Kwani kutaka kuvunja muungano ni kosa ?
Kwa nini mnatulazimishia Muungano?
Wewe Mtanganyika unafaidika nini na kakisiwa landless kale ka Zanzibar ??????
Nadhani umesoma lakini hukuelewa
Rudi katika bandiko langu, hakuna mahali nimesema kuvunja muungano ni kosa
Nilichosema ni kuwa '' hoja ya akina OMO ya mkataba ililenga kuvunja muungano'' Kwa maneno mengine nachambua mantiki ya hoja yao . Nilienda mbali na kuonyesha kuwa hivi muungano wa mkataba ukoje!
Nikasema kulitokea tofauti kati ya Unguja ya akina Pandu na Pemba ya akina Maalim na OMO
Huu ni mtazamo unaweza kuukubali au kuukataa lakini huna uwezo wa kuzuia maoni ya watu
Ukisoma kitu jaribu kuelewa kwanza kabla ya kukimbilia katika key board.
Pili, hakuna mtu anawalazimisha muungano , mnaweza kuondoka leo mkawaambia Wazanzibar wajiuzulu nafasi zao serikali ya JMT kuanzia juu, mkakataza Wabunge wasije Dodoma, mkapitisha sheria BLW kwamba hamtaki muungano!
Tatu, Tanganyika haififidiki na chochote kwa uwepo wa Zanzibar ! zigo tu