Hakuna wakati naona Serikali haijakamilika Kama hivi sasa

Hakuna wakati naona Serikali haijakamilika Kama hivi sasa

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,625
Reaction score
89,385
Huko bungeni vururuvururu tu!,wamejazana kijani tupu na wale kumi na tisa waliingia kimazabemazabe!.

Uwazirini wengi wamerithiwa na wanaowekwa kama hawajitoshelezi,nafasi ya waziri mkuu imekuwa mguu ndani mguu nje!.
Makamu wa rais nae kimya sana Kama hayupo..

Wengi wanaotaka kuteuliwa wamekuwa wakujipendekeza hata mambo yanakosa uhalisia kabisa!.. kwa yanayotokea huko serikalini naona watu wamekosa imani kabisa Mambo ni fujo na vurugu!.

Ni kama taifa halikuwa tayari kupata uongozi mpya kwa haraka!,Sasa Kama kunawaovu wanaweza kupitisha mambo yao huu ni wakati hatari zaidi ktk taifa letu kushinda wakati wowote(kwa maoni yangu lakini).
Hata hiyo katiba mpya inayoombwa naona hata isiombwe sahivi nahofia wenye ajenda zao wamaweza pitisha mambo yao!,nchi haijatulia aisee.

Makundi sahivi ndo yanawika sana sio sukuma gang sio sijui msoga gang..😬
Serikali inahitaji utulivu wakati huu kufanya mambo yake kwa umakini mitikisiko ni mingi na ajenda nazo ni nyingi!.

Mahuburi sahivi yamekuwa ya viongozi tu wala sio kulisuka taifa!,ni Kama vile tupo kwenye nusu uchaguzi!.😂
 
Back
Top Bottom