Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Waelewe tu mkuu,
97% ya Watanzania wamekuzwa kwenye mazingira ya kuamini uchawi, uganga, freemason na ushirikina. Story za ndagu, pete za bahati na chuma ulete kwa wingi sana
 
Kuna utajiri wa nguvu za Giza, Utajiri wa Nguvu za Mwanga na utajiri usiohusisha nguvu zote zaidi ya juhudi za binadamu pekee! Sasa Bongo wengi wanautajiri wa juhudi za kibinadamu, wanafuata wa nguvu za giza kisha nguvu za mwanga ambao ni wachache.
 
Waafrica wajinga Kama mtoa mada na masikini wakutupwa ndo wanaamini kuwa hakuna spiritual power .

Hoja za kijinga swala umasikini ni ukosefu wa maarifa na akili sasa ukiwa hauna maarifa na akili how you can hold spiritual power .
 
Walokole na uchawi wa kukemea mapepo katika moja na mbili

Nafutialia kwa ukaribu hapa
Kwanza hao walokole ndio maskini choka mbaya kutwa kucha kushinda makanisani kama wehu wakiimba na kupayuka kama mbayuwayu
"Napokea, napokea, napokea"

Kumbe hakuna wanacho pokea zaidi ya umaskini, ukapuku na ufukara.
 
Masikini hujipa matimaini kwa kuwa na imani za kidini, humo ndio wamejifunza huu ujinga wa miujiza ya kukutokea na kutatua matatizo yako bila hata kuhitaji kujishughulisha......
Akiona huko hakumpii matumaini, anatafuta ujinga mwingine utakaompa jibu la haraka kwenye matatizo yake kwa kuamini ujingaujinga wa kichawi kuwa unaweza kumtatulia matatizo yake, badala yake ni kuzidi kutumbukia kwenye umasikini wa milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…