Saidama
JF-Expert Member
- Jun 10, 2022
- 855
- 1,593
Hii ni kwa mujibu wa website ya masuala ya sayansi yenye makao yake nchi Uingeleza ya IFLSCIENCE ambao wameripoti kua 'Ziwa kubwa barani Afrika linageuka kua la kijani'
Hii inatokana na hali ya kiasili inayotambulika kwa kitalamu kama 'eutrofication', ambayo ni hali ya ziwa/bahari/mto kujaa virutubisho vingi kutoka nchi kavu vinavyoingia ziwani kwa kupitia maji ya mvua yanayoingia ziwani.
Kujaa kwa virutubisho hivyo ziwani pamoja na hali ya joto kua juu husababisha kuzaliana kwa magugu maji na pia kusababisha uvundo wenye rangi ya kijani majini (unaweza kua wa rangi nyingine pia). Hali hii hutokea, lakini hutokea mara chache na kwa sehemu chache za ghuba ambazo maji hayatembea sana.
Lakini shughuli za binadamu zinaweza kusababisha hali hii kutokea kwa wingi tofauti na uhalisia wake. Na kwa kesi kama ya Ziwa Victoria, hali hii inadaiwa kutokea kwa wingi kutokana na shughuli za kibinadamu ambazo zimefanywa kwa muda mrefu kando ya ziwa.
Shughuli hizo zinaweza kusababisha vitu kama kuingia majini kwa mbolea ya mashambani kunakosababishwa na mmomonyoko wa ardhi kutokana na mvua kubwa, kuingia kwa wingi kwa maji taka ziwani na hata kuingia kwa wingi kwa maji taka ya viwandani ziwani. Hizi zote ni shughuli ambazo zinaweza kufanya hali hii kutokea kwa wingi.
Kuongezeka kwa magugu na uvundo huu wa kijani juu ya maji ya ziwa huzuia hewa ya oxygen kuingia chini ya maji na hivyo kusababisha samaki na viumbe wengine wa majini kukosa hewa safi na hivyo kufa au kupunguza uzalianaji na kupelekea upungufu wa samaki ziwani, kama wanavyolalamika wavuvi wa ziwa hili hivi sasa.
View: https://m.youtube.com/watch?v=4AmUrW-sWX8&pp=ygUgVXB1bmd1ZnUgd2Egc2FtYWtpIHppd2EgdmljdG9yaWE%3D
Mbaya katika habari hii ni kua, mtandao wa IFLSCIENCE unaripoti pia watafiti kutoka chuo kikuu cha Michigan and Bowling Green State cha nchini Marekani wamefanya tafiti katika ghuba ya Winam nchini Kenya na kugundua uwepo wa bakteria aina ya 'Microcystis' katika uvundo huu ambae anazalisha kiasi kikubwa cha sumu aina ya 'Microcystin'. Hii ni sumu ambayo inaweza kuathiri maini kwa wanyama na binadamu na hata kupelekea kifo hasa kwa watu wenye kinga ya mwili iliyo chini.
Sasa ni kua sio kila uvundo una bakteria hawa wenye sumu na watafiti hawa wanafanya utafiti zaidi ili kugundua ni uvundo wa aina gani unaweza kua na bakteria huyu ili kutoa elimu zaidi kwa jamii pindi wanapoona hali ya aina hiyo kwenye maji waweze kukaa mbali ili kuepuka madhara. Na hapa ndipo litakuja jukumu la serikali kufatilia kwa karibu jambo hili kwa kushirikiana na watafiti hawa na kisha kutoa elimu kwa jamii.
Haya ni machache kati ya mengi yanayohatarisha usalama wa ziwa letu ambalo inakadiriwa linategemewa na watu zaidi ya milioni 47 kwa ajili ya chakula, maji safi na hata ajila kote kati ya nchi tatu za Afrika Mashariki.
Kama mwananchi, ni jukumu lako binafsi pia kuhakikisha ziwa linakua safi kwa kuhakikisha shughuli zako hazi athiri afya ya ziwa letu. Epuka kutupa taka yoyote ziwani kwani taka unayoitupa leo ziwani ina nafasi kubwa sana ya kuhatarisha zaidi afya ya ziwa letu kwa siku za badae.
Taarifa zaidi;
www.iflscience.com

Scientists Sounding Alarm As World’s Largest Tropical Lake Turns Green
Lake Victoria is under threat from microscopic life.