Nimemaliza kupiga kura yangu hapa Ilkiurei nje kidogo ya mji wa Arusha, watu ni wengi sana, kuna utata wa baadhi ya majina ya watu kutoonekana lakini waangalizi wako makini sana kuwaelekeza wapiga kura namna wanavyoweza kutambua vituo vyao kwani wengine majina yao yamehamishiwa vituo vingine tofauti na walipojiandikishia. Inatia moyo sana jinsi upigaji kura unavyosimamiwa hapa.
Nimejaribu kudodosa kidogo kujua msomamo wa watanzania, kwa kweli CCM mnakazi kwani kila niliemuuliza nini hasa kilimsukuma kuwahi kiasi hicho kuja kupiga kura, jibu lilikuja tofauti na nilivyotegemea. Mzee mmoja kaniambia amechoshwa na uongozi usio na maslahi kwa wananchi na sasa kawahi ili aitumie haki yake vizuri kumchagua Dr. Slaa kwa mabadiliko ya kweli, anasema "pamoja na uzee wangu naamini Dr. Slaa ataniwezesha kufanikisha ujenzi wa kibanda changu" inatia moyo sana!