Elections 2010 Hakuna uchaguzi mkuu Tz 2010

Elections 2010 Hakuna uchaguzi mkuu Tz 2010

Emma M.

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
204
Reaction score
6
Nikama hakuna uchaguzi mkuu Tz 2010 kwani kilichopo ni kuthibitisha wana CCM watakao endelea kuitafuna Tanzania.
Mwezi October na Novemba utasikia hivi CCM IMESHINDA KWA KISHINDO.
Kikwete rais tena.
Hata magazeti yaweza kuanza kuandika kuhusu matokeo sasa na kusave kwenye computers zao ili yatolewe rasmi wakati huo.
 
Ebo.Mimi nilidhani una hoja za msingi kumbe porojo tu...CCM haiwezi kushinda kwa kishindo mwaka huu.
 
Ebo.Mimi nilidhani una hoja za msingi kumbe porojo tu...CCM haiwezi kushinda kwa kishindo mwaka huu.

Nilidhani utajiamini na kusema CCM haiwezi kushinda! Lugha yako na ya mtoa hoja ni lugha za kukata/kukatisha tamaa. Tuanze kusema hivi "CCM ITASHINDWA!" Sababu za kushindwa CCM zinajulikana wazi - wameshindwa kuleta "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" kama walivyoahidi kwenye uchaguzi uoliopita. Walitudanganya ili tuwape kura. Safari hii hatudanganyiki! Huo ukiwa ndio msimamo wa kila mnyonge asiyejua kesho atakula nini na wanawe; asiyeweza kwenda hospitali kupata matibabu kwa sababu hana fedha za kununulia hata asprin ambayo haipatikani kwenye vituo vya afya; asiyeweza kununua dawati analodai Mkuu wa Mkoa Lukuvi linunuliwe; aliyepoteza nduguye/mwanawe albinoni kutokana na imani potofu za ushirikina na hakuna kiongozi yoyote aliyekuwa tayari kuwajibika kuonyesha Serikali ya CCM inajali; wananchi wa Mpanda na sehemu zingine wanaonyemelewa na njaa kwa kuwa mazao yao yameliwa na nzige ambao wangeliweza kuondolewa haraka iwapo Serikali ya CCM ingekumbuka kununua ndege za kunyunyuzia dawa za kuua wadudu badala ya kununua migari mnyeusi ya kifahari; ....... Wananchi wakiwa makini na tafakari yote hayo na vyama vya upinzani vikikazana kuwakumbusha wananchi juu ya hayo na mengine mengi ni dhahiri CCM Itashindwa!
 
Imani bila matendo ni bure.
Hakuna dalili za CCM kushindwa, kwani hakuna dalili za chama kingine KUSHINDA.
 
Emma nadhani wewe ni Mamluki! Unashirikiana na Mafisadi ii nini? maana wewe ndio wale hata Hamtamani Kumsifu Mtu Kama Dr Slaa. Ambaye Wabunge Wote Walipendekeza wajiongezee Poshe yeye akapinga. Wakamchukia au Humfagilii Mtu kama Magufuri Kwa utendaji wake Mzuri wa Kazi
 
Huwa nahisi kichefuchefu nisikiapo 'kitu' kama vile CCM! Aagh...! Hata kuitaja naona kero. Yani sijui wametuona watoto wadogo, kutupa ahadi za uongo. Eti 'maisha bora kwa kila mtanzania'. Mara 'ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya'. Labda kasi ya kujaza matumbo yao! Lakini naamini mwisho wao umefika, kwani 'hakuna marefu yasiyo na ncha' vilevile 'kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho'. 2010 PATACHIMBIKA!.. We ngoja tu!
 
ghaaaaaaaaa ghaaaaaaaaaaaa ghaaaaaaaaaa, nimetapika kuku wangu na chipsi nilipofungua thread hii na kuona bado kuna watu wanaodhani CCM ni chama cha kidemokrasia so kitashinda uchaguzi wa 2010. Kama Mwenyekiti wa CCM ndio yule aliyekua anaongea jana na wazee WA DSM hiki chama ni cha kupigiwa kura ya HAPANA.CCJ ndio mkombozi wetu.
 
Nilidhani utajiamini na kusema CCM haiwezi kushinda! Lugha yako na ya mtoa hoja ni lugha za kukata/kukatisha tamaa. Tuanze kusema hivi "CCM ITASHINDWA!" Sababu za kushindwa CCM zinajulikana wazi - wameshindwa kuleta "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" kama walivyoahidi kwenye uchaguzi uoliopita. Walitudanganya ili tuwape kura. Safari hii hatudanganyiki! Huo ukiwa ndio msimamo wa kila mnyonge asiyejua kesho atakula nini na wanawe; asiyeweza kwenda hospitali kupata matibabu kwa sababu hana fedha za kununulia hata asprin ambayo haipatikani kwenye vituo vya afya; asiyeweza kununua dawati analodai Mkuu wa Mkoa Lukuvi linunuliwe; aliyepoteza nduguye/mwanawe albinoni kutokana na imani potofu za ushirikina na hakuna kiongozi yoyote aliyekuwa tayari kuwajibika kuonyesha Serikali ya CCM inajali; wananchi wa Mpanda na sehemu zingine wanaonyemelewa na njaa kwa kuwa mazao yao yameliwa na nzige ambao wangeliweza kuondolewa haraka iwapo Serikali ya CCM ingekumbuka kununua ndege za kunyunyuzia dawa za kuua wadudu badala ya kununua migari mnyeusi ya kifahari; ....... Wananchi wakiwa makini na tafakari yote hayo na vyama vya upinzani vikikazana kuwakumbusha wananchi juu ya hayo na mengine mengi ni dhahiri CCM Itashindwa!

nimetafuta pa kukuthank nikakosa! asante, watanzania tuungane kuchagua kiongozi atakaeboresha maisha ya mtanzania
 
Jamani ukweli ni lazima usemwe kwa rangi yake hata kama ni ile ya kaniki ambaye haivutii sana ni lazima usemwe tu! ndio ni wengi hatutaki kuyakubali matokeo haya na hata mimi sipendi kuyatabiri, lakini ni wazi CCM watashinda 2010 japo sio kwa HAKI, ila hat Dr Slaa alisema juzi kama kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki na kutakuwa na uwanja sawa wa uchaguzi CCM haikatizi 2010. Lakini wasiwasi wangu ni kuwa siuoni huo uwanja sawa wa uchaguzi 2010, na kwa mbinu zao chafu chama cha "Muungwana" kitashinda tu
 
CCM itashinda kwa kishindo cha HAKI, Au wapi kuna HAKI? CHADEMA?
 
Emma nadhani wewe ni Mamluki! Unashirikiana na Mafisadi ii nini? maana wewe ndio wale hata Hamtamani Kumsifu Mtu Kama Dr Slaa. Ambaye Wabunge Wote Walipendekeza wajiongezee Poshe yeye akapinga. Wakamchukia au Humfagilii Mtu kama Magufuri Kwa utendaji wake Mzuri wa Kazi

Kwani Magufuli CCJ?
 
CCM itashinda kwa kishindo cha HAKI, Au wapi kuna HAKI? CHADEMA?

Siwezi sina for sure kama Chadema kuna haki au la, ila ambalo naweza sema kwa uhakika kabisa tena kifua mbele (kama nimedundwa ngumi ya mgongo) ni kuwa ndani ya CCM hakuna HAKI wala Demokrasia na hili wote tunajua. HAKI tunayosema hapa si ile iliyoko au isiyokuwepo ndani ya vyama vya siasa, tunasemea HAKI kwa maana ya mazingira sawa ya uchaguzi, kupiga kampeni bila vitisho, bila rushwa, bila kutumia magari na vyombo vya habari vya serikali kwa manufaa ya chama kimoja, na pia kuwe na mazingira Huru ya kupiga, kuhesabu na kutangaza matokeo! lakini kwa Tume hii ya uchaguzi iliyopo ( ambayo for sure ipo kwa ajili ya Chama Cha Muungwana) sioni hayo yote kutokea, ndio maana ninasema CCM watashinda kwa ushindi wa kutengeneza!
 
Jamani CCM haina mpinzani mwaka huu.
Nyie jipeni moyo tu.
 
Back
Top Bottom