Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Nimeshawahi kuishi Mafinga mara kadhaa lakini sijawahi kuona baridi kama ya Juzi jumatatu tarehe 19. Dadeki baridi mpaka ukungu weñye barafu nyepesi ilikuwa inadondoka.

Nimefika Saa nane Usiku nikitokea Dsm. Nilitamani nirudi kwèñye Basi, Aiseeh! Pale Stendi nikaona makundi mawili ya Vijana yakiwa yamezunguka Moto wakiwa wanaota.
Nikavaa sweta Mbili, koti Moja lakini Wapi, nikaona sina namna Hapa Acha Nani nikaote Moto.

Wenyeji wakawa wananishangaa huku wakijaribu kutaka kunijua kama ninahitaji msaada gàni au nahitaji Usafiri WA bodaboda kwani wôte pale niligundua nu bodaboda, Mimi sikujali Wala nini, sikutaka kusalimu kwa sauti kûbwa, nikamsalimia aliyekaribu yàngu Kwa sauti ya chini. Nao wakanipuuza wakaendelea na Stori zào.

Nami nikaanza kutafakari nitaanzaje harakati zangu Siku ya Kesho Asûbuhi hasa kile kilichonipeleka. Saa yàngu mkononi ikinionyesha NI Saa Nane narobo.

Najua Baadhi ya Lodge nzuri zilizopo Hapa Mafinga, hivyo nikawa natafakari niende Ipi iliyokaribu, Mara ñàona bodaboda mmoja anakoswakoswa na Lori pale Barabarani. Vijana wanapiga Milunzi huku wakishangilia, Wengine wakipiga kelele la shangwe.

Taikon nashusha pumzi kutuliza kihoro kilichokuwa kimenianza kutokana na kuona tukio lile.

Yule bodaboda Manusura akaja pale nikawa namsahili, Hofu yake ilikuwa dhahiri usoni licha ya kuwa alikuwa anaongea na wenzake waliokuwa wanamtania Tania.

Anasema Mikono ilikuwa imeshika ganzi kutokana na baridi Kali kiasi kwamba alishindwa kukata Kona Hali iliyosababishwa akoswekoswe na lile Lori.

Basi Stori ikawa baridi jinsi inavyowapa changamoto. Kîla mmoja akieleza baridi ilivyosababisha hatari ya waô kupata ajali kama mjuavyo Vijana.

Wàpo wateja pale ambao walikuwa wanaenda maeneo ya chini Kabisa àmbapo wanadai Huko kûna baridi la kufa Mtu hivyo waliwakataa kuwabeba.

Kuangalia saa inaniambia Saa tisa. Mpaka asûbuhi yalibaki masaa matatu tuu. Nikaona sina haja ya kuchukua Lodge. Nikaamua kukesha na wale Vijana kupata uzoefu mpya.

Aiseeh! Maisha haya, ukiona unapata chàkula na unaishi Vizuri Mshukuru Sana Mungu. Kûna Watu wanahangaika na wanafanya Kazi katika mazîngira Magumu hasa ikiwemo hawa bodaboda wa Mafinga.

Niligundua pia Vijana wa bodaboda wa Mafinga wanajitambua na kuelewa mambo ya kitaifa kama mambo ya Katiba, mambo ya Haki za kiraia na mambo ya Kisiasa ya Chadema na ccm.
Ingawaje wamekata TAMAA na Maisha, wanafanya mambo ilimradi.

Zaidi, niliwapenda Kwa Sababu licha ya Hali ngumu ya Kazi Yao lakini haikuwaondolea Ûtu na ukarimu Kwa Wageni àmbao tulifika pale Stendi.

Tofauti na maeneo mengine ya nchi niliyowahu kufika Kama Kahama Mjini, Mwanza mjini, Arusha Mjini, Mbeya Mjini, Moshi Mjini, Morogoro Mjini, na Dsm. Àmbapo Miji hiyo ukifika utakutana na usumbufu wa bodaboda au wapiga debe wakikung'ang'ania kama Mpira wa Kona.

Mafinga majira ya usiku ukishuka bodaboda watakuja lakini hawatakusumbua.

Pia suala la utapeli WA nauli Mahali unapoenda nimegundua Hawana TAMAA ndogondogo,
Nakumbuka Wakati fulani nilifika Arusha Saa saba Kasoro Usiku, kuuliza bajaji Ilipo hoteli àmbayo najua Kabisa Ipo upande wa Nyuma Kwa umbali usiozidi kilomita Moja, lakini Baadhi ya madereva wengi wa Arusha wanatamaa, hizô nauli walizokuwa wanataja utabaki kuwaonea huruma, na wewe hata kama unapajua jifanye upajui ili upime uaminifu wao.

Vijana uaminifu ni Jambo kûbwa Sana. Eleweni Siku hizi Mtu hawezi kwenda sehemu pasipo kuwa na ABC za muhimu za Eneo àmbalo anaenda.

Lazima Mtu aulize nauli ya Eneo analoenda Kabla hajafika Hapo Stendi, ajue bei ya hoteli au lodge atakayoenda Kulala, na umbali WA lodge au hoteli hiyo kutokea Stendi.

Hongereni bodaboda wa Mafinga Kwa kuwakilisha Vijana wenzenu WA Hapo Mafinga. Nimewapa marks 70%.
Hii inaonyesha kama utapata kijana wa huku kûna uwezekano akawa mwaminifu ingawaje haimaanishi Hakuna àmbao siô waaminifu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa, Mafinga
 
Kuna kipindi nilienda mafinga nikapanda bodaboda saa 8 usiku ilibidi nikumbatie exhaust ya pikipiki kwasababu ya baridi

Asûbuhi imefika, napanda boda dadeki, mishipa ya kichwa inauma Kwa kupulizwa na Upepo, Lips za midomo inauma na ukisema uachie mdomo meno yanagongana na unaweza kujing'ata.
Huku siô poa
 
1. Tembea duniani ukutane na baridi. Ya Mafinga cha mtoto.

2. Niliwahi kuishi Lesotho baridi mpaka Maji kwenye mambomba yanaganda. Mambomba hayatoi maji.

Kwa wale ambao hawana mpàngo wa Kutoka nje na wanataka kujua baridi NI nini, waende njombe au Mafinga.
Utalii wataufurahia
 
Back
Top Bottom