Hali tuliyonayo hivi sasa itazidi kuwa mbaya zaidi, Ila..

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
Ukimuuliza Mtanzania yeyote kuhusu hali ya maisha tuliyonayo nchini inavyozidi kuwa mbaya... Atapeleka lawama moja kwa moja kwa SERIKALI.

Wanasiasa watalalamikia katiba na CCM.

Mzazi akipokea taarifa mbaya ya matokeo ya mwanae shuleni... Lawama zinaenda kwa MWALIMU...

Mwalimu anailaumu serikali.

Hakuna anayekubali kujitathmini na kuangalia upande wake kama tatizo lipo kwake au la, wote tunawatupia lawama wengine.

KWAKWELI HALI NGUMU YA MAISHA TULIYONAYO HAITOKUJA KUBADILIKA NA KUWA NZURI HATA AJE KIONGOZI GANI... MTENGENEZE KATIBA YA AINA GANI.

Kwa aina hii ya watu ambao tunadhulumiana wenyewe kwa wenyewe... Tunaibiana wenyewe kwa wenyewe... Yaani kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Katika jamii yetu hadi mtu wa chini kama muuza mkaa... Kile kipimio cha mkaa anawekea kibati chini ili adhulumu mkaa.

Muuza mafuta anakata kipimio cha mafuta ili mteja asipate haki yake.

Muuza nafaka anaichezea mizani ili apunje kipimo.

Muuza mchele kule kahama shinyanga wanamwagia mafuta mchele ili uvutie ung'ae.

Mteja nae anatafuta mtu wake nae ampige.

Yaani ili mradi kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Jamii imezidi UOVU AMBAO HAUHIMILIKI... Mfano;-

1. USHIRIKINA sasa hivi ni sehemu ya mtu kujitetea anaabudu na kuamini atakavyo... Yaani SHIRK imekuwa waziwazi inapewa majina tofauti tofauti mara UTAMADUNI mila.

Ushirikina ilibidi upigwe vita... Ila sasa katika jamii yetu ya kitanzania unasifiwa na kutetewa na kupakwa rangi tofauti tofauti kuuhalalisha.

Wakati kila mtu anajua YUPO MMOJA TU MUUMBA MUNGU WA KUABUDIWA.

2. Eti jamii imeiga wazungu vituo vya kulea wazee.

Ina maana hao wazee hawana watoto hao wa kuwalea wazazi wao? Hawana ndugu kusitiriana ndugu?

Tanzania tumekuwa na jamii za kibinafsi na roho mbaya... Nani atamuonea mwenzake huruma.. Hata mzazi wake.

3. Mayatima. Watu hawataki kulea yatima... Hivi unakuta kituo cha kulelea yatima kina watoto 150, hivi ina maana hawa watoto wote hawa hawana KAKA, MADADA, WAJOMBA, BABA WADOGO, MASHANGAZI?

4. UZINIFU sasa hivi ni jambo la kawaida na la kujivunia mtu kufanya zinaa... Angalieni uzi ule wa kimaskhara.

5. Yaani jamii imeoza yenyewe kama jamii... Vile vile na viongozi tunawapata kutoka kwenye jamij hiyo hiyo... UNATEGEMEA TOFAUTI YA AINA GANI?

6. KAMARI sasa hivi ni jambo la kawaida.

7. USHOGA hivi sasa unatetewa kabisa.

8. Kodi... Huu ni WIZI, UJAMBAZI NA UNYANG'ANYI uliohalalishwa kwa kile walichokiita sheria... Tena waliojiandikia wao ili wawanyang'anye watu mali zao kihalali.

Huku chini kila mtu akipata nafasi upenyo anamwibia mwenzake.

9. MAUAJI... sasa hivi wanayahalalisha kwa jina la WASIOJULIKANA au WANANCHI WENYE HASIRA KALI.

10. ULEVI... Kwenye jamii yetu halina haja ya kulielezea sana linafahamika.

NA HAYO NI SEHEMU TU YA MAOVU AMBAYO JAMII YETU IMEYABEBA. NA HAYO TUNAMUUDHI MUUMBA WETU... JE UNATEGEMEA ATATUSAIDIA KWENYE MAMBO YETU MAGUMU?

HAKI NAAPA KWA MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI NA KILA KILICHOMO... MAISHA HAYA HAYABADILIKI KUWA MAZURI TENA... YATAZIDI KUWA MABAYA MAISHA HAYA KILA SIKU AFADHALI YA JANA.

TUTAKUFA TUTAYAACHA MAISHA NI MAGUMU ZAIDI.

SULUHISHO:

SISI MMOJA MMOJA KILA MTU ABADILIKE APUNGUZE MAASI YAKE AU AYAACHE KABISA... TUBADILIKE... TUACHE USHIRIKINA. TUACHE KUDHULUMIANA... TUSIMUASI MUUMBA WETU.

TUSIJIFANYE WAJUAJI... TUNAIJUA DUNIA KULIKO MUUMBA MWENYEWE... HATUNA MAHALI PA KWENDA... TURUDI CHINI TUBADILIKE.
 
katoe mawaidha msikitini au kahubiri kanisani........................wacha watu watumie mbinu mbalimbali ili wapate maendeleo,mtu akiwa na hali ngumu mnamcheka akifight ili ajikomboe mnajifanya kumpa mawaidha au mahubiri
 
Kwa asili, wanadamu ni wabinafsi. Ulioyaandika yapo kinyume na asili na hayawezekani.
 
Hivi hamjiulizi viongozi wanazidi kuzorota ubora... Toka kwa nyerere mpaka leo tunaye samia...
 
Nyerere alikuwa bora kuliko mwinyi...

Mwinyi alikuwa bora kuliko mkapa...

Mkapa alikuwa bora kuliko kikwete...

Kikwete alikuwa bora kuliko Magufuli...

(USHAHIDI: ANGALIA KILA ANAPOKUWEPO RAIS FULANI MADARAKANI... WATU HUMKUMBUKA NA KUMTAJA ALIYETANGULIA...)
 
katoe mawaidha msikitini au kahubiri kanisani........................wacha watu watumie mbinu mbalimbali ili wapate maendeleo,mtu akiwa na hali ngumu mnamcheka akifight ili ajikomboe mnajifanya kumpa mawaidha au mahubiri
Sasa hayo maendeleo... Reg. Mengi yanamsaidia nini sasa hivi?

Haya tafuta maendeleo tuone yatakufikisha wapi?
 
Ukimuuliza Mtanzania yeyote kuhusu hali ya maisha tuliyonayo nchini inavyozidi kuwa mbaya... Atapeleka lawama moja kwa moja kwa SERIKALI.

Wanasiasa watalalamikia katiba na CCM.

Mzazi akipokea taarifa mbaya ya matokeo ya mwanae shuleni... Lawama zinaenda kwa MWALIMU...

Mwalimu anailaumu serikali.

Hakuna anayekubali kujitathmini na kuangalia upande wake kama tatizo lipo kwake au la, wote tunawatupia lawama wengine.

KWAKWELI HALI NGUMU YA MAISHA TULIYONAYO HAITOKUJA KUBADILIKA NA KUWA NZURI HATA AJE KIONGOZI GANI... MTENGENEZE KATIBA YA AINA GANI.

Kwa aina hii ya watu ambao tunadhulumiana wenyewe kwa wenyewe... Tunaibiana wenyewe kwa wenyewe... Yaani kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Katika jamii yetu hadi mtu wa chini kama muuza mkaa... Kile kipimio cha mkaa anawekea kibati chini ili adhulumu mkaa.

Muuza mafuta anakata kipimio cha mafuta ili mteja asipate haki yake.

Muuza nafaka anaichezea mizani ili apunje kipimo.

Muuza mchele kule kahama shinyanga wanamwagia mafuta mchele ili uvutie ung'ae.

Mteja nae anatafuta mtu wake nae ampige.

Yaani ili mradi kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Jamii imezidi UOVU AMBAO HAUHIMILIKI... Mfano;-

1. USHIRIKINA sasa hivi ni sehemu ya mtu kujitetea anaabudu na kuamini atakavyo... Yaani SHIRK imekuwa waziwazi inapewa majina tofauti tofauti mara UTAMADUNI mila.

Ushirikina ilibidi upigwe vita... Ila sasa katika jamii yetu ya kitanzania unasifiwa na kutetewa na kupakwa rangi tofauti tofauti kuuhalalisha.

Wakati kila mtu anajua YUPO MMOJA TU MUUMBA MUNGU WA KUABUDIWA.

2. Eti jamii imeiga wazungu vituo vya kulea wazee.

Ina maana hao wazee hawana watoto hao wa kuwalea wazazi wao? Hawana ndugu kusitiriana ndugu?

Tanzania tumekuwa na jamii za kibinafsi na roho mbaya... Nani atamuonea mwenzake huruma.. Hata mzazi wake.

3. Mayatima. Watu hawataki kulea yatima... Hivi unakuta kituo cha kulelea yatima kina watoto 150, hivi ina maana hawa watoto wote hawa hawana KAKA, MADADA, WAJOMBA, BABA WADOGO, MASHANGAZI?

4. UZINIFU sasa hivi ni jambo la kawaida na la kujivunia mtu kufanya zinaa... Angalieni uzi ule wa kimaskhara.

5. Yaani jamii imeoza yenyewe kama jamii... Vile vile na viongozi tunawapata kutoka kwenye jamij hiyo hiyo... UNATEGEMEA TOFAUTI YA AINA GANI?

6. KAMARI sasa hivi ni jambo la kawaida.

7. USHOGA hivi sasa unatetewa kabisa.

8. Kodi... Huu ni WIZI, UJAMBAZI NA UNYANG'ANYI uliohalalishwa kwa kile walichokiita sheria... Tena waliojiandikia wao ili wawanyang'anye watu mali zao kihalali.

Huku chini kila mtu akipata nafasi upenyo anamwibia mwenzake.

9. MAUAJI... sasa hivi wanayahalalisha kwa jina la WASIOJULIKANA au WANANCHI WENYE HASIRA KALI.

10. ULEVI... Kwenye jamii yetu halina haja ya kulielezea sana linafahamika.

NA HAYO NI SEHEMU TU YA MAOVU AMBAYO JAMII YETU IMEYABEBA. NA HAYO TUNAMUUDHI MUUMBA WETU... JE UNATEGEMEA ATATUSAIDIA KWENYE MAMBO YETU MAGUMU?

HAKI NAAPA KWA MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI NA KILA KILICHOMO... MAISHA HAYA HAYABADILIKI KUWA MAZURI TENA... YATAZIDI KUWA MABAYA MAISHA HAYA KILA SIKU AFADHALI YA JANA.

TUTAKUFA TUTAYAACHA MAISHA NI MAGUMU ZAIDI.

SULUHISHO:

SISI MMOJA MMOJA KILA MTU ABADILIKE APUNGUZE MAASI YAKE AU AYAACHE KABISA... TUBADILIKE... TUACHE USHIRIKINA. TUACHE KUDHULUMIANA... TUSIMUASI MUUMBA WETU.

TUSIJIFANYE WAJUAJI... TUNAIJUA DUNIA KULIKO MUUMBA MWENYEWE... HATUNA MAHALI PA KWENDA... TURUDI CHINI TUBADILIKE.
Jibu la haya yote ni kumwogopa mwenyezi Mungu
Allah akuhifadhi
 
Makala nzuri tatizo hatutaisoma, yajayo yanafurahisha
 
katoe mawaidha msikitini au kahubiri kanisani........................wacha watu watumie mbinu mbalimbali ili wapate maendeleo,mtu akiwa na hali ngumu mnamcheka akifight ili ajikomboe mnajifanya kumpa mawaidha au mahubiri
Ana fight kwa dhulma,halafu siku ukiumwa UTI ukienda hospital ukatumia muda mrefu kumuona dokta utakuja hapa jukwaani kushupaza mishipa ya shingo kuwa madaktari wanapokea rushwa
 
Oneni hawa wanaoitwa viongozi wa dini... Yaani wanaishi utasema hawaishi kwenye jamii iliyojaa maovu kama hii...wakifika mbele za viongozi wanajiwazia wao na posho tu...
Screenshot_20220531-161923.png
 
Back
Top Bottom