Hali ninayokutana nayo katika Biashara inatisha nimefunga biashara 3 nimebakiza moja inayopumulia mipira, Msaada wa kiroho unahitajika

""Cha ajabu hata usiku nikilala naota ndoto za kutisha kama nipo kwetu kijijini, tena saa zingine naota nipo shule ya msingi nasoma na mara zingine naota nimepakazwa kinyesi mwili mzima. Jamani wakuu tusaidiane hapa najinasua vipi.""


πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†

Shida ipo hapo chief! Ni mambo ya kiroho hayo.. 100%
 
Wajumbe wameshakupiga PINI.

Kama kuna bibi na babu zako waliofariki ongea nao uwaombe wakusaidie. Usikariri imani za kizungu utaangamia.

Rudi kwenye kitovu cha ukoo wako, omba msamaha, jinyenyekeze, jishushe toa maombi, utafunguliwa mpaka utashangaa.

Usiende kwa waganga, fanya mwenyewe.

Ukiendelea kung'ang'ania dini za kizungu utachakaa, utapigwa mpaka unyooke.

Wewe yesu unamjua?? umewahi kumuona? Anakujua?? UTACHAKAA.

Waulize wachaga wanaenda moshi kila disemba kufanya nini!

Cc: Extrovert DR Mambo Jambo
 
Nini unachoshauri wewe sasa
 
Hi ndoto YA kujisaidia Choo kichafu Hua inamaanisha nn
Kuchafuliwa ulimwengu wako wa roho kwanza kujisaidia tu ni Ishara ndani y’a mwili wako unau chafu na kujisaidia mazingira y’a Choo kichafu maana umezungukwa na ma roho machafu umenajisika connection na Mungu haipo hutamsikia utaona vitu vya gizani tu baraka zako zinaibiwa nyota unakuta cha muhimu kuacha dhambi ndo mlango wa mateso yote asa zinaa ni mbaya sana kuishi kwenye usafi na utakatifu
 
Kwahiyo mkali wa hizi kazi nani kati ya huyu na yule wa mwanzo 😊
 
Kwahiyo mkali wa hizi kazi nani kati ya huyu na yule wa mwanzo 😊
wataalam wanapiga kazi kulingana na shida uliyonayo.

mfano unaweza kuta shida yako ni kuondoa majini mahaba, ama umerushiwa majini... ukaenda sehem ukaaminishwa mtlm ni mkali sana ila hajabobea kwenye kuondoa majini

so unapewa Plan B
 
wataalam wanapiga kazi kulingana na shida uliyonayo.

mfano unaweza kuta shida yako ni kuondoa majini mahaba, ama umerushiwa majini... ukaenda sehem ukaaminishwa mtlm ni mkali sana ila hajabobea kwenye kuondoa majini

so unapewa Plan B
Yule wa nyungu ni mtaalamu wa nn sasa 😊
 

Huyo mzee bahati ndo wewe
 
Ukisoma haimaanishi unaacha asili mimi ni mwafrica ambae najua asili yangu kusoma haimaanishi kunafanya nisijue asili yangu na mababu zangu, hata hao wasomi unaowajua ww wanashiriki ibada ya kiganga maana ni jadi yetu waafrika
Una matatizo alafu mbishiii ,ka Muha, ushauri wangu jitathimini kuanzia tabia Yako baada ya kupata pesa ,hasa kwa wateja, tabia ya mkeo baada ya kupata pesa ,hasa kwa wateja, na Kisha kama wewe ni mwafrika halisi ,maagano uliyoweka tokea mwanzo, umechinja kuku wangapi ,kwa ufupi kafara, na matokeo yake yalikuwaje , nguvu yake ni ya muda Gani,!? Upinzani wake ni Nini!? Ie tabia zako halisi dhidi ya hizo kafara vinamatch!?


Zaidi uafrika wetu ni mzuri,lakini mgawanyo wake waga ni WA maumivu,utaambiwa inabidi utoe sadaka, sadaka yenyewe Sasa ,ikiwa ndogo ni wewe kujitia ulemavu, utasikia kata kidole, ,,, kama ulianza kwa imani zetu za kiafrika ,kubali kuwa masikini alafu ujianze na upya, Mali za imani za kiafrika waga ni kama za kuazimwa, majini yakiumwa njaa yanakutikisa ,


Bora usiamini hata hizo za wazungu ila uwe wewe! Bila ya kafara Wala damu,Wala sadaka za huko kwa mababu
 
Akili yako direct imekutuma huko ila hapo juu hakuna sehem nimeandika kuwa nilishawahi kufanya hizo vitu kwa hiyo kabla hujadandia mada za watu tafakari
 
Ukiona UNAOTA Mambo ya shule ya msingi mara kurudishwa kijijini jua haupo SALAMA.

NENDA KWA MWAMPOSA PALE KAWE OMBA KILA NJIA UONANE NAE AKUWEKEE MKONO KICHWANI THEN RUDI HAPA KUTUPA MWONGOZO.

NINA SHUHUDA NYINGI SANA ZA WATU KUINUKA NA KUFANIKIWA SABABU YA MAOMBI YA APOSTLE MWAMPOSA

Uzuri wa pale KAWE hakuna MASHARTI magumu Kama ya huko kwa waganga unako taka kwenda wewe jifanye Kama unaenda kujaribu zingatia haya nayo kwambia utakuja kunishukuru..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…