Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Mi niliutafuta nikakosa mwenye ushahidi aje hapa
Mpaka sasa hakuna mtu aliyekuja na uthibitisho wa tajiri mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi na ushirikina.

Wanakuja tu kutema nyongo zao hapa.
 
1. Namimi nahitaji unithibitishie ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa pasipo assist ya uchawi na , hao si washirikina, na unielezee jinsi ulivyokuepo na kuona kila jambo alilolifanya hatua kwa hatua from the scratch mpaka hapa walipo.
 
Usijadili vitu usivyovijua. This world is governed by spiritual powers. Hata wazungu walio matajiri kuna kanuni za kiroho wanazifuata!
Kaka umenena vyema sana.
Huyu kijana Infropreneur na wengine wenye mwelekeo wake wajifunze kuhusu hili. Dunia haiendeshwi kwa njia ya msalaba
 
Utajiri wa nguvu za kibinadamu upo, na wa nguvu za kiroho upo pia. Tofauti yake ni kuwa utajiri wa nguvu za kibinadamu una ukomo wake (Mungu hawezi kukupa utajiri kuliko uwezo wako wa kujitawala). Popote ukiona mtu ana utajiri kuliko uwezo wake wa kujitawala basi jua kuna mpaka umevukwa na tayari mtu ameshahamia upande wa pili wa nguvu za kiroho. Kuna level za utajiri huwezi kuzifikia bila kushiriki katika mambo ya kiroho.

Kingine usichokijua ni kuwa utajiri wa kishirikina unaambatana na mambo matatu:-
1. Kuuza nafsi yako kwa shetani in exchange of material things.
2. Majuto
3. Huzuni
Sio wote wako tayari kuvuka mpaka wa uthubutu kufikia huko, japo kuna wachache hufika huko kwa kujizima data.
 
Kaka umenena vyema sana.
Huyu kijana Infropreneur na wengine wenye mwelekeo wake wajifunze kuhusu hili. Dunia haiendeshwi kwa njia ya msalaba
Kafuate hizo kanuni utajirike kama zipo.

Nilikwambia ulete uthibitisho wa tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi na ushirikina, Hujaleta mpaka dakika hii.

Nilikwambia ulete uthibitisho wa nchi gani duniani, Raia wake walifanikiwa kwa nguvu za kichawi, kishetani na kishirikina, Hujaleta mpaka sasa hivi!!

Unaruka ruka tu.

Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Waafrika wanashindwaje kuutumia wawazidi wazungu?

Tumieni huo uchawi au ushirikina kujenga maviwanda makubwa, kujenga miundombinu, kujenga viwanja vya ndege na bandari.

Angalau basi tufikie level za utajiri wa wazungu.
 
Niambie na thibitisha ni tajiri gani mkubwa hapa nchini Tanzania, Afrika au duniani alifanikiwa kwa nguvu za kiroho tu?
Niambie na thibitisha ni tajiri gani mkubwa hapa nchini Tanzania, Afrika au duniani alifanikiwa kwa kuuza nafsi yake kwa shetani?

Kwanza thibitisha uwepo wa shetani.

Kisha eleza na thibitisha hiyo nafsi ni nini?

Na hiyo nafsi inauzwaje kwenda kwa huyo shetani?
 
Kijana kama utaweza kununua kitabu kinaitwa 'Illuminati Testaments' kutoka Amazon unaweza kuanza kupata mwanga kwa nini unabishana na wakubwa zako. Hii itaanza kukupa mwanga kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi na kisiasa yanavyoendeshwa duniani. Its full occult
 
Kwa kuanza kasome kitabu kinaitwa Illuminatiam (Illuminati Testaments) uanze kufunguka.
 
1. Wafuasi wa Freemason.
2. Wafuasi wa P. Diddy.
3. Wateja wa Prof. Majimarefu (rip)
4. Wamiliki wa mapaka pale Tunduma.
5. Wenye misukule mbele ya maduka yao.
6. Askofu Gwajima ....mfufua misukule.

Wakiuona huu uzi watakushitaki.
 
Nenda kwenye hizo occult kama wana uwezo wa kukupa utajiri wa kuweza kumzidi Dangote.

Sikia wewe, Hakuna utajiri wowote kwenye occult.

Huo utajiri wa kwenye occult ni utajiri wa watu walio utafuta kwa jasho na damu.

Halafu wajinga kama wewe mnaotaka Utajiri wa bure bure tu, Ndio mnawekewa masharti makali ya kupewa utajiri huo.

Na hawawezi kukupa utajiri mkubwa kuliko uwezo wa huo utajiri walionao wao.

Kama unabisha, Tafuta occult society yeyote jiunge nao halafu waambie wakupe utajiri mkubwa wa kumfikia au kumzidi Elon musk kama wataweza.

Wakiweza rudi hapa JF uniambie.
 
Muache kama alivyo naona hakuna anachokijua
Wewe hicho unacho kijua ni nini?

Niambie na thibitisha ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi au ushirikina kama unamjua?

Niambie na thibitisha ni nchi gani, Raia wake walifanikiwa kwa nguvu za kichawi, kishetani na kishirikina kama kweli unajua?

Au unaleta stori zako za vijiweni huko.
 
Njoo ujionee namna tunavyo miliki nyoka wanao tapika pesa Kila ijumaa mchana kiasi Cha 200M inaingia Kila ijumaa Cha muhimu kuzingatia mashart
 
Njoo ujionee namna tunavyo miliki nyoka wanao tapika pesa Kila ijumaa mchana kiasi Cha 200M inaingia Kila ijumaa Cha muhimu kuzingatia mashart
Mimi nataka huyo nyoka 🐍 atapike kiasi cha Dola za kimarekani Billion 500 kama ana huo uwezo.
 
Unabisha bila hoja. Nadhani ni utoto unakusumbua.
Kama upo serious, kasome hicho kitabu nilichokutajia kisha urudi tena hapa kubishana na mimi
 
Mimi nataka huyo nyoka 🐍 atapike kiasi cha Dola za kimarekani Billion 500 kama ana huo uwezo.
Ila Wewe dogo ni Bogus sana...Kakwambia nenda kwake umuone huyo nyoka ww unaanza kusema unamtaka si ukamtafute wako.
Kumbe wewe n Mwehu unajaza Server tu apa.
 
Ila Wewe dogo ni Bogus sana...Kakwambia nenda kwake umuone huyo nyoka ww unaanza kusema unamtaka si ukamtafute wako.
Kumbe wewe n Mwehu unajaza Server tu apa.
Mwehu ni baba na Mama yako waliozaa punguani kama wewe usiyefikiri sawasawa.

Kama huyo nyoka anaweza kutema hela, Si ateme hela nyingi za kuweza kumtajirisha huyu jamaa anayedai huyo nyoka anatema hela?

Walau huyu jamaa "HaMachiach" aweze kuwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk.
 
Unabisha bila hoja. Nadhani ni utoto unakusumbua.
Mpaka sasa umeshindwa kuthibitisha ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi na ushirikina?

Mpaka sasa umeshindwa kuthibitisha ni nchi gani raia wake walifanikiwa kwa nguvu za kichawi, kishetani, ki Illuminati, au kishirikina.

Halafu unasema sina hoja.

Wewe ndio huna hoja.

Unaleta stori zako uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.
Kama upo serious, kasome hicho kitabu nilichokutajia kisha urudi tena hapa kubishana na mimi
Kama una uthibitisho wa tajiri yeyote mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi au ushirikina ndio uje hapa kujenga hoja.

Unless otherwise, Find someone of your league to parallel your mediocrity.
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Endelea kuamini unachokiamini mkuu.
Hivi zile ng’ombe zinazotolewa na waarabu mwaka hadi mwaka zinachinjwa wanagawiwa watu anataka kusema wana roho nzuri wanatoa bure tu??? Huyi hajui mambo ya spiritual ni kumuacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…