Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Mambo ya kiimani ni illusions zilizoteka dunia hii hasahasa Africa , mtu hawezi kukuelewa kumwambia mambo ya Imani ni vitu vya kufikirika, Yani kumwambia mtu hakuna MUNGU Wala shetani , weee atakuona kama vile we ndo shetani mwenyewe😂 . Maisha ndo haya haya tuyaishi Wala hakuna nguvu ya kiroho ( mwanga au Giza) inayokufanikishia jambo lako sijui uhai pesa , Imani ni stori za abunuwasi
Imani za kichawi zimetoka Afrika

Imani za kiungu zimetoka Asia na ulaya

Ila waafrika kwenye uchawi tunazingua sana aisee yani mpaka dini wanahubiri uchawi

Ukipata maendeleo ni uchawi

Ukikosa maendeleo ni uchawi

Yani uchawi uchawi uchawi kila mahali
 
Unajua mwanadamu Ni mbishi Sana Sana Hadi pale akipigwa ndumba vizuri ndipo atajua kwamba hizi vitu zipo.

Kuna Mambo nayatafakari bado hayaleti kuamini kwamba uchawi haupo. Nakumbuka nikiwa mdogo nakua, mama mzazi Kuna dawa moja yakienyeji alikuwa anawachanja watoto tu pale mtaani ambayo anadai alirithishwa na mkwe wake. Ilikuwa inaitwa dawa ya bengu. Ugonjwa wenyewe unaitwa bengu ambao mtoto anavimba tumbo anapata na homa, mwili kudhoofu na kinyesi kinakuwa manjano na kijani.
Sasa Kuna mti wa porini alikuwa anachubua magamba yake anaanika nakusaga ungaunga then anachimba matunda Fulani yaporini yapo Kama viazi mviringo Kisha anapasua vipande viwili ili wakati anamtibu mtoto huchukua matunda hayo kama kiazi mviringo na kuyachovya kwenye ule ungaunga kisha kumpaka mtoto eneo la tumbo ambapo tayari ameshamchanja chale eneo lote linaloumwa.
Tukio hili la kuchanja linafanyika njia panda
Na vifaa vyote vinawekwa kwenye kigae/kipande Cha chungu.
Akimaliza kumchanja nakumpaka dawa anamwambia mama mtoto aondoke atangulie nyumbani lkn asiongee na mtu wala kugeuka nyuma afike afungue mlango nakuingia ndani Kisha anasimama kwa ndani Kisha mama anafika na kumwita mama mtoto " mama Fulani mama Fulani"
Anaitika Kisha anamuuliza "bengu umeiacha wapi? Anajibu " nimeiacha njia panda" hapo zoezi la tiba linakuwa limekamilika hivyo Basi mama anampa maelekezo kwamba aondoke na Yale matunda Kama viazi mviringo achimbe kwenye jiko lakuni alafu awe anapikia hapo. Na kila anapokuwa anapikia hapo ule Moto kadri unavyounguza yale matunda ndivyo ugonjwa unavyozidi kuungua na hatimae mtoto anapona kabisa.

Toka nikiwa mdogo naona mama anawachanja watoto wanapoona kabisa na mama akawa anasifika Sana pale mtaani Hadi vijiji jirani walikuwa wanakuja kutibiwa.

Kitu ambacho kimenifanya kuandika hivi Ni kueleza namna ambavyo dawa ile inafanya kazi. Of course Ni Mambo ya kiganga ya jadi lakini chakushangaza zaidi pale Ni kwamba; mama mtoto alipouliza bengu umeiacha wapi? Yaani ugonjwa kauacha wapi? Anajibu nimeuacha njia panda. Maana yake ule ugonjwa unabaki njia panda kusubiri mama yeyote mwenye mtoto apite na hapohapo ugonjwa unamvaa mtoto na kwahivyo Ni lazima amtafute mama amtibu mtoto wake na kuuacha ugonjwa Tena njia panda.
Kitega uchumi Cha mama yangu ilikuwa njia panda kwa kila mtoto atakayepita hapo.

Huo Ni mfano mdogo kuonesha kwamba haya Mambo ya kiganga na kishirikina yapo duniani Ni vile tu mtu unakuwa hujayashuhudia.
Hebu relate hiyo content na utajiri tuone mtu anatajirikaje hapo

Uganga wa miti shamba sio uchawi miti shamba inathibitika kisayansi uchawi upo kiimani na kiroho
 
Waooh what a testmony...
Tena inayomuhusu mama yako...
Ndio mama mzazi lkn ameshaacha kutibu. Juzi nimempigia cm kumuuliza Kama Kuna mtoto aliwahi kufariki wakati wa tiba zake akadai ndio lkn ni mtoto mmoja tu toka aanze kuwatibu but anadai mtoto yule hakufariki kutokana na tiba yake mama Bali alikuwa na tatizo lingine hahahah!
 
Hebu relate hiyo content na utajiri tuone mtu anatajirikaje hapo

Uganga wa miti shamba sio uchawi miti shamba inathibitika kisayansi uchawi upo kiimani na kiroho
Iko hivi: upande wa mama hakuwa akiwachaji pesa nyingi ilikuwa Ni Kama msaada tu. Lkn tukisema kwa ishu yakutajirika sijui kiundani but kinachoshangaza Ni ule ugonjwa kuwa unazunguka tu kutoka kwa huyu kwenda kwa mwingine na mama anatibu na pesa inaingia na ugonjwa hauishi sababu unabaki njia panda akipita mtoto unamwingia, so ni ishu endelevu ambayo haina kikomo. Endapo mama angeamua atajirike angefanyia town then akapandisha bei hapo sawa, maana ugonjwa unaua kabisa.
 
Sasa anachomiliki mama yako ni ugonjwa au ni tiba?

Yaani ni kama ukimwi au covid 19 ya wazungu?

Kama ugonjwa ulikuwepo bila yeye kuhusika kuwepo kwa huo ugonjwa tiba ya miti shamba anayoitoa mama yako sio uchawi

Hakuna mchawi tajiri duniani
 
Niambie ni nani aliyemuua Albino akapata utajiri na akatajirika kweli?

Leta uthibitisho hapa wa mtu yeyote yule aliye tajirika kwa ushirikina wa kuua Albino.

Wewe si unadai na kuamini kuna utajiri wa kishetani na kishirikina.

Sasa Thibitisha mtu yeyote yule aliyepata utajiri kwa kuua Albino.
Ngoja tusiende mbali huyu msanii huko Marekani aliyeko mahabusu akisubiri kesi ianze kusikilizwa, Ina maana hujajifunza chochote kutoka kwenye matendo yake, au unahisi Kila kitu ni utani?
 
Hunijui sikujui halafu unasema mimi ni mtoto, Yani unafanya speculations zako uchwara zisizo na uthibitisho wala mantiki yeyote.

Umeishiwa hoja unaleta Viroja.

It clearly seems you are not mentally enough to think and reason properly and critically.

Don't come here to advertise your ignorance.
Inawezekana ni mtu mzima ila mwenye akili za kitoto. Unavyochanganya lugha nakuona kama slay queen maana ndo wenye hizo pigo.
 
Sasa anachomiliki mama yako ni ugonjwa au ni tiba?

Yaani ni kama ukimwi au covid 19 ya wazungu?

Kama ugonjwa ulikuwepo bila yeye kuhusika kuwepo kwa huo ugonjwa tiba ya miti shamba anayoitoa mama yako sio uchawi

Hakuna mchawi tajiri duniani
Anachomiliki mama Ni tiba. Kwa sisi wa imani ya ukrito huwa tunaamini ktk maagano na ulimwengu wa roho kupitia damu. Mf. Yesu kufunga agano kupitia damu.
Ulimwengu wa Giza pia maagano Ni damu mf. Utaambiwa na mganga ulete kuku anachinjwa inatoka damu inafunga agano au lete ng'ombe kulingana na uhitaji wako.

Sasa upande wa mama yeye anafanya tiba lkn pale anapomchanja mtoto na kupaka dawa nafkiri ndipo agano lilipo. Hivyo Basi kinachouondoa ule ugonjwa kwa mtoto Ni ile nguvu ambayo umeagana nayo kupitia damu kisha hiyo nguvu ndiyo inayopeleka Tena ugonjwa kwa mtoto mwingine atakaye kanyaga katiba kwa kupita njia panda ugonjwa ulipo.
 
Inawezekana ni mtu mzima ila mwenye akili za kitoto. Unavyochanganya lugha nakuona kama slay queen maana ndo wenye hizo pigo.
Hata wewe mwenyewe tayari umesha changanya lugha.

Ulivyosema "Kama slay queen" tayari umesha changanya kiswahili na kiingereza.

Kwanza jitathmini wewe mwenyewe kabla hujakurupuka kusema kitu.
 
Waafrika wengi hasa watanzania wamekuwa wakiamini kwa muda mrefu kwamba kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Cha kushangaza hali zao za kiuchumi ziko vilevile miaka nenda rudi.

Kama kweli kwa hakika unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote uwe tajiri mkubwa nchini Tanzania, Afrika na duniani?

Kwa nini ujihangaishe kufanya kazi na kuchoka ilhali unajua kuna utajiri wa kishetani?

Kamtumie huyo shetani akutajirishe kama ni rahisi hivyo!!

Katoe kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako wote tuone kama biashara yako itakuwa kubwa au utaweza hata kufikia utajiri wa Bakhressa.

Kama kweli kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa Afrika kama Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na matajiri wengine wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos?

Kama kweli unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini hujautumia huo uchawi, ushirikina, uganga angalau ufike hata level za utajiri wa Mo Dewji?

Kama unaamini kuna Shetani akitolewa kafara anatoa mali au atakupa mali za kukutajirisha, Katoe kafara wazazi wako au wanao wote tuone kama hata utafika level za utajiri wa Dangote.

Au kama unaamini kuna utajiri wa ndagu, uganga, ulozi n.k
Mwambie huyo mtoa ndagu au mganga, Akupe utajiri angalau umfikie au umzidi Bakhressa kama ana huo uwezo.

Au mwambie huyo mganga akuwezeshe umiliki private jet ✈️, Kiwanda kikubwa cha uzalishaji, Magari makali ya kifahari kama Rolls-Royce Boat tail, Mercedes Maybach, Buggati, Lamborghini, Cadillac escalade au akishindwa sana angalau akupe Range rover sport kwa uganga wake tu.

Waafrika wengi hasa watanzania wana amini kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina lakini bado maisha yao ni ya kimaskini, kikapuku, kifukara pangu pakavu tia mchuzi.

Kama unaamini au unajua kuna Shetani anatoa utajiri, Kamtumie kwa nguvu zako zote akutajirishe na uwe tajiri kweli, Angalau ufike level za utajiri wa kina Dangote.

Kisha ndio uanze kusema kwamba kuna utajiri wa kishetani.

Habari za utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina, Husikika tu kwa waafrika maskini choka mbaya, wajinga, wavivu, makapuku, makabwela na mafukara ambao wanashinda vijiweni na vilabuni waki danganyana na kupeana matumaini uchwara ya utajiri wa kufikirika.

Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani kinacho toa utajiri. Utajiri na pesa hutoka kwa binadamu. Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani chenye pesa.

Pesa ni za binadamu, Si za Mungu wala Shetani.

Hakuna Mungu, Shetani, Jini, Pepo au nguvu yeyote ile ya kimiujiza inayotoa Utajiri.

Pesa, Mali na utajiri hupatikana kwa nguvu za kibinadamu na wanadamu.

Ni wajanja wachache tu huwalaghai na kuwadanganya watu wengine kwamba kuna shetani anatoa utajiri ili kuwahadaa na kuwapumbaza watu wajinga wasiotaka kuhustle wenyewe wakitegemea mafanikio ya kuletewa.

Ndio maana unakuta wanawekewa masharti makali ya kupata pesa hizo ambao wao hudhani ndio masharti ya kishetani ya huyo shetani, Kumbe ni masharti ya binadamu wajanja tu.

The supernatural power is You, Yourself.

Hakuna Mungu wala Shetani anayetoa utajiri, pesa au mali.

I'm out.
Samahani.
Kabla ya kukujibu naomba kujua umri wako.
 
Ngoja tusiende mbali huyu msanii huko Marekani aliyeko mahabusu akisubiri kesi ianze kusikilizwa, Ina maana hujajifunza chochote kutoka kwenye matendo yake, au unahisi Kila kitu ni utani?
Matendo yake ni matendo ya kibinadamu na makosa ya kibinadamu kama binadamu wengine.

Si kwamba ni shetani ndio alimtuma au alimfanya afanye vile.

Ni tamaa zake za kibinadamu wala hakuna shetani yeyote yule.
 
Anachomiliki mama Ni tiba. Kwa sisi wa imani ya ukrito huwa tunaamini ktk maagano na ulimwengu wa roho kupitia damu. Mf. Yesu kufunga agano kupitia damu.
Ulimwengu wa Giza pia maagano Ni damu mf. Utaambiwa na mganga ulete kuku anachinjwa inatoka damu inafunga agano au lete ng'ombe kulingana na uhitaji wako.

Sasa upande wa mama yeye anafanya tiba lkn pale anapomchanja mtoto na kupaka dawa nafkiri ndipo agano lilipo. Hivyo Basi kinachouondoa ule ugonjwa kwa mtoto Ni ile nguvu ambayo umeagana nayo kupitia damu kisha hiyo nguvu ndiyo inayopeleka Tena ugonjwa kwa mtoto mwingine atakaye kanyaga katiba kwa kupita njia panda ugonjwa ulipo.
Hapa nimegundua shida ipo kwenye imani ya dini yako na sio uchawi

Mama yako sio mchawi bali anatibu kupitia tiba asilia yani miti shamba huo ugonjwa upo tu siku ukikoma na tiba itakuwa imeishia hapo au zikigundulika dawa nyingine eneo hilo au vinginevyo

Haitoshi kurelate tiba anayotoa bi mdashi na utajiri wa nguvu za giza

Hakuna utajiri wa nguvu za giza ni imani za masikini juu ya matajiri ndio maana wote wanaosema upo wanashindwa kutoa mifano ni nani duniani ana utajiri wa kichawi hakuna
 
Back
Top Bottom