Kwa heshima kubwa, naomba nikuulize. Mkuu, umefanya upembuzi yakinifu wa kutosha na kugundua kuwa Katiba Mpya ndiyo itatuwafanya watanzania tuboreshe zaidi maisha yetu kiuchumi, kijamii huku Tanzania ikizidi kuimarika kimataifa katika nyanja zote...?
Ni hivi sasa Kenya wanataka kukarabati katiba yao ambayo ilikuwa mpya kuliko ya kwetu miaka michache illyopita! Mkuu unataka kuniambia Kenya walipata katiba 'mtumba'? Jibu nadhani ni hapana. Pia nafikiri kama sijakosea kuna uwezekano Kenya walitaka katiba mpya baada ya kushindwa kufanya upembuzi makini kujua hasa ni nini wanataka ili waboresha maisha yao wao kama wakenya na Kenya yao kwa ujumla.
Binafsi,nadhani Katiba mpya si- muarobani wa kutatua changamoto tulizonazo. Kwa katiba hii mnayoinoa 'kuu kuu' tukiwa makini kabisa na tukiendelea kujielewa kama nyakati hizi, hii katiba ya sasa inatosha kutuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea na tutakayojiwekea!
Hata hivyo, Mkuu nakurudisha kwenye aya ya kwanza ya post yangu hii. Mkuu ebu tufafanulie kinaga ubaga ni kwa namna gani Katiba mpya itaboresha maisha ya Watanzania wote na itatuhakikishia Muungano wetu kama nchi unaendelea kudumu.
Karibu.
Tatizo kubwa la nchi za Dunia ya Tatu Ni Gorvanance' ie uendeshaji na management ya Uchumi,Siasa,na masuala yote ya huduma za Jamii.Hapa ndio tukipokwama!
Katiba Bora Ni Muarabaini ya yote!
Nchi yetu Ni masikini na inaRasilimsli za kutosha!
Tatizo Ni namba Bora ya kutumia Rasilimali zilizopo kuboresha maisha.
Mfano ...katiba ya Sasa inamla Madaraka makubwa Sana Rais,hiki hakufai...Ni lazima kuwe na check and balance..!
Fikiria ujenzi wa Daraja la Baharini la Surrender pale Koko Beach !
Huu Ni uamuzi usio na busara Wala tija...fedha hizo zingeweza kuchimba visima lukuki vya maji,au kujenga mabwawa ya maji kuvuna maji ya mvua na kuendekeza kikimo Cha mbogamboga,ambazo zinahitajika Sana nchini na nje ya nchi!
Hili lingewezekana kupitia mijadalayenye tija!
Kuna watu wanaushi kando ya mito na maziwa lakini hawana maji salama ya kunywa!
Daraja la Koko Beach linawahusu !?
Leo hii tuna Bunge lisilo na meno! haliwezi kujadili miswaaada kwa maslahi ya walipa Kodi!
Hii yote Ni matunda ya Katiba mbovu!
Hii Ni mifano michache tu !
Mojawapo ya urithi mbovu kabisa wa Nyerere Ni huu!
Na yeye alikiri!
Lissu lete Katiba Mpya ,tuanzie alipoishia Warioba!