Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Umerogwa nakwambia haiwezekani unashindwa kutofautisha namba sio bure wachawi hawapendi maendeleo yako..
 
Wewe ndiye mjinga mkubwa kwasababu huna akili hata kidogo
 
Kwa wale wanaoamini uchawi upo wajibu maswali haya

1: uchawi ni nini

2: Nani anaemiliki huo uchawi na anaumiliki kwa namna gani

3: anauhamisha vipi kutoka kwenye umiliki wake na kuutuma kwenda kumdhuru kiumbe mwingine na unaingia kwa huyu kiumbe mwingine kupitia njia zipi.
 
Hujakutana na usiku unaojifungua........
Mi nilikuwa kama wewe ila mwaka 2019 nilipigwa tukio....acha kabisa
 
Wewe ni lazima uje kutetea hiyo imani ya kufikirika kuhusu uchawi coz wengi humu umewashikia akili zao kwa kuwaongopea kuhusu upuuzi huo,kuna wengine mpaka wanakuona eti wewe ni GT,
Hiki ni kichekesho kwa karne hii.
 
Nasubiri majibu pia.
 
Wewe ni lazima uje kutetea hiyo imani ya kufikirika kuhusu uchawi coz wengi humu umewashikia akili zao kwa kuwaongopea kuhusu upuuzi huo,kuna wengine mpaka wanakuona eti wewe ni GT,
Hiki ni kichekesho kwa karne hii.
Hili huwa linanichekesha sana. Watu huwa wanamuona mshana eti ni GT. Sema huyu mwamba na mwenzake Likud wana maslahi na hili suala
 
Fuatili story za akina nimrodi wa babeli , akina farao wa misri, mwambie mchungaji wako akusimulie sisi wengine hatutoweza
 
Unajua ishu ya chuma ulete ni uzembe na kujisahau tu?

Na mbaya zaidi ni pale unaposahau na hujiweki katika nafasi ya kusahau au kukosea na kuanza kufikiria kitu kingine kama sababu

Mfano unaweza zidisha chenji kwa mtu, kitendo hicho kwako kwa wakati huo unapokifanya unaona kama ni sahihi kurudisha kiwango hicho cha pesa kwa mteja

Baadaye unapokuja kuangalia hesabu zako unaona kuna pesa haionekani, ukianza kufanya diagnosis kufikiria wapi utakuwa umeipotezea hiyo pesa, kila unaporejea kumbukumbu ya yule mteja uliyemzidishia pesa utaona kuwa pale hakukua na tatizo na ni pesa ambayo ni halali uliyo mrudishia

Kila wakati ukifikiria utaona upo sahihi na hapo ndio utaanza kufikiria kuwa ni chuma ulete, lakini kumbe sio.
 
Kwa heshima kubwa bro Mshana Jr eti vip kuhusiana na chimaulete (sijui kama nimeandika sahihi) vip hii kitu ipo? Na kama ipo, imekaaje hii?

Ukiachana na Mengi yanayohusiana na uchawi lakin hii pia hunifikirisha sana

Bila kusahau Mimi nipo 50/50 kwasabab sijawahi shuhudia Jambo lolote linalohusiana na uchawi, halikadhalika sijawahi kuwa na uthibitisho kwamba uchawi hakuna kabisa. Kwasabab ni jambo ambalo sijawahi kulifuatilia kwa kina japo matamanio yangu siku moja ni kulifuatilia na kuwa elimu nalo ili kujua ukweli wake na hii ni kwasabab ya impact yake kwenye jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…