Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Imani za kichawi zimetoka Afrika

Imani za kiungu zimetoka Asia na ulaya

Ila waafrika kwenye uchawi tunazingua sana aisee yani mpaka dini wanahubiri uchawi

Ukipata maendeleo ni uchawi

Ukikosa maendeleo ni uchawi

Yani uchawi uchawi uchawi kila mahali
 
Hebu relate hiyo content na utajiri tuone mtu anatajirikaje hapo

Uganga wa miti shamba sio uchawi miti shamba inathibitika kisayansi uchawi upo kiimani na kiroho
 
Waooh what a testmony...
Tena inayomuhusu mama yako...
Ndio mama mzazi lkn ameshaacha kutibu. Juzi nimempigia cm kumuuliza Kama Kuna mtoto aliwahi kufariki wakati wa tiba zake akadai ndio lkn ni mtoto mmoja tu toka aanze kuwatibu but anadai mtoto yule hakufariki kutokana na tiba yake mama Bali alikuwa na tatizo lingine hahahah!
 
Hebu relate hiyo content na utajiri tuone mtu anatajirikaje hapo

Uganga wa miti shamba sio uchawi miti shamba inathibitika kisayansi uchawi upo kiimani na kiroho
Iko hivi: upande wa mama hakuwa akiwachaji pesa nyingi ilikuwa Ni Kama msaada tu. Lkn tukisema kwa ishu yakutajirika sijui kiundani but kinachoshangaza Ni ule ugonjwa kuwa unazunguka tu kutoka kwa huyu kwenda kwa mwingine na mama anatibu na pesa inaingia na ugonjwa hauishi sababu unabaki njia panda akipita mtoto unamwingia, so ni ishu endelevu ambayo haina kikomo. Endapo mama angeamua atajirike angefanyia town then akapandisha bei hapo sawa, maana ugonjwa unaua kabisa.
 
Sasa anachomiliki mama yako ni ugonjwa au ni tiba?

Yaani ni kama ukimwi au covid 19 ya wazungu?

Kama ugonjwa ulikuwepo bila yeye kuhusika kuwepo kwa huo ugonjwa tiba ya miti shamba anayoitoa mama yako sio uchawi

Hakuna mchawi tajiri duniani
 
Ngoja tusiende mbali huyu msanii huko Marekani aliyeko mahabusu akisubiri kesi ianze kusikilizwa, Ina maana hujajifunza chochote kutoka kwenye matendo yake, au unahisi Kila kitu ni utani?
 
Inawezekana ni mtu mzima ila mwenye akili za kitoto. Unavyochanganya lugha nakuona kama slay queen maana ndo wenye hizo pigo.
 
Anachomiliki mama Ni tiba. Kwa sisi wa imani ya ukrito huwa tunaamini ktk maagano na ulimwengu wa roho kupitia damu. Mf. Yesu kufunga agano kupitia damu.
Ulimwengu wa Giza pia maagano Ni damu mf. Utaambiwa na mganga ulete kuku anachinjwa inatoka damu inafunga agano au lete ng'ombe kulingana na uhitaji wako.

Sasa upande wa mama yeye anafanya tiba lkn pale anapomchanja mtoto na kupaka dawa nafkiri ndipo agano lilipo. Hivyo Basi kinachouondoa ule ugonjwa kwa mtoto Ni ile nguvu ambayo umeagana nayo kupitia damu kisha hiyo nguvu ndiyo inayopeleka Tena ugonjwa kwa mtoto mwingine atakaye kanyaga katiba kwa kupita njia panda ugonjwa ulipo.
 
Inawezekana ni mtu mzima ila mwenye akili za kitoto. Unavyochanganya lugha nakuona kama slay queen maana ndo wenye hizo pigo.
Hata wewe mwenyewe tayari umesha changanya lugha.

Ulivyosema "Kama slay queen" tayari umesha changanya kiswahili na kiingereza.

Kwanza jitathmini wewe mwenyewe kabla hujakurupuka kusema kitu.
 
Samahani.
Kabla ya kukujibu naomba kujua umri wako.
 
Ngoja tusiende mbali huyu msanii huko Marekani aliyeko mahabusu akisubiri kesi ianze kusikilizwa, Ina maana hujajifunza chochote kutoka kwenye matendo yake, au unahisi Kila kitu ni utani?
Matendo yake ni matendo ya kibinadamu na makosa ya kibinadamu kama binadamu wengine.

Si kwamba ni shetani ndio alimtuma au alimfanya afanye vile.

Ni tamaa zake za kibinadamu wala hakuna shetani yeyote yule.
 
Hapa nimegundua shida ipo kwenye imani ya dini yako na sio uchawi

Mama yako sio mchawi bali anatibu kupitia tiba asilia yani miti shamba huo ugonjwa upo tu siku ukikoma na tiba itakuwa imeishia hapo au zikigundulika dawa nyingine eneo hilo au vinginevyo

Haitoshi kurelate tiba anayotoa bi mdashi na utajiri wa nguvu za giza

Hakuna utajiri wa nguvu za giza ni imani za masikini juu ya matajiri ndio maana wote wanaosema upo wanashindwa kutoa mifano ni nani duniani ana utajiri wa kichawi hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…