Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Ripoti ya utafiti wa Hali ya Maisha ya Vijana Viziwi Tanzania uliofanywa na Mwanafunzi wa Sayansi ya Jamii Monica Har kutoka Loma Linda University (2011) ilionyesha changamoto wanazokumbana nazo viziwi kwenye kupata elimu Tanzania. Malengo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (UN) unazitaka nchi kuwa na mfumo ya elimu jumuishi katika shule zote unaoweza hata kueleweka kwa wanafunzi viziwi.
Mtalaa wa elimu kwa wanafunzi viziwi uko tofauti na wanafunzi wengine. Wanafunzi viziwi hupata elimu ya awali kwa miaka kumi ikilinganishwa na miaka saba kwa wanafunzi wengine. Utafiti ulionyesha tayari zipo shule maalumu kumi na tatu za viziwi Tanzania bara na hakuna shule rasmi ya viziwi ambayo imegundulika Zanzibar.
Shule zilizopo Tanzania bara hazijaweza kukidhi kundi kubwa la wanafunzi wanaosubiri udahili kutokana na upungufu wa madarasa na uhaba wa waalimu wa kufundisha. Upungufu wa nyenzo za elimu kwa viziwi imewapelekea wazazi na walezi kuwapeleka wanafunzi viziwi katika shule za kawaida ambako hukutana na changamoto zaidi.
Shule maalum za viziwi zilizopo hivi sasa zina changamoto ya ukosefu wa vifaa vya mawasiliano, nyenzo za kujifunza, mahusiano hafifu kati ya walimu na wazazi.