Hali tete Ukraine waanza kutumia vikongwe na watoto. Wagner Group yamtaka Zelensky atangaze kuipoteza Bakhmut maana hali ni tete

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Mkuu wa kampuni ya masuala ya kijeshi nchini Urusi, Wagner Group, amesema wapiganaji wake wameuzunguka mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine, ambao Urusi imekuwa ikijaribu kuutwaa kwa miezi kadhaa sasa.

Kufikia asubuhi ya Ijumaa (Machi 3), Yevgeny Prigozhin alisema sehemu pekee ambayo haikuwa imechukuliwa na wapiganaji wa kundi lake "ni barabara moja kuelekea mji huo" wenye utajiri wa migodi ya chumvi na viwanda vya mvinyo.

Mkuu huyo wa Wagner Group alimtolea wito Rais Volodymyr Zelensky kuwaamuru wanajeshi wake kuondoka kwenye mji huo.

"Ikiwa pale mwanzo tulikuwa tunapigana na jeshi lenye utaalamu, sasa tunazidi kukutana na wazee na watoto.

Wanapigana lakini maisha yao mjini Bakhmout ni mafupi, labda siku moja ama mbili, wape fursa ya kuondoka kwenye mji huo." Alisema Prigozhin, ambaye ana mahusiano makubwa na Ikulu ya Kremlin, kupitia ujumbe kwa njia ya vidio.

Kwenye mkanda huo wa vidio aliwaonesha vijana wawili na mzee mmoja wakimuomba Zelensky awaruhusu kuondoka.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, alisema nchi yake haitayaruhusu tena mataifa ya Magharibi kuripuwa mabomba yake ya gesi na wala kamwe haitayategemea mataifa hayo kuwa washirika wake kwenye masuala ya nishati.

Moscow inaamini kwamba mataifa ya Magharibi yanahusika na mripuko ulioharibu mabomba ya mafuta ya Nord Stream mnamo mwezi Septemba na inataka uchunguzi huru wa kimataifa ufanyike.

64473868_803.jpg
 
View attachment 2536148
Putin must failed. Is the matter of time. Western leader they need head of W so keep silence
 
Back
Top Bottom