Hali ngumu sana mtaani, unaweza kuuawa kwa sababu ya Elfu 20

Hali ngumu sana mtaani, unaweza kuuawa kwa sababu ya Elfu 20

Mkuu laki kwa siku ni matumizi ya kawaida tu sema tunatofautiana ufukara, mfano wafanyakazi wengi wana magari ambayo huwarahisishia usafiri kwenda makazini, lakini huwezi kuwaweka kwenye kundi la watu wenye vipato vya juu. Ukijaza tu mafuta ya kwenda na kurudi kazini, ukapita sokoni na dukani kwa mangi kidogo hiyo laki hutaiona, hapo hujapigwa mizinga ya hapa na pale na kubananishwa na trafiki barabarani.
Haelewi
 
Tukiacha kundi dogo la Viongozi wa Kisiasa wa Chama kilichojimilikisha madaraka, kwa kweli hali ya maisha kwa Wananchi ni ngumu sana huku mtaani,tuache kuvunga..

Hela hakuna wakuu, Ukitoka nyumbani na sh. laki moja unarudi huna hata sh. 100...bila shaka hali hii hainikabili mimi peke yangu

Hela hakuna mazee, Mishahara haitoshi na vimiradi vya kijasiriamali tunayojaribu pia vinakufa katika mazingira ya kustaajabisha sana

Ukikutana na Vijana waliomaliza Vyuo miaka miwili-mitatu iliyopita Utawaonea huruma, wamechoka, wamekonda, hawana tumaini...

Wafanyakazi wa Sekta ya Umma wako hoi

Wafanyabiashara taabani

Saivi unaweza kuviziwa getini kwako ukala shaba kisa tu Sh. elfu 20...

Hali ni ngumu sana, sema inaelekea wengi tumeamua kufa na tai shingoni..
Hatari sana
 
Back
Top Bottom