KERO Hali ya fukwe za Bahari Mbezi Beach (Jangwani) haziridhishi; Tutaenda na hali hii AFCON?

KERO Hali ya fukwe za Bahari Mbezi Beach (Jangwani) haziridhishi; Tutaenda na hali hii AFCON?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716

photo_2026-08-18_09-08-50.jpg
Kwa takribani siku tatu nilikuwa kikazi kwenye hoteli moja iliyopo Mbezi Beach. Jumapili, Agosti 16, 2026, kabla ya kumaliza siku zangu za kuwepo hapo, nilijipa muda wa kutembelea fukwe za bahari za Mbezi Beach, upande wa chini wa mitaa ya Jangwani. Nilikuwa sijafika maeneo hayo kwa takribani miaka mitano, tangu nilipohama Dar es Salaam.

Kwa kweli, nilichokiona kilinisikitisha. Mandhari ya maeneo hayo muhimu hayaridhishi. Taka zimezagaa kila sehemu, maeneo ni machafu, huku viroba na uchafu unaosukumwa na bahari vikiwa vimezagaa katika maeneo hayo jambo ambalo linaonesha kwamba hali hiyo imekuwepo kwa muda mrefu.

Ilibidi niongee na baadhi ya vijana wenyeji wa maeneo hayo. Walisema ni nadra sana kuona usafi ukifanyika katika maeneo hayo. Inavyoonekana, hali hiyo imezoeleka, jambo ambalo linaweka watu hatarini kupata magonjwa na majeraha kutokana na mazingira kutokuwa salama, hasa kwa wanaotembea kwa miguu au kuogelea katika ukingo wa bahari.

Kama tunavyofahamu, maeneo ya fukwe ni sehemu pendwa na kivutio kwa wageni, hasa ikizingatiwa hali ya hewa ya Dar es Salaam. Wageni wengi hutamani kutembelea maeneo yenye utulivu na mandhari nzuri. Kutokana na hali hiyo, nilishtuka sana kuona hali ilivyo, hasa wakati Tanzania inajiandaa kuwa sehemu ya waandaaji wa Africon. Swali lililobaki kwangu nikijiuliza: Je, suala la mandhari na usafi wa fukwe zetu linapewa umuhimu unaostahili?

Tukumbuke kwamba eneo hilo licha ya kuwa ni eneo la wazi limezungukwa na hoteli na maeneo ya starehe ambayo, sina shaka, yanaweza kuwa sehemu za kupokea wageni endapo mambo yataenda kama inavyotarajiwa. Kwa nini hakuna jitihada, hata kupitia ushirikishwaji wa wadau, za kupendezesha mandhari ya maeneo hayo na kuyafanya yawe katika hali ya kuvutia huku yakibakia kuwa maeneo ya wazi?
photo_2026-08-18_09-08-47.jpg
photo_2026-08-24_09-13-06.jpg
Licha ya mkakati wa AFCON, tunapaswa pia kuwakumbuka watoto wetu na wananchi wanaotembea katika maeneo hayo mara kwa mara. Kwa nini mamlaka, hasa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hazichukui hatua za wazi kuhakikisha mandhari na usafi wa maeneo hayo vinaboreshwa? Je, tunasubiri hadi nini kitokee ndipo hatua zichukuliwe?

Hili si suala la AFCON pekee. Ni suala la usalama, afya, mazingira na hadhi ya jiji letu. Ni muhimu mamlaka husika kwa kushirikiana na wadau wengine kuchukua hatua mapema ili maeneo haya ya wazi yawe salama, safi na yenye kuvutia kwa wananchi na wageni wanaoyatembelea.

Pia soma
~
Rais Samia: Dar es Salaam ni kuchafu, ni aibu
~ DC Mpogolo: Atakaye tupa taka Ganda la Ndizi na Pipi faini Milioni 1, Dar
 
Serikali ya CCM kila kukicha wapo bize na Lissu, hayo mambo watayafanya muda gani?
 
sijaelewa, kwa hiyo wasafishe kwa sababu ya kuwafurahisha afcon? au kwa sababu ya kuhudumia wakazi wa mbezi beach? ...
 
Back
Top Bottom