Hali ya Mwili wa Binadamu baada ya kufariki

Hali ya Mwili wa Binadamu baada ya kufariki

No kuna stage ikifika mwili unalainika tena baada ya kukakamaa.
Ok, baada ya kufariki maziko yakawa ni kesho yake , so hatukumfanyia treatment yoyote ya mwili ,yani kumchoma sindano au dawa yoyote, wakati amefariki nilikaa naye hapo wodini kitandani kwa muda wa masaa matatu , yani kafariki saa moja usiku, kitendo cha kukubali mwachia awekwe motuary ilikua imesha fika saa nne usiku , so tume kaa naye zaidi ya masaa matatu, kipindi hicho chote hakukakama, ,kesho yake tukaenda chukua mwili , mpaka tuna wingize msikitini tukiwa tume mbeba kwenda kuoshwa alikua laini viungo vina kunjika, so una maana alipo kuwa morturary ali kakamaa na asubuhu ndio aka rudia kuwa laini tena ?
 
Yeah kuna stages kabisa. Ndio maana huwa anafungwa mdomo kabla hajakakamaa. Misuli inakaza kisha baadae inalegeaga.
 
Mmh huyu atakuwa hajafa kabisa kwakuwa kama amekufa kabisa damu huanza kuganda kwakuwa haizunguki tena na mwili hukakamaa.. Dalili za viungo kuwa flexible ni kwamba bado kuna uhai

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sahihi kabisa kwamba utengano (mwili wa marehemu kuharibika) huanza dakika kadhaa baada ya kifo na mchakato unaoitwa "autolysis", au kujitegemea. Mara baada ya moyo kuacha kupiga, seli hunyimwa oksijeni, na asidi huongezeka kama sumu na athari za kemikali huanza kujilimbikiza ndani ya seli mfu.

Masaa 24-72 baada ya kifo - viungo vya ndani vinaharibika. Siku 3-5 baada ya kifo — mwili huanza kuoza na kuvuja povu za damu kutoka kinywani na puani. Siku 8-10 baada ya kifo - mwili hugeuka kutoka kijani hadi nyekundu kama damu inavyoharibika na viungo katika tumbo hujilimbikiza gesi.
 
Suala la kumkuta marehemu akiwa na atokwa na damu puani baada ya kulala mortuari kwa masaa 16 na je inakuaje mwili wa binadamu kukaa kwa masaa yote hayo bila ya kukakamaa yaani mwili unakuwa uso umevimba lakini viungo vyote viko laini havijakakamaa kwa masaa hayo yote mpaka anazikwa?

Rigor Mortis/kukakamaa kwa viungo baada ya kufariki.

Huanza saa mbili baada ya uhai kutoka, huchukua takribani saa 6-8 kukamilika.

Hali hiyo huweza kubaki hivyo kwa saa 12-24 baada ya uhai kutoka na kuondoka.

Hivyo, inawezekana kukawa na hali nyingi zinazoweza kusababisha utofauti.

1: Muda rasmi wa uhai kuondoka/uhalisia.

2: Size ya mwili.

3: Kiasi cha ufunikaji mwili baada ya kifo

4: Hali ya afya kabla ya kifo

5: Aina ya tiba kabla ya kifo

6: Mazoezi ya mwili aliyokuwa akifanya mhusika

7: Joto la eneo husika

MFANO:
A: Kwenye joto la 6 centigrade
Hufanyika ndani ya saa 48-60
Huisha kwenye saa 168

B: Kwenye joto la 24 centigrade
Huchukua saa 5 kuanza
Huisha ndani ya saa 16

C: Kwenye joto la 37 centigrade
Huanza ndani ya saa 3
Hisha ndani ya saa 6

NB: Autolysis: ni kitendo cha cell za mwili kuharibiwaa na vimeng'enyo vya mwili/enzymes. Hii huanza mara tu baada ya kifo au ndani ya wastani wa dakika 4.
 
Back
Top Bottom