Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la leo

Hii ni makala yangu ya pongezi kwa Wakili Mwabukusi kuchaguliwa kuwa rais wa TLS, na kumpa ushauri wa bure, aibadili TLS kutoka kule juu ilipo, aishushe chini ground zero Ihudumie wananchi wa kawaida wanaohitaji huduma za kisheria, badala ya kuhudumia wanachama wake tuu.

Kwa vile yeye ni Mwanaharakati, namuomba sana, chonde chonde asituletee uana harakati wake kwenye TLS yetu , TLS sio chama cha siasa, sio chama cha ki harakati, TLS ni a Professional Body.

Hapa naomba kumtumia rais wangu wa TLS, rais wa r ndogo, Salaam rais wangu Mwanaharati Wakili Boniphase Mwabukusi, kutoka kwa Rais wa R kubwa, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kuhusu TLS ya chama cha wanasheria na TLS ya chama cha kiharati
View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=Fkur0u0qguoovPMoIla pia naishauri Serikali yetu tukufu na mihimili yake ya Bunge na Mahakama, sasa ikae mguu sawa, usiempenda kaja!, lazima ijifunze kusikiliza na kuwa sikivu kwa hoja za kiprofesheni za kisheria za TLS, kwasabu kwa hapa tulipo, tumeshuhudia, Serikali, Bunge na Mahakama Kiburi na Jeuri, yenye Madharau kuidharau TLS na hoja za TLS baada ya kufanikiwa kuwachomeka machawa wake kwenye uongozi wa juu wa TLS, hivyo kuiweka TLS mfukoni!.

Lakini safari hii, sisi wanasheria mawakili tunaotaka mabadiliko, tumewagomea kutupandikizia viongozi vibaraka, na kuamua kumchagua mtu independent, jasiri na mwanaharakati Mwabukusi, hivyo vyombo hivi vikiendeleza ile tabia yake mbaya ya kiburi na jeuri, this time around, watakula jeuri yao!, Mwabukusi sio mtu wa mchezo mchezo, wakileta zile za kuleta, hachelewi kuwapelekea moto na kuwawasha!.

Wiki hii, kumefanyika uchaguzi wa chama cha mawawili Tanzania, TLS, mmoja wa wagombea, alikuwa ni mtu “asietakiwa” (naomba nisiseme asietakiwa na nani), lakini zilifanyika juhudi mbalimbali kumkwamisha asigombee, Mahakama ndio ikaokoa jahazi kwa kumtendea haki, huyu si mwingine ni Wakili Msomi, Boniface Mwabukuzi, ambaye amechaguliwa kwa kishindo, hivyo sasa “usiemtaka kaja”, itakuwaje?.

Hivyo mimi mwandishi wako wa makala hizi, nikiwa pia ni mwanasheria, wakili na mwanachama wa TLS, pia nimeufurahia ushindi huu, nikiamini ni Mungu ndio amewezesha, kuna jambo la kisheria Mungu anataka kulifanya kwa watanzania, baada ya serikali yetu tukufu, kushindwa kulifanya tangu tulirejesha mfumo wa vyama vingi.

Ushindi wa Mwabukusi umepokelewa na vifijo na nderemo ukumbi mzima, hivyo unatuma ujumbe mzito kwa waliokuwa hawamtaki Mwabukusi kuwa sasa ndio yeye, ndiye kaja.

Mimi kama mwanachama wa TLS, sio mara moja au mbili, nimeeleza kupitia maandiko yangu mbalimbali jinsi TLS inavyonyamazia madudu ya kisheria yanayofanywa na serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu.

Kwa vile mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TLS alipangwa awe Rais Samia, mimi niliwaandikia Waraka TLS, wamwambie nini Rais Samia Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi
Hii ni sehemu ya waraka huo.

Hii maana yake ni Chama cha Mawakili Tanzania, TLS, kinaadhimisha miaka 70!, hiki ni moja ya vyama vikonge kabisa vilivyoanzishwa hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru.

Kwenye Majukumu ya TLS, mimi naomba kujikita kwenye jukumu moja tuu, "to support the State Organs in legislation and administration of justice and the rule of law" kuisaidia serikali kwenye utungaji wa sheria na utawala wa sheria.

Kabla sheria yoyote haijatungwa, TLS kama wadau wa sheria, inapitishwa kwao, TLS wanatupa wanachama wao wote, fursa ya kutoa maoni, kisha TLS, wanapeleka maoni yake ya kisheria, ndipo sheria inatungwa.

Ushauri wangu wa kwanza kwa Wakili Mwabukusi, kwa vile hakuna ubishi kumhusu yeye kuwa ni mwanaharakati, ombi la kwanza, asiigeuze TLS kuwa TLS ya kiharakati, TLS ni profesheno body, lazima ifanye mambo yake ki profeshenali na sio kiharakati.

Kitu cha pili, aibadili TLS kutoka kuwa chama cha mawakili wasomi, kugeuka ni taasisi ya kuwahudumia wananchi, hivyo aishushe TLS took huko juu ilipo, aiteremshe chini kwa wananchi ikiwemo matumizi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwenye tovuti yake, kw asana ni kimombo tuu!.

Tangu nimejiunga TLS kuwa mwanachama wao, nomekuwa nahudhuria vikao vya kukusanya maoni ya TLS kuhusu ule mkataba wa IGA ya DPW na Bandari zetu, nikaipongeza TLS kwa maoni yake mazuri ya kisheria kwa mkata ule, , lakini pia nikauliza swali Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya? . TLS ya Mwabukusi, hili sio la kulinyamazia.

Yakaja mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, kama kawaida TLS ikatoa fursa kwa sisi wanachama wake kutoa maoni yetu, siku ya siku serikali ikaitisha kikao kupokea maoni, TLS wakatoa maoni yake, serikali ikayapuuza na TLS wakanyamaza!. TLS ya Mwabukusi, tukitoa maoni ya kisheria kwa serikali yetu, isipotusikilize, tusinyamaze, tuibananishe kisheria.

Ubatili wa Katiba na Ubatili wa Sheria, na Kilio cha Haki
Kwa muda mrefu, nimekuwa nikipigia kelele ubatili wa katiba yetu, na ubatili wa sheria zetu uliopoka haki. kuu ya mzingi, haki ya kuchagua na kuchaguliwa iliyotolowe na ibara ya 5 ya katiba, inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kuchagua viongozi anaowapenda kwa kuwapigia kura, na ibara ya 21 inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kushiri kwenye kwenye serikali, toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu kwa haki ya kugombea uongozi, lakini haki hizo kuu mbili, zikaja kupokwa na ibara ya 39 na 63, zilizochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, ambazo zinakwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa katiba yetu hii yenye ubatili, ile haki ya kuchagua yaani haki ya kupiga kura kumchagua kiongozi yoyote unayempenda imepokwa na kukasimiwa kwa vyama vya siasa, kuwa Mtanzania hayuko huru tena kumchagua kiongozi anayemtaka, analazimishwa lazima amchague kiongozi aliyepitishwa na chama cha siasa. Na kwenye kugombea uongozi, Mtanzania hana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21, ili Mtanzania kugombea uongozi, analazimishwa, lazima ajiunge na chama cha siasa, hicho chama kimdhamini ndipo aruhusiwe kugombea!

Marais Sio Wanasheria, Wanaijua Katiba
Japo Marais Wetu Sio Wanasheria, Lakini Katiba Wanaijua, Kati ya Marais wote watano wa Tanzania, ni Rais Mwalimu Nyerere Pekee, Ndiye Aliitambua Haki hii imepokwa, Wanasheria Tumweleze Rais Samia, Airejeshe na kutuondolea ubatili huu ndani ya Katiba yetu.

Hili la ubatili wa katiba ni jambo kubwa na very serious, kabisa ambalo TLS ilibidi, wa deal nalo toka pale mahakama kuu iliutamka ubatili huo wa katiba na sheria hiyo ya TLS yetu ilinyamaza, TLS ya Mwabukusi, hili sio la kulinyamazia.

Naiomba sana TLS ya Mwabukusi iwe makini sana kwa kujipusha na uanaharakati, rudia tena kuusikiliza huu msimamo wa Rais Samia, kwa wanasheria wanaharakati wakileta za kuleta, na yeye atatumia sheria hizo hizo kuwabananisha.
Rudia kumsikiliza
View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=Fkur0u0qguoovPMo
Tunaomba TLS ya Mwabukusi isiturudishe huko. Tunaomba tujikite kwenye profeshenolizimu Hivyo ujio wa rais Mwabukusi hii miaka 70 ya TLS ni fursa, kwa TLS kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kuwawezesha Watanzania wapate haki zao zilizoporwa kipindi kirefu.
Kwa heri Wakili Harold Sungusia, Karibu Wakili Mwabukusi

Mungu Mbariki Mwabukusi,

Mungu Ibariki TLS

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
Harakati zina tatizo gani?
Hakuna tatizo lolote kwa mtu kuwa mwanaharakati kwasababu harakati hazina tatizo kwa taasisi za ki harakati, TLS sio taasisi ya kiharakati, its a professional body. Professional bodies zinaendesha mambo yake professionally na harakati ndio zinaendeshwa ki harakati.
Mwana harakati kama Mwabukusu anapochaguliwa kuendesha a professiona body, there is a very thin line kati ya professionalism and activism!.
P
 
Sema we jamaa una kaujuaji Fulani ka kishamba.
Kuhusu ushamba, sisi watu wa kanda ile ni washamba sana.
BAK is far better than you.
Kwani kuna mashindano humu who is good, better and best? kila mtu ana maeneo yake ya kujidai, ni kila mtu is good, better and best depends ni kwenye nini, yes anaweza kuwa better than me, lakini na mimi ni better kuliko mwingine!, hata kwenye top ten, wa kumi ndie wamwisho but is better than wa 11 etc,
P
 
Harakati ni nin?
Mwanaharakati ni mtu wa aina gani?
Naomba msaada
Pia ntafarijika nikijua faida na hasara za kua mwana wa harakati kwa jamii...
 
kama ulikuwa haujui, wanasheria wote ni wanaharakati, na hawana mwanaume wala mwanamke.wote ni wanaharakati. ndio maana walipigiwa kampeni na pengine kupewa hadi pesa wapige kinyume na mwabukusi wakawa wanawazoom tu, pesa walichukua na kura wanajua watakakozipeleka. usifanye mchezo na mwanasheria, tunajuana sisi wenyewe.
 
Kwahiyo na huyu kumbe alimpa boss kura yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…