Tetesi: Hali mbaya uakandarasi KONOIKE yabwaga manyanga, yafunga ofisi Tanzania.

Tetesi: Hali mbaya uakandarasi KONOIKE yabwaga manyanga, yafunga ofisi Tanzania.

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Katika hali ambayo si ya kushangaza sana kampuni maarufu ya Kijapani ,KONOIKE, wamefungasha virago na kufunga ofisi zao Tanzania.
Haiko wazi kwa nini KONOIKE wanaondoka lakini hii ni kampuni ya pili ya Kijapani kuondoka Tanzania.
Miezi takriban minne iliyopita, NATIONAL PANASONIC, kampuni iliyokaa Tanzania karibia miaka 50 toka enzi za Mwalimu, nayo ilifungasha virago.
Tunakumbuka redio za mkulima NATIONAL 177 na 277.
Huu mtonyo ni kutoka kwa mdau Wizara inayosimamia zege.
 
Twafwaa! Zimbabwe hiyoooo inatunyemelea kwa kasi!
Konoike
wameishitaki Jamhuri kwenye mahakama nchini Marekani halafu unategemea Jamhuri itawapa tena kazi za Ujenzi?

Hii ilikuwa ni lazima tu wabwage manyanga na kurudi kwao kama kweli wameondoka.

Soma hapa;
LINK>>>KONOIKE CONSTRUCTION CO. LIMITED v. MINISTRY OF WORKS, TANZANIA et al (1:17-cv-01986), District Of Columbia District Court
 
Konoike ilishapotea kwenye ligi za ukandarasi miaka mingi,ilikuwa kmpuni kubwa miaka hiyo,iliporomoka na kuuza karibu kila kitu kwa aliyekuwa sub contrctor wake Estim ambao ndio wanatamba kwa mijengo mingi mikubwa Dar
 
Katika hali ambayo si ya kushangaza sana kampuni maarufu ya Kijapani ,KONOIKE, wamefungasha virago na kufunga ofisi zao Tanzania.
Haiko wazi kwa nini KONOIKE wanaondoka lakini hii ni kampuni ya pili ya Kijapani kuondoka Tanzania.
Miezi takriban minne iliyopita, NATIONAL PANASONIC, kampuni iliyokaa Tanzania karibia miaka 50 toka enzi za Mwalimu, nayo ilifungasha virago.
Tunakumbuka redio za mkulima NATIONAL 177 na 277.
Huu mtonyo ni kutoka kwa mdau Wizara inayosimamia zege.
Huo ndio mwanzo wa anguko
 
Back
Top Bottom