Hali tete Marekani inaomba msaada wa washirika wake na dunia dhidi ya China katika vita vya uchumi

Hali tete Marekani inaomba msaada wa washirika wake na dunia dhidi ya China katika vita vya uchumi

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Huenda umelisikia sana jina Scott Bessent tangu Trump aingie madarakani hasa wakati huu wa vita vya kiuchumi kati ya Marekani na China.

Huyu ni U.S Treasury Secretary na ndiye mwakilishi anayeongoza jopo la wajumbe wa Marekani katika mikutano ya China na Marekani ya kusuluhisha mzozo wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Hivi karibuni baada ya China kuzuia uuzaji rare earths kwa Marekani imeonekana nyundo hii imeielemea sana Marekani kusimama peke yake hivi kwamba Bessent amefikia hatua ya kusema haya
:​

"Tumesukumwa nyuma kwa nguvu na China ambayo imedhibiti uuzaji nje wa rare earths."

"Hii ni hatua ya uchochezi. Tayari tumewasiliana na washirika na tunakutana nao wiki hii."

"Hii ni China Vs Dunia, hatutaruhusu vikwazo vya usafirishaji wa China viendelee."

"Tunatarajia kuungwa mkono na India na wengine. Tunaamini China iko tayari kujadiliana kuhusu hili.
"

—Scott Bessent (U.S Secretary of Treasury)​

Taifa la Marekani linaendeshwa na viongozi vichaa wakiongozwa na raisi wao Trump.

Mapema April mwaka huu Raisi wa Marekani aliyapiga ushuru mataifa yote duniani leo Marekani inataka mataifa hayohayo yawaunge mkono dhidi ya China.

Bessent ana matumani kuwa Marekani itaungwa mkono na India, taifa ambalo mwezi Septemba mwaka huu waliliwekea ushuru wa 50% kwa sababu ya kununua mafuta kutoka Russia.

Na kama haitoshi Marekani ndiyo iliyoanzisha vita ya ushuru dhidi China na dunia.

Hii ni U.S Vs Dunia.
​
 
Yani sijaelewa....wanalazimishwa kuuziwa hayo madini na China?
 
Mfa maji haachi kutapatapa
Ni sahihi Marekani ni kama mfa maji nimeona Trump ameishiwa mbinu za kupigana kiuchumi na China sasa hivi amekimbilia kwenye biashara ya mafuta ya kula kutoka China 😅😅😅​

20251015_191726.jpg
 
Yani sijaelewa....wanalazimishwa kuuziwa hayo madini na China?
Marekani ni importer mkubwa wa rare earths kutoka China na si Marekani mataifa yote duniani

Wanayahitaji sana kwa ajili ya kutengeneza silaha za maangamizi na chips na bidhaa zingine za high tech

China ndio taifa pekee ambalo lina teknolojia ya ku-refine aina zote za rare earths ina control zaidi ya 80% ya refined rare earths duniani

Na China imezuia uuzwaji wa rare earths kwa matumizi ya kutengeneza silaha ila kulinda amani duniani

Upande wa Marekani miongoni mwa biashara zake kubwa ni silaha na high end semiconductors

Hivyo defense contractors na watengeneza chips wa Marekani kwa sasa wanapitia kipindi kigumu kutokana na Mchina kupiga pini refined rare earths na dual goods zake
​

20250913_084750.jpg
 
Mi siku zote huwa kuwa nasemaga Trump ni raisi taahira kuwahi kutokea Marekani kuna watu hawanielewagi.
Umesema vyema, hata Wamarekani hawajui Trump anawapeleka wapi wanapitia kipindi kigumu

Juzi masoko ya hisa ya Marekani, bitcoin mining na cryptocurrency zilianguka vibaya sana baada ya China ku-retaliate

Trillion of dollars zilipotea, na bado Wamarekani watapigwa tena na inflation kwa bidhaa zinazoingia kutoka China baada ya MAGA kuziongezea ushuru
 
Miezi mitatu nyuma nilikwenda Ithaca,NY kwenye sehemu inayo husika na kutengeneza na silaha za marekani company inayoitwa Lockheed Martin na nyengine ipo Stanford,CT inaitwa Sikorsky.

Niliongea na CEO wao kwa maelezo yao nilibaki mdomo wazi tu jamaa kiufudi wapo hoi. Miezi miwili ijayo nitakwenda kwenye sehemu inayo tengeneza silaha ipo Indiana sijui watasemaje nao.
 
Trump anawapeleka raia KUSIKOJULIKANA?
Rednecks na ubaguzi wao hawajuwi!
Mwisho wa siku Ili kuiokoa nchi yao, Trump/Tramp itabidi abadilishe sera zake ZOTE!
 
Huenda umelisikia sana jina Scott Bessent tangu Trump aingie madarakani hasa wakati huu wa vita vya kiuchumi kati ya Marekani na China.

Huyu ni U.S Treasury Secretary na ndiye mwakilishi anayeongoza jopo la wajumbe wa Marekani katika mikutano ya China na Marekani ya kusuluhisha mzozo wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Hivi karibuni baada ya China kuzuia uuzaji rare earths kwa Marekani imeonekana nyundo hii imeielemea sana Marekani kusimama peke yake hivi kwamba Bessent amefikia hatua ya kusema haya
:​

"Tumesukumwa nyuma kwa nguvu na China ambayo imedhibiti uuzaji nje wa rare earths."

"Hii ni hatua ya uchochezi. Tayari tumewasiliana na washirika na tunakutana nao wiki hii."

"Hii ni China Vs Dunia, hatutaruhusu vikwazo vya usafirishaji wa China viendelee."

"Tunatarajia kuungwa mkono na India na wengine. Tunaamini China iko tayari kujadiliana kuhusu hili.
"

—Scott Bessent (U.S Secretary of Treasury)​

Taifa la Marekani linaendeshwa na viongozi vichaa wakiongozwa na raisi wao Trump.

Mapema April mwaka huu Raisi wa Marekani aliyapiga ushuru mataifa yote duniani leo Marekani inataka mataifa hayohayo yawaunge mkono dhidi ya China.

Bessent ana matumani kuwa Marekani itaungwa mkono na India, taifa ambalo mwezi Septemba mwaka huu waliliwekea ushuru wa 50% kwa sababu ya kununua mafuta kutoka Russia.

Na kama haitoshi Marekani ndiyo iliyoanzisha vita ya ushuru dhidi China na dunia.

Hii ni U.S Vs Dunia.
​

Propaganda za kijinga😂😂
 
Back
Top Bottom