- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Waziri wa fedha alisema hakuna wizi serikalini ndio maana maendeleo yanaonekana.
Je, ni kweli hakuna wizi Serikalini?
Kauli yake ina ukweli kiasi gani? Jamiicheck tunaomba mhakiki suala hili.
Je, ni kweli hakuna wizi Serikalini?
Kauli yake ina ukweli kiasi gani? Jamiicheck tunaomba mhakiki suala hili.
- Tunachokijua
- Wizi ni wakati mtu mmoja au kikundi kinachukua kutoka kwa watu wengine au mtu mwingine kitu chochote kisichokuwa chao au halali kukichukua, kwa mfano pesa au habari bila idhini ya wamiliki. Mtu aliyehukumiwa kwa wizi anaweza kuitwa mwizi.
Kuna aina nyingi za wizi, kwa mfano kwa kunyakua, kwa kuvunja milango au madirisha, kwa kuingilia kompyuta na kuchukua taarifa au kubadili taarifa ili ujipatie kitu kisicho chako au kupindisha hesabu na kuchukua fedha, vitu au kufanya ubadhilifu wa mali za umma na pia kutumia mamlaka ya kiofisi kujipatia fedha au mali kinyume na taratibu. Duniani kote wizi ni kitendo kiovu na unaadhibiwa na sheria za nchi husika.
Hivi karibuni kumezuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali kuhusu kauli iliyowahi kutolewa na Waziri wa Fedha Dr. Mwigulu Nchemba, Oktoba 28, 2023 kuwa sasa hakuna wizi wa fedha Serikalini, na kwamba Rais Samia kafanya makubwa kutokomeza kabisa wizi wa fedha za umma Serikalini. Kauli ya Mwigulu Nchemba kuwa hakuna Wizi Serikalini huku watu wakihoji ukweli wa kauli hiyo wanaonesha kutokubaliana na kauli hiyo.
Je, Ni kweli hakuna wizi Serikalini?
Suala la kuwepo kwa wizi Serikalini sio suala geni wala jipya kwani limekuwepo kwa muda mrefu kwa awamu zote za Serikali, ambapo katika awamu hii ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu suala la wizi Serikalini limejitokeza pia, miongoni mwa watu waliotoka hadharani na kuzungumzia suala la kuwepo kwa Wizi Serikalini ni Rais Samia ambapo Agosti 27, 2023 akiwa mkoani Pwani, katika hotuba yake ya kufunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa alisema amebaini mtandao wa kuchepusha fedha za umma huko Mbeya.
Pia wabunge wamekuwa wakipigia kelele juu ya wizi wa fedha za umma, Viongozi na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali imebainisha kuwepo kwa hati chafu zinazoonesha kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za umma, Pia TAKUKURU wameendelea kubaini kuwepo kwa watu wanaofanya wizi wa fedha za umma.
Hivyo basi, kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingi zinazoonesha uwepo wa wizi na ubadhilifu wa fedha na mali za umma Serikalini, Kauli ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kuwa hakuna wizi Serikalini ni kauli ya uzushi isiyo na ukweli wowote.
Pia soma
Mwigulu Nchemba-Out of touch. Anasema hakuna wizi serikalini, Rais ampa mfano wa mtandao wa wizi Mbeya
Rais Samia: Mbeya wametengeneza mtandao wa kukusanya Fedha kisha zinachepushwa na kuingia mifukoni kwao ilhai kuna Viongozi Wakuu pale!