Hii dunia ya watu wastaarabu. Ukitaka kuwarudisha nyuma kwenye ushenzi, wengine watapinga, hata kama raia wako watanyamaza kwa kuzidiwa nguvu au kutojua.
Haya ni matokeo ya kawaida kwa siasa za kihuni, ushenzi, kiburi na kutesa raia, eti kwa kuwaletea maendeleo. Mbona Botswana, Senegal, Mauritius zinaendelea haraka sana bila ya kutukana watu, kuuwa watu wala makeke?
Nimejifunza mtu hawezi kufeki kusoma. Mtu kama hakusoma vizuri, hata akiwa na tittle ya Udokta, Uprofesa....ataonekana tu katika matendo yake. Ukitazama hizo nchi nilizozitaja zote zinashirikiana katika kitu kimoja muhimu: viongozi wake wamesoma kikweli, na si bora elimu. Na hakuna kati yao anayeitwa dokta au profesa!
Hebu tazama matamshi haya kama kweli hayawezi kuleta madhara kwa nchi, yanasemwa na mtu mwenye weledi na kuliepushia madhara taifa lake:
1- Tanzania hakuna Covid-19 (lakini dunia nzima ipo).
2- Jizalieni tu Tanzania tajiri!
3- Sisomeshi wasichana wenye watoto!
Kwa mtu ajuaye dunia na mahusiano ya Kimataifa, statement kama hizo (na nyingine nyingi) ni lazima zilete madhara kwa nchi. Haya ndiyo matokeo yake. Jamii ya Kimataifa huenda ikawa slow ku react, lakini kwa uhakika itajibu, maana baadhi ya mambo haya yanachukuliwa kuwa yanaweza kuja kuhatarisha usalama wa dunia yakiachiwa. Tayari Tanzania imeishaanza kuzalisha wakimbizi!
Mbaya sana kiongozi kufanya kama nchi yote ni milki yake pekee. Wakati matatizo yanapotokea sisi wote tunaathirika!
Huyu mzee ashauriwe bila woga kabla mambo hayajaharibika. Tanzania ni nchi ndogo sana katika dunia, wala haina athari yeyote, si ya kiuchumi wala kisiasa (hivi sasa)> Wakitaka kuamua mara moja waiwekee ngumu...........hatutoki. Hakuna nchi yeyote dunia ya leo inayoweza kujikimu yenyewe pekee. Hii haina maana kulamba miguu. Kuna ukosefu wa kufahamu kwamba unaweza kuwa na msimamo bila ya kuwakasirisha wengine. Ndiyo maana kukawa na kitu kinaitwa diplomasia.