Hali si shwari chuo kikuu St John

Hali si shwari chuo kikuu St John

intruder

Member
Joined
Nov 25, 2014
Posts
47
Reaction score
16
Ikiwa ni wiki mbili toka wanafunzi wa St John waingie barabaran kupinga mambo mabalimbali yanayoendelea chuoni hapo, leo hii tena walimu na watumishi mbalimbali chuoni hapo wamekuwa na vikao visivyoisha kujadili mustakabali wao chuoni hapo hali iliyotafsiriwa kuwa ni mgomo kwani kwa siku nzima ya leo hawajaingi madarasani.

Itakumbukwa kuwa chuo hicho kimekuwa na matatizo mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu wenye sifa,kuwa na kozi zisizotambuliwa na NACTE/TCU, upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia,upungufu wa vyumba vya kusomea na kadhalika,

Jioni ya leo wanafunzi wa chuo hicho kwa kushirikiana na umoja wa wanataaluma wa chuo hicho wameungana na kukubaliana kutoingia madarasani mpaka hapo madai yao ya msingi yatakapotatuliwa.Itakumbukwa kuwa jumamosi ijayo trh 6/12/2014 ilitarajiwa kufanyika mahafali ya 5 tangu kuanzishwa kwake.
 
Someni msiwaige UKAWA.... wenzenu wanasiasa wanalipwa kwa kugoma....
 
kimenuka nako, kila sehemu ya nchi hii ni vurugu mechi. Ngoja tuendelee kusubiri kauli ya ikulu kwanza kuhusu wale watajwa wa ccm waliokwapua fedha za uchaguzi kutoka eskrol
 
Turudishieni mazengo yetu, mlidhani chuo ni siasa...napata mashaka sana hiyo taaluma kutoka hapo..
 
Huu mtindo wa kubadiri Primary kuwa Sekondari na Sekondari kuwa University, SIUPENDI KAMS NINI. Hii ni dalili ya jamii iliyoshindwa kujiendeleza na kupata maendeleo. Ni jamii iliyokata tamaa kujenga taasisi mpya. Taifa letu limefika pabaya hata tezi dume hatuwezi kutibu.
 
Tatizo Kanisa Anglican wanamuogopa sana Donald Mtetemela amekifanya Chuo kama taasisi yake binafsi, ameajiri watoto wake kila Campus ya Chuo wanna kibri balaa, ukiwagusa tu huna Chuo
 
Duuuuuh!!! Alafu nakumbuka kulikuwa na mwanafunzi wa hapo St John alikuja field shuleni kwetu akawa anasifia hicho chuo kumbe ni bure kabisa. ..
 
Tatizo Kanisa Anglican wanamuogopa sana Donald Mtetemela amekifanya Chuo kama taasisi yake binafsi, ameajiri watoto wake kila Campus ya Chuo wanna kibri balaa, ukiwagusa tu huna Chuo

Huyu ndie yule mzee mwenye kialaza alikuwa kimbelembele kutetea ujinga BMK?
 
Na haya ndo matatizo ya kugeuza shule (Mazengo sekondari) kuwa chuo kikuu. Wajipange upya!!!
 
Vijana komaen na mgomo hamuwez rundikiwa TA wenye GPA ZA 2 wakawapiga lekcha wakat mnalipa ada kubwa,hiyo c haki.
 
Sipend vyuo ambavyo mwenye digrii ya kwanza anamfundisha mtu anayesomea digrii ya kwanza!utumbo mtupu!hv TCU mko wap?
 
Vyuo vikuu ving vya private ni utumbo mtupu,wapo after money hakuna cha maana wanachowachia kichwan wafnz wao.
 
Back
Top Bottom