Hakunakiri Namba ya mtihani na Ajira portal iko under maintenance afanyaje?

G.T.L

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
1,254
Reaction score
2,519
Wakuu, kuna aliyepitia changamoto kama hii ya ku Log in kwenye mfumo jana au leo akakuta Under maintenance?

MREJESHO: Wakuu naona mfumo umefunguka tayari mambo yako vizuri
 
Attachments

  • Screenshot_20240903_212739_Chrome.jpg
    Screenshot_20240903_212739_Chrome.jpg
    162.7 KB · Views: 26
Ishakula kwake
Nayo ni moja ya interview
Sasa kwanini hawakutoa ufafanuzi mapema kwamba waombaji wanakiri hizo namba haraka endapo walijua watafunga mfumo?
 
Kama alitumia chrome . Fungua chrome kisha fuata hatua zifuatazo

1. Juu kulia kuna vidot vitatu, bonyeza hvyo, zikuta option nyingi

2. Nenda option ya Setting

3. Baada ya setting nenda password manager

Ukifika hapo utakua username na password zote ulizowahi kuzi save kwenye sites mbali mbali ulizoingia. Kisha tafuta ajira portal. Ukibonyeza itakuonesha user name na password
 
Asante kwa maelezo mkuu, ila shida sio password wala username bali shida ni mfumo unaandika uko under maintenance na dogo anatakiwa aingie achukue namba ya mtihani aliyotumiwa na utumishi kwaajili ya usahili
 
Hujamuelewa, ukishaingia kwenye account ya ajira portal Kuna sehemu unakuta umetumiwa namba ya mtihani na kwa kuwa account ya ajira portal Iko under maintainance hakuna namna yyte anaweza kufanya kupata hiyo number mpaka account irudi hewani.
 
Kwanini hawatumi kwenye email?
Wabongo wengi tuna uzembe, kujua namba nayo kunahitaji kila muda mtu alog-in kwenye mfumo? Si anapiga picha tu na simu anakaa nayo, au anaandika pembeni. Hawa madogo wana uzembe mwingi sana
 
Hakuna uzembe wwte hapo kwanza ukiingia kwenye account hawakuambii kwamba hii ndio namba Yako ya mtihani unakuta imeorodheshwa tu pale
 
Mwambie dogo aende kituoni na kitambulisho, namba atapewa huko huko na msimamizi
Kama hana kitambulisho mwambie aende na cheti cha form four au hata cheti chochote rasmi chenye picha yake ili wajiridhishe kuwa ni yeye amekuja kufanya mtihani...
Kuhusu website; watu walilalamika kupangwa vituo vya interview shaghala baghala naona wakaitoa hewani...... sijui ambao walikuwa hawajatazama, labda watasogeza tarehe mbele
 
Hakuna uzembe wwte hapo kwanza ukiingia kwenye account hawakuambii kwamba hii ndio namba Yako ya mtihani unakuta imeorodheshwa tu pale
Uzembe. Graduates Kuna vitu hahitaji kuambiwa. Number inajulikana

Hivi mmeshawahi kufanya aptitude test za taasisi za kimataifa? Maana hii hulka yenu inatisha aisee
 
Huko kimataifa umeenda mbali ndugu wengine utumishi ndio mara ya kwanza kufanya interview tuache ujuaji wazembe ni hao utumishi maana kama wanaweka vitu kama hivyo kwenye account binafsi ya mtahiniiwa na account imezingua wao ndio wanaotakiwa kuutafuta alternative.
 
Subiria ifike mida ya wanga. Utafunguka.
 
Asante kwa maelezo mkuu, ila shida sio password wala username bali shida ni mfumo unaandika uko under maintenance na dogo anatakiwa aingie achukue namba ya mtihani aliyotumiwa na utumishi kwaajili ya usahili
Aende tu, kabla hawajaingia kwenye mtihani aeleze tu watamsaidia kupata namba.
 
Hakuna uzembe wwte hapo kwanza ukiingia kwenye account hawakuambii kwamba hii ndio namba Yako ya mtihani unakuta imeorodheshwa tu pale
Mkuu una akili nyingi sana kama Mesut Özil, nimependa responses zako.
Splendid! 👊
 
Back
Top Bottom