Nilidhani utajiamini na kusema CCM haiwezi kushinda! Lugha yako na ya mtoa hoja ni lugha za kukata/kukatisha tamaa. Tuanze kusema hivi "CCM ITASHINDWA!" Sababu za kushindwa CCM zinajulikana wazi - wameshindwa kuleta "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" kama walivyoahidi kwenye uchaguzi uoliopita. Walitudanganya ili tuwape kura. Safari hii hatudanganyiki! Huo ukiwa ndio msimamo wa kila mnyonge asiyejua kesho atakula nini na wanawe; asiyeweza kwenda hospitali kupata matibabu kwa sababu hana fedha za kununulia hata asprin ambayo haipatikani kwenye vituo vya afya; asiyeweza kununua dawati analodai Mkuu wa Mkoa Lukuvi linunuliwe; aliyepoteza nduguye/mwanawe albinoni kutokana na imani potofu za ushirikina na hakuna kiongozi yoyote aliyekuwa tayari kuwajibika kuonyesha Serikali ya CCM inajali; wananchi wa Mpanda na sehemu zingine wanaonyemelewa na njaa kwa kuwa mazao yao yameliwa na nzige ambao wangeliweza kuondolewa haraka iwapo Serikali ya CCM ingekumbuka kununua ndege za kunyunyuzia dawa za kuua wadudu badala ya kununua migari mnyeusi ya kifahari; ....... Wananchi wakiwa makini na tafakari yote hayo na vyama vya upinzani vikikazana kuwakumbusha wananchi juu ya hayo na mengine mengi ni dhahiri CCM Itashindwa!