Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Waafrika wengi hasa watanzania wamekuwa wakiamini kwa muda mrefu kwamba kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Cha kushangaza hali zao za kiuchumi ziko vilevile miaka nenda rudi.

Kama kweli kwa hakika unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote uwe tajiri mkubwa nchini Tanzania, Afrika na duniani?

Katoe kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako wote tuone kama biashara yako itakuwa kubwa au utaweza hata kufikia utajiri wa Bakhressa.

Kama kweli kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa Afrika kama Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na matajiri wengine wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos?
Kamwe binadam hatuwezi kua sawa ktk jambo lolote kama utakavyo.

Wachukue hata atheist, wasioamini ushirikina wape nyenzo sawa, bt bado hawawezi kukupa matokeo sawia ktk jambo lolote.
 
Basi kama kuna mtu Huwa namuona ni mpumbavu ni yule anayesema hakuna Mungu. Kuna vitu vonatia hasira sana.

Nimeumia sana kwa ajili yako. Kwa hiyo na wewe unajiweka kwenye kundi la wanasayansi ambao hawaamini kuwa kuna Mungu.

Hao wanasayansi deep down wanaamini Mungu yupo sema wameshindwa kuthibitisha kisayansi ndio maana wanakana.

Aliyekulisha huo upuuzi wa atheist amekosea sana.
mkuu kashike malli basi ,unangoja nin?
 
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika, kuhisika na kupimika.

Hewa ipo inahisika,inavutwa na inapimika ipo.

Usingizi upo, una hisika, una u experience na kujua upo.

Upendo upo unapimika kwa kumu observe mtu.

Hasira ipo inapimika kwa kumu observe mtu pia.

Sasa huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Haonekani, Hashikiki, Hasikiki, Haisiki na wala hapimiki.

Mungu huyo ni mawazo ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.

Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu ndio maana huwezi kuthibitisha uwepo wake.
umeona vile hata uelewa wa darasa la tatu huna

hujui hata majina dhahania, hujui kama muumba anaingia kwenye kuhisika hujui hayo yote hewa, hasira, usingizi yako humo

alafu unakaza fuvu
 
Kamwe binadam hatuwezi kua sawa ktk jambo lolote kama utakavyo.

Wachukue hata atheist, wasioamini ushirikina wape nyenzo sawa, bt bado hawawezi kukupa matokeo sawia ktk jambo lolote.
Ni kwasababu binadamu tuna tofautiana hivyo hatuwezi kuwa sawa kwenye kila kitu.

Lakini kusema kwamba kuna kiumbe kiitwacho Shetani kinacho toa utajiri kwa watu sikweli.

Binadamu tuna tofautiana jitihada za utafutaji huo utajiri ndio maana lazima tutofautiane.
 
umeona vile hata uelewa wa darasa la tatu huna

hujui hata majina dhahania, hujui kama muumba anaingia kwenye kuhisika hujui hayo yote hewa, hasira, usingizi yako humo

alafu unakaza fuvu
Ndio ni dhahania lakini yanapimika, yanathibitishika na kujulikana yapo.

Hewa inapimika na kuthibitishika ipo.

Muumba hayupo hata kwa kuhisika. Niambie unamuhisi kupitia nini na anapimika kwa namna gani na kuonekana vipi?

Zaidi ya mawazo yako ya kufikirika tu.

Hasira na usingizi ni hali za kibinadamu ambazo zipo kwa binadamu zinapimika na kuonekana.

Mtu akiwa usingizini unamuona, mtu akiwa na hasira unajua na kumuona kwamba ana hasira.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile zaidi ya mawazo ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.
 
I am aware of the difference, and I have already implied that you are lack spiritual knowledge.
You are completely entitled to your opinions that are not supported by evidence.

But the moment you spread that opinion as fact, You are a liar.

And if you spread it as fact, Knowing it is not supported by evidence, You are both a liar and a fraud.
 
Unasema kwa utafiti ulioufanya kwa wenye utajiri wangapi au unasema Sema tu kutafuta Habari za uhakika humu ndani.
Shetani ni nini kwa mtazamo wako.
Shetani ni dhana ya kufikirika. Imaginations just an illusion.
Anaonekanaje? Je yeye ni tajiri kwa kiasi gani? Je anaweza kugawa huo utajiri kwa kila anayehitaji? 😀
Shetani hayupo kwa namna yoyote ile. Na hana utajiri wowote ule.
Wewe binafsi unaweza chukua utajiri wake akikupa?
Shetani hayupo.
 
Waafrika wengi hasa watanzania wamekuwa wakiamini kwa muda mrefu kwamba kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Cha kushangaza hali zao za kiuchumi ziko vilevile miaka nenda rudi.

Kama kweli kwa hakika unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote uwe tajiri mkubwa nchini Tanzania, Afrika na duniani?

Kwa nini ujihangaishe kufanya kazi na kuchoka ilhali unajua kuna utajiri wa kishetani?

Kamtumie huyo shetani akutajirishe kama ni rahisi hivyo!!

Katoe kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako wote tuone kama biashara yako itakuwa kubwa au utaweza hata kufikia utajiri wa Bakhressa.

Kama kweli kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa Afrika kama Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na matajiri wengine wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos?

Kama kweli unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini hujautumia huo uchawi, ushirikina, uganga angalau ufike hata level za utajiri wa Mo Dewji?

Kama unaamini kuna Shetani akitolewa kafara anatoa mali au atakupa mali za kukutajirisha, Katoe kafara wazazi wako au wanao wote tuone kama hata utafika level za utajiri wa Dangote.

Au kama unaamini kuna utajiri wa ndagu, uganga, ulozi n.k
Mwambie huyo mtoa ndagu au mganga, Akupe utajiri angalau umfikie au umzidi Bakhressa kama ana huo uwezo.

Au mwambie huyo mganga akuwezeshe umiliki private jet [emoji3575], Kiwanda kikubwa cha uzalishaji, Magari makali ya kifahari kama Rolls-Royce Boat tail, Mercedes Maybach, Buggati, Lamborghini, Cadillac escalade au akishindwa sana angalau akupe Range rover sport kwa uganga wake tu.

Waafrika wengi hasa watanzania wana amini kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina lakini bado maisha yao ni ya kimaskini, kikapuku, kifukara pangu pakavu tia mchuzi.

Kama unaamini au unajua kuna Shetani anatoa utajiri, Kamtumie kwa nguvu zako zote akutajirishe na uwe tajiri kweli, Angalau ufike level za utajiri wa kina Dangote.

Kisha ndio uanze kusema kwamba kuna utajiri wa kishetani.

Habari za utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina, Husikika tu kwa waafrika maskini choka mbaya, wajinga, wavivu, makapuku, makabwela na mafukara ambao wanashinda vijiweni na vilabuni waki danganyana na kupeana matumaini uchwara ya utajiri wa kufikirika.

Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani kinacho toa utajiri. Utajiri na pesa hutoka kwa binadamu. Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani chenye pesa.

Pesa ni za binadamu, Si za Mungu wala Shetani.

Hakuna Mungu, Shetani, Jini, Pepo au nguvu yeyote ile ya kimiujiza inayotoa Utajiri.

Pesa, Mali na utajiri hupatikana kwa nguvu za kibinadamu na wanadamu.


Ni wajanja wachache tu huwalaghai na kuwadanganya watu wengine kwamba kuna shetani anatoa utajiri ili kuwahadaa na kuwapumbaza watu wajinga wasiotaka kuhustle wenyewe wakitegemea mafanikio ya kuletewa.

Ndio maana unakuta wanawekewa masharti makali ya kupata pesa hizo ambao wao hudhani ndio masharti ya kishetani ya huyo shetani, Kumbe ni masharti ya binadamu wajanja tu.

The supernatural power is You, Yourself.

Hakuna Mungu wala Shetani anayetoa utajiri, pesa au mali.

I'm out.
Kuna kitu kinaitwa peace of mind isikie tu hyo kitu.
 
Kuzaliwa katika familia ya kitajiri, Hiyo tayari ni bahati kwa mtoto. Si kila mtoto anapata bahati ya kuzaliwa kwenye familia tajiri.

Mtu anaye bahatika kuoa au kuolewa kwenye familia za kitajiri, Huyo tayari ana bahati ya kwenda kuukuta utajiri.

Hato hangaika sana kama wale wanao oana wakiwa na hali duni za kimaisha. Hiyo tayari ni bahati.

Bahati huweza kumtokea mtu yeyote yule awe mwema, muovu, mtoto, mtu mzima, mwanaume, mwanamke n.k

Bahati ni kama probability, inaweza kutokea ama isitokee.

Mikosi ni dhana ya kufikirika inayo husishwa na nguvu fulani za kufikirika tu.

Mfano mwanafunzi akifeli darasani, Anaweza kuhisi ana mikosi kumbe hakusoma na kujiandaa vizuri, Au alisoma akasahau alichosoma.

Na si kwamba ni hiyo "mikosi" ndio imemsababisha afeli.

Chanzo cha bahati ni uwezekano wa kutokea jambo, Ambalo katika nafasi ya kutokea lipo tayari.

Mfano kuzaa na kuzaliwa kupo tayari automatically, Na wewe unaweza kuwa ni tajiri na mtoto wako akapata bahati ya kuzaliwa na wewe ukiwa tajiri.

Vivyo hivyo anaweza akazaliwa na wewe ukiwa maskini au kwingineko kwenye familia maskini. Maana bahati ni probability.

Mikosi haipo, mikosi ni dhana ya kufikirika tu.
Infro... Hebu NINI maoni yako katika kisa hiki (Ni kisa cha kweli na mhusika ni mpwa wangu kabisa)
Ipo hivi huyu kijana alimaliza kidato cha nne 2022, matokeo yalipotoka alipata four ya 32... Kwa kuwa Mimi ni mjomba wake, na Hali ya dada yangu siyo ya kuchangamka sana kiuchumi, na Mimi ndiye niliye kuwa mtu wa karibu katika kusoma kwake (dada yangu ni single mother), nilimshauri akasome ufundi wowote anaopenda, akakataa katakata... Akawa bodaboda kwa mtu. Mwaka huu mwezi 2 alimpa rafiki yake hiyo pikipiki akasababisha ajali iliyogharimu Uhai wa mtu, akatoroka (huyo aliyesababisha ajali) Kesi ikabaki kwa mmiliki wa hiyo pikipiki na dereva halisi ambaye ni mpwa wangu. Tumepambana na hiyo Kesi mpaka mwezi 7 tulipoyamaliza kifamilia. Wakati huo wote mpwa wangu huyo hakuwahi kutulia kufanya shughuli yoyote kwa uhakika kutokana na Kesi. Cha kushangaza, WIKI MBILI ZILIZOPITA NILIPANDA BAJAJ MOJA AMBAYO DEREVA WAKE NI KIJANA NINAYEMFAHAMU, AMBAPO KATIKA MAZUNGUMZO YASIYO RASMI AKANIELEZA KWAMBA BAJAJI HII NI YA MPWA WANGU... NA KWAMBA ANAZO MBILI ZILIZOINGIA BARABARANI KWA KUPISHANA WIKI MBILI TU. NI BAJAJ TVS MPYAAA NAMBA T....ERB...
Nilipomuuliza mpwa wangu hakukubali Wala hakukataa, nilipomuuliza mama yake, anasema na yeye amesikia japokuwa kijana hajamwambia, ila mazingira anayoishi kijana wake sasa hivi yapo TOFAUTI na mwanzo kwani kwanza kahama nyumbani kwa mama yake na kapanga nyumba nzima mahali pengine, na pia amekuwa mtu wa "HARAKATI" nyingi.... Hadi sasa HIVI mama yake hachanganyikiwa, anasema "Kaka niokoe, sipo salama Tena, kifo kinanifuata"
MKUU INFROPRENUER, HAPA MAONI YAKO NI YAPI??
 
Mimi sina hasira.

Mimi najenga hoja hapa, kwa watakao jenga hoja.

Ila kwa hawa wajinga wanaokuja kutema nyongo hapa, Nitadili nao.

They shouldn't come here to vomit their nonsense.

Wewe kama ulishakuwa exposed kwenye hayo mambo, Ulishindwaje kuwa tajiri mkubwa walau hata hapa Tanzania tu?

Au unafikiri kila tajiri mkubwa alitumia hayo mambo ndio akawa tajiri?
Kuna mambo mengi hujui na ni vema ukaendelea kutojua. Baki na huo msimamo wako.
 
Haya maisha tuyaonayo kwa macho ya kawaida ni matokeo ya ulimwengu wa kiroho....hua unaota ndoto? Inakuwaje unajiona katika ndoto upo sehemu fulani tofauti na ulipo? Ni mfano wa ulimwengu wa kiroho ....mtafute mganga(kichawi)/mchawi muombe sana akuthibitishie ulimwengu wa kichawi ...namna wanavyoruka wakiiacha miili yao ndani na hatimaye kuirudia tena. Ni kweli huyajui haya....?
Hahahahhh walokole mna shida sana ndio maana mnapigwa na mhuni mmoja anajiita mwamposa

Yani wewe kiumbe mwenzio anapumua kama wewe anakuzidi ujanja
 
Una ubishi wa kipumbavu mno. Unaweza kujenga hoja bila kuwa emotional. Emotions waachie wanawake.
Kuna hoja yeyote umejenga zaidi ya viroja?

This kind of fallacy is called ad hominem.

Hujengi hoja unamshambulia mleta hoja. Na mimi ukija bila hoja utapata stahiki zako.

Ukija na hoja tutajenga hoja.
 
Sihitaji kusali.

Mimi sisali.

If prayers without work is nothing then prayer itself is nothing.

Hivyo huitaji kusali.
Ila unajua kuwa Kuna prayers!
Anyway hivi unawezasema tu na ukakaa pesa zikaja zenyewe au unatakiwa kupiga kazi Sawasawa na ulichosomea? Kama ndio basi hata prayers ni hivyohivyo.
Imani bila matendo imekufa😄
 
Kuna mambo mengi hujui na ni vema ukaendelea kutojua. Baki na huo msimamo wako.
Kama kitu unakijua kwa uhakika njoo na ushahidi, Pia leta uthibitisho.

Sio hadithi, stori za kusimuliwa na imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.
 
Rafiki utajiri wa ibilisi siyo mwepesi hivyo kama ulivyoandika, kuna mengi ndani yake na ni maumivu na majuto...so kupanda kwa kasi inawezekana ila na maumivu na majuto ni makubwa....wengi wana utajiri huo ila hawana furaha nao, wanajuta kwa nini waliingia... kutoka wanaumia mawazo na akili, wakikumbuka wamesha fanya ya hovyo mengi na wataanza vipi kutafuta kutoka sifuri....ni bora hauamini itakusaidia usiingie kwenye majuto.
Hebu mtaje mmoja tu unaemjua na sio kuhisi yani iwe unajua kuwa ana huo utajiri wa kichawi na anajuta

Hivi nyie Waafrika mtatoka lini usingizini
 
Back
Top Bottom