Sio peke yake, kuna mto Kilombero unaanzia mbaali Njombe uko, pia kuna mto kama jina ni Lukuledi unafanya mpaka wa Morogoro na Lindi, unaanzia Tunduru unapita Mbuga ya Nyerere Morogoro, pia kuna Mito mingi midogo midogo ya Morogoro. Huo Ruaha unatumika sana ndio maana unaasirika, kuanzia Kitulo Makete unatumika hadi Chimala unatumika, madibila, Usangu wanamwagilia mpunga bado mifugo, mbugani Ruaha, pawaga, mtera wanayazuia maji kuzalishia umeme, Ruaha mbuyuni wanalimia vitunguu, Kidatu wanazalishia umeme, Kilombero wanamwagilia miwa, kila mto unapokwenda unatumika lazima ukauke. Bora mto Kilombero na Lukuledi.