Hakuna usiri wowote kwenye mitandao ya simu ndio maana hata sauti za akina Nnauye na Makamba zilivujishwa. Tusikuze mambo!

Hakuna usiri wowote kwenye mitandao ya simu ndio maana hata sauti za akina Nnauye na Makamba zilivujishwa. Tusikuze mambo!

Kama unadhani kwenye mitandao ya simu kuna usiri mkubwa basi utakuwa unajidanganya sana bwashee.

Popote duniani kipaumbele ni usalama wa jamii kupitia njia za mawasiliano.

Muhimu ni watu kutenda matendo mema, basi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Vipi yule Mkulima wa Karoti shahidi no3 ataleta call logs za WhatsApp kutoka kwa Mark Zuckerberg ?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Usiri upo sema kwenye nchi kama zetu ambazo hazizingatia sheria hakuna anaeweza kuzingatia hilo la haki ya faragha
Hakuna cha faragha mkuu. Usalama wa nchi kwanza, ndiyo maana vikatengenezwa Vifaa vya Interceptor. Najua hujui ila kuna siku utajua ukibarehe akili zako.
 
Kama unadhani kwenye mitandao ya simu kuna usiri mkubwa basi utakuwa unajidanganya sana bwashee.

Popote duniani kipaumbele ni usalama wa jamii kupitia njia za mawasiliano.

Muhimu ni watu kutenda matendo mema, basi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
tusiwe wajinga kiasi hicho faragha ya mtu ni kitu muhimu sana
 
Kama unadhani kwenye mitandao ya simu kuna usiri mkubwa basi utakuwa unajidanganya sana bwashee.

Popote duniani kipaumbele ni usalama wa jamii kupitia njia za mawasiliano.

Muhimu ni watu kutenda matendo mema, basi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Hakuna usiri popote duniani,taarifa zako zipo salama tu,inategemea nani anazitaka,kama nazitaka mie chinga hapo itakuwa vigumu kuzipatia,lakini kama taasisi za kiusalama za serikali wanazitaka,zitapatikana tu,overtly or covertly(mbinu za wasiojurikana).
Juzi nilikuwa nasoma story ya rubani captain wa jeshi wa Iran aliyekimbilia Uturuki kuomba hifadhi,wanausalama wa Iran walioanza kumsaka,Majasusi wa Uturuki walimpa kifaa ambacho kinaweza kufatilia mawasiliano ya whatsaap,sms,calls nk.mwishowe hao majasusi wa Iran walikamatwa kama kuku,na huyo rubani sasa hv amewekwa sehemu salama zaidi.
Sasa Kuna watu wanafikili whatsaap calls zipo salama,haziwezi dukuliwa,wanajidanganya.
 
acha zivuje ili tuwajue wanafiki na wahuni...
inashangaza hawa wanaopinga tigo kuweka wazi data za uhalifu, mlitaka wafiche il iweje?? hata kama ni mimi nmemkosea mtu, akichukua data zangu mitandaoni na kunishitaki sio kosa, maana ni sehemu ya ushahidi, na makampuni yote ya mitandao yako chin ya serkali, kwa hiyo ninyi pinga pinga Fc muache kuwaficha wahalifu,

alafu mujuwe kuwa hata mkisusia tigo kwa kuvunja laini mujue kuwa hakuna mnaemkomoa zaid zaid mnajionesha mlivyo na akili chafu, yaan wew uharbu lain ya tigo ukitegemea kuwakomoa ambao wanawateja zaid ya mamilion? na kila siku wateja wapya wanaongezeka, acheni utoto.
 
Kama unadhani kwenye mitandao ya simu kuna usiri mkubwa basi utakuwa unajidanganya sana bwashee.

Popote duniani kipaumbele ni usalama wa jamii kupitia njia za mawasiliano.

Muhimu ni watu kutenda matendo mema, basi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Hii haina ubishi

Hakuna siri yoyote inayoweza kupewa kipaumbele na kuzingatiwa zaidi ya usalama wa jamii, taifa na dunia.

Tuwe makini kwa lolote tunalofanya popote pale mitandaoni maana kuna nyakati hufika na yalifichwa hudhihirika.

Tunaweza fanya upuuzi na masihara yote kwa malengo yoyote lakini siku zote tuzingatie usalama wa jamii kwanza!!
 
acha zivuje ili tuwajue wanafiki na wahuni...
inashangaza hawa wanaopinga tigo kuweka wazi data za uhalifu, mlitaka wafiche il iweje?? hata kama ni mimi nmemkosea mtu, akichukua data zangu mitandaoni na kunishitaki sio kosa, maana ni sehemu ya ushahidi, na makampuni yote ya mitandao yako chin ya serkali, kwa hiyo ninyi pinga pinga Fc muache kuwaficha wahalifu,

alafu mujuwe kuwa hata mkisusia tigo kwa kuvunja laini mujue kuwa hakuna mnaemkomoa zaid zaid mnajionesha mlivyo na akili chafu, yaan wew uharbu lain ya tigo ukitegemea kuwakomoa ambao wanawateja zaid ya mamilion? na kila siku wateja wapya wanaongezeka, acheni utoto.

Na sio tigo tuu....
Hakuna kampuni isiyozingatia usalama wa taifa kwanza
 
Na sio tigo tuu....
Hakuna kampuni isiyozingatia usalama wa taifa kwanza
Uko sahihi hata posta tu ukituma barua au kifurushi lazima kipitie process usije kuwa unasafirisha bomu .

Dk mondlane Raisi wa kwanza Msumbiji aliuawa na bomu lililokuwa kwenye kifurushi Cha posta alichotumiwa kufungua tu likalipuka

Kwa hiyo mawasiliano ya Simu kampuni zote huajiri wanausalama wa kufa mtu Kama hawana huwaazima serikalini ili kampuni zao zisije futiwa usajili au kuwa black listed Kama facilitators wa uhalifu na ugaidi

Kifupi Wana Usalama wabobezi wako kibao kampuni za simu serikali inajua na kampuni za simu zinajua

Cha msingi tumia mitandao ya Simu vizuri ila Kama mhalifu au gaidi kudakwa nje nje uwe Tanzania au nje ya nchi . Usalama wa mtu mzuri upo sana ila wa mhalifu na gaidi mhatarisha Usalama wa nchi Usalama wake wa privacy ni zero
 
Usiri upo sema kwenye nchi kama zetu ambazo hazizingatia sheria hakuna anaeweza kuzingatia hilo la haki ya faragha

Kuna nchi yoyote ambapo haki ya faragha inazingatiwa zaidi usalama wa nchi!? Yaani, kuna sheria ya faragha itakayopewa kipaumbele hata taifa liingie kwenye matatizo?

Basi kungekua hakuna hata sababu ya kuwa na regulations
 
Kama unadhani kwenye mitandao ya simu kuna usiri mkubwa basi utakuwa unajidanganya sana bwashee.

Popote duniani kipaumbele ni usalama wa jamii kupitia njia za mawasiliano.

Muhimu ni watu kutenda matendo mema, basi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Crap.

Out of content. Inashangaza mtu analeta mada ambayo haihusiani na jambo ambalo watu wanahoji.
 
Nadhani shida kubwa ni kutofuata masharti ya mkataba kati ya hayo makampuni na wateja wao na pia maadili ya kazi. Nchi zinazofuata utawala wa sheria usiri kati mteja na kampuni fulani unaweza tu kuvunjwa endapo mteja anajihusisha na vitendo vya kihalifu na ili iwe hivyo ni lazima kuwepo na 'court order' kwa service provider kutoa ushirikiano wa mawasiliano ya huyo mteja na hakuna njia nyingine yeyote ya kupata habari za uhusikaji wake kwenye huo uhalifu na hiyo court order hutolewa baada ya 'full public hearing'. Kwa mantiki hiyo, mere police order is not enough.
Mleta mada ni mbumbumbu. Haelewi hata kile ambacho watu wanahoji.
 
Siyo popote duniani unaweza kupewa siri za mteja wa simu kinyemela acha uongo!!! Nchi nyingi za Magharibi ni lazima uwe na court order ya kupewa info hizo na kampuni husika na kampuni husika inaweza pia kwenda mahakamani ili kupinga court order hiyo katika kulinda integrity ya kampuni zao na privacy ya customers.

Back
Top Bottom