Hali ninayokutana nayo katika Biashara inatisha nimefunga biashara 3 nimebakiza moja inayopumulia mipira, Msaada wa kiroho unahitajika

Biashara inayokuingizia faida ya laki 2 sijui 3 kwa siku mbona hela ndefu sana? Au ulikosea masharti
Hivi hamuwezi kufanya biashara bila ndumba?
Ina maana unafuata masharti bila akili yako
Yaani unamsikiliza mganga tu wa kuomba kuku eti
Sasa anza ya bila kumshirikisha mganga bali akili yako tu
 
Wapi niliandika hapo kuwa nilienda kwa mganga??

Mbona pesa ya kawaida sana ukipata sehem na kuna watu wanaingiza hizo pesa kawaida tu!
 
Rudi kwenye asili takatifu uchawi una nafasi ndogo sana ningekushauli sana ufanye meditation lakini kwa situation ulionayo sasa huwezi kufaulu hili kwa akili yako kutawaliwa na mapito unayo pitia.
Sasa fanya maombi yalio onganishwa na kufunga siku11 chakula chako iwe matunda katika hayo
tende👈 usikose.
HAKIKA UTAONA MIUJIZA MIKUBWA.
 
Habari Wakuu, Maelezo mengi yatawachosha.

Nilianza Biashara 2019, ya umachinga nikawa nachukua bidhaa mjini napeleka vijijini, Biashara ilikubali nilikuwa napiga profit nzuri sana kwa siku, Biashara yangu haikuwa na ushindani wala haikuwa ya kufikilisha kama kuna faida napata, Ila nilikuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya Laki moja hadi 3 kwa siku,

Nikaendelea na Biashara hii kwa mda wa Mwaka mmoja nikaamua kununua kiwanja na kujenga nyumba yangu wa kwanza ya kuanzia maisha, nikahamia, Nikaendelea kukomaa nikajenga nyumba ya pili ya ndoto zangu...

Kwa bahati nzuri location niliyojenga kwa mbele kuna barabara nikaona sio mbaya nikajiongeze nikajenga Viflemu vya biashara nikapata na wapangaji nikaanza kupokea vikodi. Kiukweli nilianza kuona natimiza ndoto kimasihara sana.

Mwaka juzi nikapambana nikapata kigari nikanunua,, na baadae nikawaza biashara ya Umachinga sio Biashara ya kudumu, Hivyo nikaona nijiwekeze nikaona ni bora nifungue vitega uchumi vingine ili nitanue biashara..

Nikaamua kufungua Duka la kwanza katika moja ya flem zangu, Mwanzoni biashara ilienda vzuri hadi nikawa najiuliza nilikuwa nachelewa nini.

Baadae nikaona shemej yenu nae anafaa apate biashara yake ili asinitegemee na Yy nikatafta location nikamfungulia Cafe ya kuuza misosi napo biashara ikatiki nikaongeza kipato zaid nikazidi kuinjoy..

Nikaona niongeze ofisi ya tatu, Nikafungua Duka la spea za pikipiki eneo baada ya kuona location inafaa, Biashara zikazidi kupamba moto.

Cha ajabu na cha kushangaza ni ndani ya Mda mfupi biashara zote zimesimama hakuna mteja anakuja dukani kwangu watu wanapita tu na kwenda kununua bidhaa kwingine, cha kusikitisha ni kwamba upepo umenata ofisi zote, Pale kwa wife vyakula vinapikwa vinatupwa, Dukani panya wanashambulia vitu bila huruma, na hakuna mteja, Duka la spea hakuna wateja na mafundi wamehama sina fundi wala bidhaa haziuziki.

Nimeamua kufunga biashara zote maaa naona ni hasara tupu, Kwanza nilianza na Mgahawa wa wife, likafuata Duka na hivi juzi nimemalizia kufunga Duka la spea

Nimeamua kurudia biashara yangu ya awali ya Umachinga ambayo ndio ilinipa msingi.. cha ajabu nayo saizi wateja wangu wanataka kunikopa tu hamna la maana. Natoka nazunguka narudi nyumbani na pesa ya kula tu hamna cha maana.

Cha ajabu hata usiku nikilala naota ndoto za kutisha kama nipo kwetu kijijini, tena saa zingine naota nipo shule ya msingi nasoma na mara zingine naota nimepakazwa kinyesi mwili mzima. Jaman wakuu tusaidiane hapa najinasua vipi.

Kwa upande wangu napendelea kujinasua katika hiki kifungo kupitia wataalam wa jadi ndipo imani yangu inanituma japo sijui ni wapi nitaanzia wala ni wapi nitaishia,
siwiwi na walokole kuponya tatzo langu, kama yupo ambae alishawahi kukutwa na janga kama hili na akachomoka na kurudi katika hali yake ya kawaida anisaidie Pm Iko wazi jamani. Ndugu tusaidianane, Napitia fedheha kubwa sana, Nimejaribu kushirikisha akili yangu ila imefika ukomo,

Napewa namba za wataalamu wengi ila ukimpigia katika maongezi pyschologically nawastukia ni wapigaji wengi wao wanajisifia ila ukipima maongezi yake unaona kama hayana uhalisia.. Na mwisho wanataka kutumiwa pesa ili wanisaidie.
Mkuu ngoja tumuite Mshana Jr atuelekezee hii
 
Usijichanganye kwenda kwa wanaojiita manabii, au makanisa sijui ya kiroho
 
Yani izo ndoto za kurudi kijijini na mashuleni zote zinaashiria umetupiwa roho ya kurudishwa nyuma ndo mana hamna jambo linaloenda mbele
Na kutoka kwenye Ivo vifungo ni kupitia maombi coz uko kwa waganga unaenda kupotea mazima.
Kuna Uzi umu ndani umezungumzia vizuri maswala ya kiroho ukiufatilia itakusaidia sana.
Hakuna cha maombi wala nini,makanisa na wachungaji wote matapeli tu, type ya kina kiboko ya wachawi
 
Kuna hali mbaya ya kibiashara mtaani. Unakuta fremu kila baada ya kodi ya kwanza kuisha mtu anaachia haemdelei. Kama hujui unaweza fikiri kuna biashara kwasababu fremu zinapata watu kumbe kila mkataba ukiisha anakuja mpangaji mpya.
Kama unataka uzoefu wa hali mbaya angalia watu walivyochoka,angalia bia hazitembei,wakora wameongezeka,bei hazina shida lakini Kuna kitu hakiko sawa kwa mtawala mkuu huenda alipora maisha ya mwenda zake
 
Back
Top Bottom