Nimeishi Dar maisha yangu yote (takriban miaka 32), nimekuja dom nina miaka takribani mi3 tu kwa sasa, changamoto ya ngozi kuwa mbaya ilinitesa sana, hasa kwa yake mazoea ya Dar kutopenda kupaka mafuta mara kwa mara , ama kutumia lotion ya kuondoa unyevu usoni (sbb ya joto), niliishi Arusha kipindi fulani pia ilinitesa sana vilevile ka dom
Ila kwa sasa naweza kusema napapenda zaidi dom kuliko Dar...atlst niseme nimekubaliana na mazingira
Kupambana na changamoto ya ngozi kuwa kavu dodoma ni kutotumia sabuni usoni (ama paka mara chache sana), pia tumia lotion za kumoisturize ngozi Kama vile NIVEA repair & care kila unapopaka maji usoni hata ka haupo nyumbani, kutooga maji ya moto sana hasa kwa muda mrefu, ukipata fursa ya kuwa na humidifier ndani pia itasaidia
Mbali na hivyo ninaweza kusema napenda hali ya hewa ya dom kuliko joto kali la Dar na vurugu zake
Dar ipo na itazidi kung'ara, ila dom pia itaenda kuwa mji mzuri sana wa kuishi hapo baadaye
Karibuni Kisasa