DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mwalimu wangu Mr. Kaluhawe alikuwa na ulemavu wa kutoona. Akiwa anatoa lecture pale M9 SAUT mida baada ya lunch, ungemsikia anasema, "I see you sleeping"! Ahahahahaha! Alikuwa mwamba sana!
Hawa watu wanavipaji vya ajabu na vya kutisha sana!! Ni vile serikali imeshindwa kutambua uwezo wao!!!

Nawaambia tena, Laiti Kama mngejua kwamba mtu mwenye ulemavu anatumia ubongo wake kwa asilimia kubwa sana kuliko hata mtu ambaye Yuko physical fit msinge zarau Walemavu...

Magenius wengi mara nying wanakuwaga na kasoro ndogo ndogo Kama hizo ambazo nyie mnaita ulemavu..

Hakika nchi inakosa watu wenye akili nying sana, ni basi tuu
 
Kuna kijana mmoja japo sikutaka kuwapa hii story, coz ni sad story lakn ngoja niwaelezee kilichomtokea!!

Wakati wa usaili flani, zilikuja Cv na barua za watu wengi sana katika dawati la ajira KAMPUNI hiyo..

Lakini Ma HR walipendezwa na CV na cover letter moja wapo kwakuwa iliandikwa kwa ustadi mzuri sana.

Wakaagiza aitwe kwenye usaili, maana hata nafasi yenyew ni ya mtu mmoja kwahio nafikiri waliona Waite mtu huyo tu. Kutokana na uandish wake mzuri

Sasa wakati amefika, ile kuingia kwenye chumba Cha interview, ghafla kukawa kimyaa.. hii yote ni kwamba walipigwa na butwaa baada ya kuona mtu Yuko chini anatambaa.

Anasema kijana yule kwamba, kati ya wote ni mmoja tu angalau alijitahid kuongea pale!! Na kauli aliyoambiwa ni kwamba "Okay tumepokea barua yako tutakupigia simu, tunaomba uende"
Kwakuwa hakuulizwa swali lolote alirudi analalamika na kilio.

Kwa bahati mbaya hivi sasa kijana alishafariki, wengi waliomwona walisema kuwa alikuwa na mawazo mengi sana, alikonda! Mwisho akawa amefariki😢

All in all, (RIp comrade) tutapambana mpka tueleweke kweny jamii.

Tuna uwezo mkubwa sana, mtu ajiri jamii yetu tunawaomba.. lakin pia tengenezeni system nzuri ieleweke ya mtu mwenye ulemavu kuajiriwa
 
Japo nataman kuwepo na system maalumu ya kuwajiri wenye ulemavu, ili isije ukawa hawa wakaajiri kwakuwa tu watu wamepaza sauti, then mwakani makosa yakajirudia vilevile kwakuwa labda hakuna wa kusema hili.

System nzuri ya kuajiri, hata wakiwa na namna Yao ya kuwa recruit itapendeza sana
Ni kweli Mkuu

Wakati mwingine majibu ya kudumu hupatikana kutokana na hoja kama hizi
 
Natamn mods wanisaidie kweny Uzi huu!! Angalau sauti yangu isikike!
 
Mkuu,

Shukrani sana kwa kunitoa tongo tongo, ni kweli kama ni wajibu na sheria kupata hizo favors na ikafanyika vinginevyo basi ni ukiukwaji mkubwa sana wa haki, ukizingatia tunatambua namna ndugu zetu mnavyopata changamoto mpaka kufika hatua kubwa za kielimu kutokana na changamoto za miundombinu isiyo rafiki.
Watu wengi hawafahamu hili, nataman watu waelemishwe
 
Mkuu pole sana. Nenda gran melia hotel -Arusha. Geti la tatu dogo la juu kabisa kulia kama unaelekea philips kutokea round about ya impala ( au kama unatokea philips ni geti la kwanza kushoto) . Kuna kitengo pale kinatoa ajira kwa walemavu sikumbuki jina kinaitwaje.. ila nenda pale wale wazungu wana ajiri walemavu tuu kwa asilimia 99%
Hao jamaa naweza pata mawasiliano nao mkuu!!
 
Pole sana ndugu yetu 😔
Jaribu pia kupeleka CV kwenye taasisi za kimataifa hata kama hawajatangaza ajira omba kazi kama intern.

Kama uko interested njoo inbox nikupe suggestions za ambazo nazifahamu ambapo wana prioritize diversity.
☝️
 
Back
Top Bottom