Hali ngumu ya Maisha kwa Wananchi: Mwalimu wa Chuo Kikuu amlilia Rais Magufuli anusuru wafanyakazi

Hali ngumu ya Maisha kwa Wananchi: Mwalimu wa Chuo Kikuu amlilia Rais Magufuli anusuru wafanyakazi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Mheshimiwa Rais, wafanyakazi tunakuomba msamaha

FRIDAY JANUARY 29 2021


Mheshimiwa Rais, nakusalimia kwa heshima na taadhima, Mimi kijana wako naendelea kulitumikia taifa nikiwa kituo changu cha kazi hapa Mlimani, kuna jamaa wengine wanapaita Jalalani, ingawa silipendi kabisa hili jina.

Mheshimiwa Rais, nakusalimia kwa heshima na taadhima, Mimi kijana wako naendelea kulitumikia taifa nikiwa kituo changu cha kazi hapa Mlimani, kuna jamaa wengine wanapaita Jalalani, ingawa silipendi kabisa hili jina.

Kilichonisukuma kukuandikia ni baada ya kukutana na Profesa mmoja akinunua mihogo kwa ajili ya chakula cha mchana, mitaa ya jirani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Profesa huyo kapandishwa cheo mwaka jana, lakini bado hajaanza kulipwa mshahara wa uprofesa hadi sasa.

Nilipomuuliza kwanini ananunua mihogo ya Sh2,000 akadai kuwa ‘purchasing power’ yake ni kidogo na haijaongezeka tangu uingie madarakani. Nilimkemea kwa niaba yako kwa sababu anakuonea; umekuwa ukipambana kukuza uchumi wa nchi.

Ingawa kiukweli wako wafanyakazi wengi wa kundi lake ambao hadi sasa wanalilia kulipwa mishahara stahiki kwa muda mrefu, lakini hawaoni dalili zozote. Na wengine bado wanasubiri malimbikizo.

Ukiacha maprofesa, wapo manesi, walimu, waganga, mabwana na bibi shamba na mifugo, askari polisi, magereza, uhamiaji, makarani, makatibu muhtasi, wakunga, waganga wa maabara, mafundi umeme, wakufunzi na wahadhiri, na wengine wengine. Orodha ni ndefu, nao kilio chao ni hicho hicho.

Nimekusanya sahihi zao kutoka maeneo mbalimbali ya Tandahimba, Newala, Namtumbo, Madaba, Ludewa, Makete hadi Ileje, Nkasi, Mlele, Buhigwe, Kakonko, Karagwe, Ngara, Busega, Itilima, Mkalama, hadi Rorya. Nilitaka niwakatae jamaa wa kutoka Runzewe, Katoro na Bwanga nikiamini wanaweza kukufikishia wao wenyewe, lakini nikaona si vibaya ngoja niwawakilishe.

Ila mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya hawahusiki na msamaha.

Wafanyakazi wengi uwezo wao wa kufanya manunuzi ni mdogo. Kiasi kilichokuwa kinaingia mwaka 2016 ndo hicho hicho hadi mwaka 2021, wanatamani waone nafuu fulani kwenye uwezo wao wa kuhimili manunuzi kwa ajili ya kuhudumia familia.

Naona kama wenzetu wa Bodi ya Mikopo walinusa hilo mapema . Wao wakaweka kipengele cha ‘value retention fee’ toka 2016 kulinda thamani yao ya hela. Walijua kila mwaka thamani ya hela inashuka kwa asilimia sita na ikifika 2021 hela waliyoweza kumpatia mwanafunzi 2016 itakuwa haitoshi 2021, hivyo wakapachika hicho kijamii kinaitwa ‘value retention fee’.

Ukiacha Bodi ya Mkopo kutukata asilimia 15 ya mkopo, kuna hawa jamaa wa TRA nao naona wameamua kutukomalia zaidi wafanyakazi tuwe na TIN. Wamesema bila TIN mwezi huu wa Januari tunatoka bila bila kwenye akaunti zetu.

Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii kuzishukuru benki tunazopitishia mishahara yetu. Ingawa wanatengeneza faida, lakini huwa wanatuokoa. Baada ya mshahara kuingia wakakata hela yao waliyonikopesha mwezi uliopita. Nilipochungulia kilichosalia kikawa hakitoshi kunifikisha wiki moja mbele, basi siku hiyo hiyo nikakopa tena ‘salary advance’. Sasa hivi ndo ‘salary advance’ ndio mkombozi wetu.

Mheshimiwa, siyo kwamba tunapenda kuishi hivi, ila majukumu ya kifamilia ni mengi na uwezo wa kuyamudu kwa hiki tunachopokea ni mdogo, maana wakataji ni wengi.

Sitaki kuingia nao ugomvi lakini mishahara yetu inachukuliwa na TRA, HESLB, NHIF, PSSF/NSSF kwa sehemu kubwa.

Mheshimiwa Rais, nisikuchoshe na maneno mengi. Wafanyakazi wenzangu walioko Serikalini wameniomba nije kukuomba radhi, kama wakati wowote tangu ukiwa waziri hadi Rais kuna mahali tulikukosea, tunaomba msamaha. Maisha yetu huku mtaani ni magumu, hatuna furaha, baadhi yetu tuna sura za uzee kumbe bado vijana.

Ndoa zetu sasa hivi ziko hatarini, wake zetu wanatudhania wote tuna tabia za wangoni kumbe shida yetu ni hela. Tuna changamoto nyingi za kifamilia, kijamii na binafsi.

Sasa hivi hata viongozi wa dini tunawaona kama wapiga dili kwa sababu nao hawajui tumesahauliwa kwenye ‘value retention’ ya mishahara yetu, utawasikia wakisema, ‘safari hii tegemeza jimbo ongezeko ni asilimia 40 ya mwaka jana’.

Wakiangalia vitambi vyetu wanajua tuna hela kumbe thamani ya mifuko yetu bado ni ile ile ya mwaka 2016.

Tuonee huruma Mheshimiwa Rais, usishangae asilimia kubwa ya wafanyakazi wa Serikali tukianza kukusanya chupa tupu mtaani na kuzigombania kwenda kuuza. Natumaini wewe ni baba mwenye huruma utasikiliza maombi yetu ya msamaha.


Imeandikwa na Faraja Kristomus, mwandishi anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 
Mhadhiri ameandika ujumbe kiungwana sana. Ingekuwa mitano ya kwanza angepata misukosuko ya wapambe kwa tafsiri ya uchochezi ila kwa sasa haina shida na wala hatadhurika ukizingatia mlengwa hana cha kupoteza tena kutoka kwa watumishi.

Kwa hali ilipofikiwa hata watoto majumbani wanajua kwamba "Wazazi watumishi wapo" hoi.

Naamini kama aliiona ile Clip ya Shule ya Msingi kule Ubungo na akaifanyia kazi haraka hata huu uzi ataufanyia kazi haraka. Mwandishi angetupia picha ya Prof. akiwa na furushi lake la mihogo ingenoga zaidi.
 
Ugumu wa maisha unachangiwa kwa kiasi kikubwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu

Mtu achukue 15% per month kwenye gross salary na deni lina-automatic renew unategemea nini?

Na serikali haijawawahi kuongeza salary hata kwa bahati mbaya

Naona makato ya bodi wayaondoe kwa sisi tunaoitumikia serikali; walimu tupo vijijini nyumba hamna miundombinu mibovu wanafunzi nyomi na bodi juu. Mpaka tunaona kuna faida gani ya kuwa mtumishi wa umma?

Hii haipo sawa
 
Mihogo ni chakula cha kitajiri nenda katikati ya jiji ukaone inavyouzwa bei mbaya!
 
Tulikotoka ni mbali, Kama asingekuwa kikwete na Mkapa tusingefika hapa. Walituletea jini Sasa linanyonya damu ya kila mmoja. Hadi 2025 tutakuwa tumedhoofu bin Hali. Nola huenda akatunusuru kwa namna ya pekee
 
Aiseeeee Kama ulikua unalipwa 420000, 2016 na mshahara ujapanda ni uonevu wa Hali ya juu, maisha yamepanda angalia sukar, mafuta nk, afu 15% ya loan bod juu yake, nabaki kusema 5tena
 
Mihogo ya buku mbili si haba, kuna Masela wanashindia Muhogo wa mia.

By the way, Prof hajaoa?
 
Hao mafropesa hawataki kusema ukweli ili kupalilia vyeo
Wale tu hata njaa watashinda
 
Ngoja niamke niwahi mihogo kbla haijaisha, lakin kwel huyu jamaa sijui hasikii kilio cha watu au ndo ukishashiba humjui mwenye njaaa,.
 
Hata mleta mada ameleta hadithi tamu nzuri na ya kuvitia!
Huu ni ukweli wa "Kiutalii" wa kufurahia kukaa kwenye nyumba za nyasi na kulipia bei kubwa lakini tukikuambia yawe maisha yako rasmi na ya kudumu hutathubutu.
 
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Hivi professor mzima uzalendo unamshinda kabisa
Sijui unalalamika nini
Watanzania inatakiwa tufikie pahala tutangulize maslahi ya nchi kwanza
Professor unajua kabisa zaidi ya theluthi mbili ya mapato ya nchi inaenda kwenye mishahara
Hivi professor hauoni nchi ilivyopendeza?
Hauoni flyover?
Huoni Midege hewani?
Huoni mabarabara?
Huoni mashule?
Huoni vituovya afya?
Tupo Uchumi wa kati
Shule bure
Huduma za afya bure
Yaani Tanzania ya Magufuli neema tupu
Kuanzia Wafanyabiashara. Wafanyakazi hata Wakulima maisha ni bam bam isipokua wapiga dili Ndio wanaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Professor hawezi kuandika upuuzi kama huu.Wala professor hawezi kupaita Mlimani Jalalani.Nina wasiwasi na elimu ya huyu mfanyakazi.Unaanzaje kulalamika kula mihogo ilhali kuna wengine wapo mtaani hawana hata hiyo ajira wanashindia mikate siku nzima? Huku ni kukosa uzalendo na dharau kwa wasio na kazi.
 
Back
Top Bottom