'Maambukizi' Tanzania kamwe hayawezi kupungua, NGOs zinashindana kutengeneza takwimu takwimu za kutisha kwenye maeneo yao ili waendelee kupata Funds.
Huko NGos hazifanyi vile zinatakiwa, zimeishiwa kabisa ubunifu, matokeo yake, nchi unakua victim wa kwanza kwa kupewa wrong data.
Identification ya positive clients ni biashara nzuri inayolipa kwa NGOs za afya nyingi.
Akija Donor akitangaza Extra Funds kwa mikoa ambayo maambukizi yamepungua utaona vile maambukizi mapya yatakavyoshuka na jitihada zitafanyika kuwaondoa wale ambao tayari wapo. Ikitangazwa tena fund itatolewa kwa mikoa yenye waathirika wengi mtaona vile ghafla waathirika wanavyoibuliwa ghafla.
Hata malaria, sasa hivi ni kama vile jitihada za kuitokomeza ni kama inaelekea kufanikiwa, lakini akiibuka donor na kutangaxa fungu utaona Malaria inavyokuzwa, hadi Makete itaonekana ndiyo inayoongoza kwa Malaria nchini kama vile ambavyo mikoa ya Njombe, Iringa na Singwe inavyoongoza kwa utapiamlo.
Mbele ya Pesa utapata data zinazoongea chochote mahala popote.
Mbele ya Pesa unaweza ukaletewa Data zunazoonyesha Pemba ndiyo segemu inayoongoza kwa idadi ya Makanisa nchini.
Hatuheshimu data kabisa matokeo yake tumetengeneza majiko mazuri kwa ajili ya kuzipika.