Hali ninayokutana nayo katika Biashara inatisha nimefunga biashara 3 nimebakiza moja inayopumulia mipira, Msaada wa kiroho unahitajika

Hali ninayokutana nayo katika Biashara inatisha nimefunga biashara 3 nimebakiza moja inayopumulia mipira, Msaada wa kiroho unahitajika

Yani izo ndoto za kurudi kijijini na mashuleni zote zinaashiria umetupiwa roho ya kurudishwa nyuma ndo mana hamna jambo linaloenda mbele
Na kutoka kwenye Ivo vifungo ni kupitia maombi coz uko kwa waganga unaenda kupotea mazima.
Kuna Uzi umu ndani umezungumzia vizuri maswala ya kiroho ukiufatilia itakusaidia sana.
Uzi wenyewe unaitwa

Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo​

Exactly mkuu
Ni Uzi mzuri mnoo
 
Mkuu kwanza Pole sana
Pili; Jambo lako linatibika, ila kwasababu umeamua kutumia solution ya waganga, mimi sijui chochote kuhusu upande wa giza, ukitaka upande wa nuru niambie nikusaidie hapahapa
Mkuu hii changamoto wanaipitia wengi ila hawajapata nafasi ya kuleta vilio vyao hapa jf, hivyo basi, kwa heshima na taadhima, nikuombe ushushe nondo kupitia uzi wa huyu member na utaponya walio wengi. Karibu
 
Sijawahi kuishi kwa mashart mkuu, lakini kwa hii fedheha ninayopitia saiz hata kama kuna masharti nitakuwa tayari kuyapokea kwa mikono miwili, usiombe uone unafirisika mkuu hiko kiskie kwa jirani yako ila kisiwe kwako. Unaweza kuwa unaongea peke yako njian
Kuna uzi humu unazungumzia waliowahi kupata pesa kisha wakafirisika, uko hapa jukwaani! hakika maumivu ya kufirisika anayajua mhusika na mungu wake..ni mapito magumu na ya kuogofya sana!
 
Cha ajabu hata usiku nikilala naota ndoto za kutisha kama nipo
kwetu kijijini, tena saa zingine naota nipo shule ya msingi
nasoma...

Kwenye kuota upo class unapiga kitabu hii ni ndoto mbaya sana umesha kanyagishwa kitu tena utakuta ni ndugu yako

Pole sana mwisho wa picha utapata ajali na mwisho wako utakuwa hapo.. Wakati unapambana ujinasue na yeye anapambana na wewe
 
Kuna hali mbaya ya kibiashara mtaani. Unakuta fremu kila baada ya kodi ya kwanza kuisha mtu anaachia haemdelei. Kama hujui unaweza fikiri kuna biashara kwasababu fremu zinapata watu kumbe kila mkataba ukiisha anakuja mpangaji mpya.
 
Habari Wakuu, Maelezo mengi yatawachosha...
Nilianza Biashara 2019, ya umachinga nikawa nachukua bidhaa mjini napeleka vijijini, Biashara ilikubali nilikuwa napiga profit nzuri sana kwa siku, Biashara yangu haikuwa na ushindani wala haikuwa ya kufikilisha kama kuna faida napata, Ila nilikuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya Laki moja hadi 3 kwa siku,

Nikaendelea na Biashara hii kwa mda wa Mwaka mmoja nikaamua kununua kiwanja na kujenga nyumba yangu wa kwanza ya kuanzia maisha, nikahamia, Nikaendelea kukomaa nikajenga nyumba ya pili ya ndoto zangu...

Kwa bahati nzuri location niliyojenga kwa mbele kuna barabara nikaona sio mbaya nikajiongeze nikajenga Viflemu vya biashara nikapata na wapangaji nikaanza kupokea vikodi. Kiukweli nilianza kuona natimiza ndoto kimasihara sana.

Mwaka juzi nikapambana nikapata kigari nikanunua,, na baadae nikawaza biashara ya Umachinga sio Biashara ya kudumu, Hivyo nikaona nijiwekeze nikaona ni bora nifungue vitega uchumi vingine ili nitanue biashara..

Nikaamua kufungua Duka la kwanza katika moja ya flem zangu, Mwanzoni biashara ilienda vzuri hadi nikawa najiuliza nilikuwa nachelewa nini,,,

Baadae nikaona shemej yenu nae anafaa apate biashara yake ili asinitegemee na Yy nikatafta location nikamfungulia Cafe ya kuuza misosi napo biashara ikatiki nikaongeza kipato zaid nikazidi kuinjoy..

Nikaona niongeze ofisi ya tatu, Nikafungua Duka la spea za pikipiki eneo baada ya kuona location inafaa, Biashara zikazidi kupamba moto.

Cha ajabu na cha kushangaza ni ndani ya Mda mfupi biashara zote zimesimama hakuna mteja anakuja dukani kwangu watu wanapita tu na kwenda kununua bidhaa kwingine, cha kusikitisha ni kwamba upepo umenata ofisi zote, Pale kwa wife vyakula vinapikwa vinatupwa, Dukani panya wanashambulia vitu bila huruma, na hakuna mteja, Duka la spea hakuna wateja na mafundi wamehama sina fundi wala bidhaa haziuziki.

Nimeamua kufunga biashara zote maaa naona ni hasara tupu, Kwanza nilianza na Mgahawa wa wife, likafuata Duka na hivi juzi nimemalizia kufunga Duka la spea

Nimeamua kurudia biashara yangu ya awali ya Umachinga ambayo ndio ilinipa msingi.. cha ajabu nayo saizi wateja wangu wanataka kunikopa tu hamna la maana. Natoka nazunguka narudi nyumbani na pesa ya kula tu hamna cha maana.

Cha ajabu hata usiku nikilala naota ndoto za kutisha kama nipo kwetu kijijini, tena saa zingine naota nipo shule ya msingi nasoma na mara zingine naota nimepakazwa kinyesi mwili mzima. Jaman wakuu tusaidiane hapa najinasua vipi.

Kwa upande wangu napendelea kujinasua katika hiki kifungo kupitia wataalam wa jadi ndipo imani yangu inanituma japo sijui ni wapi nitaanzia wala ni wapi nitaishia,
siwiwi na walokole kuponya tatzo langu, kama yupo ambae alishawahi kukutwa na janga kama hili na akachomoka na kurudi katika hali yake ya kawaida anisaidie Pm Iko wazi jamani. Ndugu tusaidianane, Napitia fedheha kubwa sana, Nimejaribu kushirikisha akili yangu ila imefika ukomo,

Napewa namba za wataalamu wengi ila ukimpigia katika maongezi pyschologically nawastukia ni wapigaji wengi wao wanajisifia ila ukipima maongezi yake unaona kama hayana uhalisia.. Na mwisho wanataka kutumiwa pesa ili wanisaidie.
Rudi nyumbn kaongee na wazee vizuri...anzia hapo hayo mengne watakuambia wao
 
Cha ajabu hata usiku nikilala naota ndoto za kutisha kama nipo
kwetu kijijini, tena saa zingine naota nipo shule ya msingi
nasoma...

Kwenye kuota upo class unapiga kitabu hii ni ndoto mbaya sana umesha kanyagishwa kitu tena utakuta ni ndugu yako

Pole sana mwisho wa picha utapata ajali na mwisho wako utakuwa hapo.. Wakati unapambana ujinasue na yeye anapambana na wewe
Upo mkoa gani?
 
Mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema Mola wangu Mlezi amenikirimu!

Na anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema Mola wangu Mlezi ameniacha.

Ni changamoto tu hiyo jipange upya chuma ilikua gear no 5 sahivi imekutana na mlima rudi 3, 2 kama kilima ni kikali anza 1.

Kwanza jikague kama ulimdhulumu mtu, jitahidi mpe haki yake.

Kama kuna mke wa mtu unatembea nae,tafuta namna ya kujiepusha nae.

Tenga muda wa falagha wa kuongea na Mungu wako hasa iwe usiku tulivu.

Tumia chumvi ya mawe kuogea husaidia kuondoa hizo balaa.
 
Yani izo ndoto za kurudi kijijini na mashuleni zote zinaashiria umetupiwa roho ya kurudishwa nyuma ndo mana hamna jambo linaloenda mbele
Na kutoka kwenye Ivo vifungo ni kupitia maombi coz uko kwa waganga unaenda kupotea mazima.
Kuna Uzi umu ndani umezungumzia vizuri maswala ya kiroho ukiufatilia itakusaidia sana.
Fata huu ushauri uliopewa nenda kwenye maombi kama upo dar nenda kkkt kimara korogwe au kkkt Kariakoo uponyaji bure dakika mbili tu umeoshwa kwa damu y’a Mwanakondo ( Yesu) stori kwisha nyota hiyo inarudi hayo mavi umechafuliwa ulimwengu wa roho wateja wanakuona unanuka hakuna atakaye sogea ndoto shule maana umerudishwa nyuma kijiji huo uchawi unatoka uko kwenu usipo angalia utarudi kijijini upo mjini kopo tu vitu vinaaanza roho then mwilini kwa waganga utapoteza ufalme kwa ufalme haufitiniki cha msingi atakuwekea jini lakutuliza kingine kuwa msiri asa kwenye maendeleo Bila nguvu y’a Mungu utoboi tumepita uko kwenye hizo ndoto za shule kuona unajisaidia choo kichafu ila niliposurrender mikono juu kwa Yesu kristo damu yake iliniosha nikawa mpya natembea kifua mbele atakayeroga kwa vida mu vya kuku sijui ng’Ombe anakutana na nguvu y’a damu
 
Yani izo ndoto za kurudi kijijini na mashuleni zote zinaashiria umetupiwa roho ya kurudishwa nyuma ndo mana hamna jambo linaloenda mbele
Na kutoka kwenye Ivo vifungo ni kupitia maombi coz uko kwa waganga unaenda kupotea mazima.
Kuna Uzi umu ndani umezungumzia vizuri maswala ya kiroho ukiufatilia itakusaidia sana.
Uzi wenyewe unaitwa

Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo​

Tatzo hawa wanaozungumzia haya mambo hawa reflect wanachozungumzia ndio maana hatuwaamini, unakuta mtu anakupa siraha tano za kiroho ila yeye bianfsi na wafuasi wake wanasaga baiskeli, tunapoteza uaminifu kwao.. ndio maana tunaona Waganga wa kienyeji baadhi ni wa kwel hapo sio wote
 
Kwanza jikague kama ulimdhulumu mtu, jitahidi mpe haki yake.

Kama kuna mke wa mtu unatembea nae,tafuta namna ya kujiepusha nae.

Tenga muda wa falagha wa kuongea na Mungu wako hasa iwe usiku tulivu.

Tumia chumvi ya mawe kuogea husaidia kuondoa hizo balaa.
Kuhusu kudhurumu sijawahi... kuhusu kula mke wa mtu labda kama nilikuwa sijui
 
mara ya mwisho kutoa sadaka lini???
mara ya mwisho kusaidia wenye uhitaji lini ???

watu wengi tunamtanguliza Mungu kwenye mambo yetu mwanzoni lakini pindi tu mambo yakianza kutiki automatically tunajisahau ukiweza kulishinda hili jambo lazima mafanikio yako yalindwe

my take.:: mimi sina dini yoyote lakini huwa naomba MUNGU maana naimani yupo na anasikia
 
Back
Top Bottom