mashariki ya kati na mambo mengine ambayo Muhammad alichota kwa wayahudi .

Huwez kusema wanafanana kwa 80% ,basi muislamu angeweza kufanya ibada kwenye dini ya kiyahudi

Sunni na madhehebu mengine ya kiislamu ndio yanafanana kwa asilimia zaidi ya 80-90 ,japo Bado wanapingana Hadi kuitana makafiri na kuuana
 
Nakuomba urejee ule mstari wa 12, ili kujua ni wapi alipo.
Sawa Sasa Nijibu maswali kadhaa..

Soma Haya Mafungu kutoka vitabu kadhaa Kisha Nijibu maswali..

Zekaria 3:1-2

" Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.

Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?"


Twende kwa Ayubu 1:6-8

"Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.

Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu."



Sasa Umeona Hayo maandiko Unasemaje Shetani alitupwa Chini wakati swali la Mungu kutola.kitabu cha Ayoub Linamaanisha anauliza Alikuwa Wapi kwa Kitokumuona Mbinguni na Ndo mana hata Alipojibu Natoka Kuzunguka Duniani Mungu hakushangaa tena aikabidi aulize Kuwa Umenionea Ayubu..

Hiyi inamaanisha kwamba Huyu Mtu hakutupwa Duniani kwa Sababu duniani huwa anakuja Kutembea..
Au Wewe Unasemaje..?
Tufate kauli y ufunuo au Kauli ya Ayoub au Kauli ya Zekaria?
 
Ok Sawa ila Kwa aliyesoma Hoja Nilizoandika Zote atakuwa amepata Kitu na aamejua hasa nini nilikuwa nazungumzia..
KAtika maisha Yangu Kitu Kilichonifanya Nijue Kijielimu kidogo sana Kuhusu Dini na Vitu Vingi..

Ni Kutokuwa na Chuki hata Chembe nilipokuwa Mkristo Sikuwa na Chuki na Wayahudi, Wamormons wala wayahudi au Waislamu wala Dini Zingine za Mythology na Mystical..
Na baada ya Kuwa Dini Hizo nilijua kwanini Wanakuwa Hivyo..
Na mpaka Sasa nawapenda Dini zote Upendo ule ule..

Sina Chuki na Ukristo, Sina chuki na Uislamu sina chuki na Uyahudi wala sina chuki Na Dini yoyote ila Hindu, Budha na Zingine zote Zina shina Moja
 
Hata Mimi Sina chuki na dini yoyote ,na Ukristo unafundisha hivo ,

Tukubaliane kutokubalina ,Mimi nashukuru nimejifunza pia vitu vingine kutoka kwako
 
Ndio mjue kuwa Mungu fundi alitaka wakati anapewa utume awe brain washed Ili nyinyi makafiri msije mkasema alikopi na kupest Kwa kuwa alikuwa msomi
Ningekubali kwamba haku copy kama angekuwa kiziwi
 

Nina majibu ya hayo maswali yote.
Lkn kitu ambacho nimegundua kinakupa shida ni chronological order of the Bible. Joshua aliambiwa hayo kwenye kipindi cha kale, ambacho shetani na majeshi yake yalikuwa huru kwenda kokote ambako wanataka. Lakini kutoka kwenye kitabu cha mwisho cha biblia cha ufunuo kwa Yohana. Ndiyo, ni maono ambayo Mungu alimfunulia Yohana. Kwenye lile fungu la 12, inaonesha wazi kwamba shetani alifukuzwa na hakuruhusiwa tena kurejea mbinguni kama alivyokuwa akifanya hapo awali. Kama unakumbuka majeshi ya shetani kabla ya gharika ya Nuhu walikuwa duniani na walikuwa na uwezo wa kuoa na kuzaa watoto na mabinti wa kibinadamu. Lakini gharika ilivyokuja wakapaa mbinguni, lkn wengine wote wakagharikishwa. Lkn that time around kulingana na fungu la 12 alifukuzwa na hana uwezo tena wa kurudi mbinguni. Na ndiyo maana ana ghadhabu kali kwa maana kafukuzwa mbinguni na pia anajua hapa duniani pia atamalizwa.
 
Hili ni swali Nililouliza mwanzoni kabisa kabla ya Mjadala kuanza..
Na wewe Nitakuuliza Tena Shetani alifukuzwa Lini Mbinguni?

Ni baada ya Kuumbwa Mwanadamu Kabla ya Kuumbwa mwanadamu au Ni baada ya Mwanadamu kuasi au Ni kipindi cha Yoshua au Yesu au ni lini hasa alifukuzwa..

Natamani nipate Idea tofauti
 
Mkuu kama umeshindwa kutofautisha kati ya sunna na hadithi na badala yake ukaandika hadithi/sunna hiyo inaonesha huna elimu yoyote uliyoipata kwenye uislam.
 
Mkuu kama umeshindwa kutofautisha kati ya sunna na hadithi na badala yake ukaandika hadithi/sunna hiyo inaonesha huna elimu yoyote uliyoipata kwenye uislam.
Samahani kama kuna makosa au kutokuelewana katika maelezo yangu. Ili kufafanua, tofauti kati ya Hadithi na Sunna ni muhimu sana katika Uislamu

Hadithi hizi ni ripoti au masimulizi ya maneno, matendo, au idhini ya Mtume Muhammad (SAW) kama ilivyosimuliwa na maswahaba wake na kuripotiwa na wasimulizi mbalimbali. Hadithi zina daraja tofauti (sahihi, dhaifu, hasan n.k.) kulingana na uhakika wa mnyororo wa wapokezi.

Sunna hiz mwenendo au njia ya maisha ya Mtume Muhammad (SAW), ambayo ni kielelezo cha utekelezaji wa Uislamu kwa vitendo. Sunna inajumuisha matendo yaliyopitishwa au kurithiwa kutoka kwa Mtume (SAW) na mara nyingi hutegemea Hadithi kuthibitisha asili yake.



Kwa kifupi Hadithi ni chanzo cha Sunna, lakini Sunna ni mwongozo wa jumla wa maisha ya Kiislamu unaotokana na matendo ya Mtume (SAW).

Ikiwa kuna hoja au maoni yanayohitaji ufafanuzi zaidi, niko tayari kujifunza na kujibu.
 

Shetani alifukuzwa mbinguni na Yesu miaka mingi sana baada ya mwanadamu kumuacha Mungu. Pia baada ya Yesu kufa. Hivyo alifukuzwa miaka mingi cha Baada ya Kristo kufa na kufufuka na kurudi mbinguni.
 
Shetani alifukuzwa mbinguni na Yesu miaka mingi sana baada ya mwanadamu kumuacha Mungu. Pia baada ya Yesu kufa. Hivyo alifukuzwa miaka mingi cha Baada ya Kristo kufa na kufufuka na kurudi mbinguni.
Sijakuelewa Lini Shetani alifukuzwa na Yesu?
Sijaelewa Ulichoandika kabisa hebu Jitahidi kama Utaweza unielewwshe zaidi..
 
Quran Imeandikwa Kwa mtindo wa Ushairi labda kama Unataka Kubishana na Huyo Member Mkuu!

Huwa nachukia sana kuona watu wanaandika mambo ambayo hamna elimu nayo. Huu ujasiri sijui mnautoa wapi aisee ?

Kuna muda huwa tunakaa kimya sababu kama hizi. Nakupa miaka yote mpaka unakuta huwezi kuleta ushahidi ya kuwa Qur'an imeandikwa katika mtindo wa mashairi.

Una elimu yoyote juu ya mashairi ya Kiarabu ? Acheni ujinga vijana, mnaita hasira sana, muda ambao haya mambo yako wazi.

Hao waarabu wenyewe ambao walikuwa wanadai ya kuwa Qur'an ni mashairi walishindwa kuthibitisha hilo, halafu unakuja wewe mjinga mmoja ambaye hata Elimu ya Arudhi na kawafi huna.

Nikuwekew mashairi ya Kiarabu na aya za Qur'an ulinganishe ?
 
Yesu Hakuwa Muislamu Alikuwa Myahudi

Hilo tatizo lingine, unajua kama Uyahudi ni Ukafiri ? Vipi Yesu awe Myahudi ? Unajua maana ya tamko Uyahudi au dini ya Uyahudi ?

Unajua Uyahudi kama dini imeanza lini ?
 
YESU hajawahi kuwa muislamu,alikuwa dini ya kiyahudi , Uislamu umekuja mwaka 622 hapo

Msidanganywe ,

Uislamu hujui, hili la kwanza. Uislamu umegawanyika sehemu kuu mbili :
1. Uislamu wa ujumla, ambao ndio manabii na mitume wote dini yao ni Moja.

2. Uislamu alio kuja nao Mtume Muhammad, huu ni tofauti kwa sababu ya Sheria tu ila Imani ni Moja kwa mitume wote na manabii wote.

Hivi unaujua Uyahudi lakini au unaandika tu. Yaani kwa akili yako tu ya kawaida, Mtume wa Allah awe Myahudi yaani kafiri aliye potea ? Hivi marejeo yenu ya haya mnayo yaandika huwa ni wapi ?
 

Kabla ya Mtume Uislamu ulikuwa katika msingi wa kumuabudu Allah pekee na kuwapiga vita washirikina na hali zao zote. Na ndio Uislamu ambao tuko nao mpaka Kiama kinasimama.

Imetufikia juu ya vitabu vitabu vinne na msahafu wa Ibrahimu. Kwa maana Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an ndio kitabu Cha mwisho. Vitabu vyote vimepotea na hakuna nakala yoyote iliyo bakia kwa Sasa, isipokuwa Qur'an pekee.

Majengo ya ibada yalikuwa katika miji yao.

Sijui kwa mtindo upi, ila Musa alikuwa ana fanya ibada kutwa mara mbili. Hao wengine sijui walipewa muongozo gani juu ya ufanyaji wao wa ibada.

Usiseme hakuna ushahidi, sema wewe hujui hili. Labda nikuulize marejeo yako ya Historia ni wapi ? Tuanziw hapo, au ukitaka kujua matukio ya kihisitoria unaangalia machimbuko gani ?
 
Wewe ni lofa wa elimu, hakuna kitabu kukizidi quraan, pia torati, zaburi na injili ni sehemu ya maneno ya Allah, na vilikua kwa sehemu maalum tofauti na Quran ni applying kwa dunia nzima
 
🤣🤣🤣.kwa hyo Muhammad Ali weka kwenye utumie na roman Catholic.
Vichekesho hivi.
Sasa je
Monk Bahira na Waraqa bin Nauf si ndio waliompa utume Mohammad Abdula bin Mutalib?
Mbona ipo wazi hao ma priest ndio walifanya manuva jamaa aweze kuiunganisha Jamii ya Quraish Ili watawaliwe kwa kupitia Dini mpya Islam!

Haya hawawezi kukufundisha ukafunguka akili kua Uislamu ni moral and dogma za waarabu!
 
Kama vitabu vilipotea nyie mlijuaje kua kuna vitabu vinaitwa Torati,Zaburi,injili na hivyo vitabu walipewa mnaowaita waislamu ambao kimsingi Uislamu ulianzishwa na Mohammad Abdula bin Mutalib?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…