Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana

Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hili soko ni Maarufu kama Mahakama ya ndizi , liko Mabibo , Mkoa wa Dar es Salaam , Ushuru unaopatikana kwenye soko hili kwa mwaka ni zaidi ya hela ya madafu Bil 1.2

Subpost%201%20-%20Soko%20la%20Mabibo%20(mahakama%20ya%20ndizi)%20linaingizia%20halmashauri%20y...jpg
Subpost%202%20-%20Soko%20la%20Mabibo%20(mahakama%20ya%20ndizi)%20linaingizia%20halmashauri%20y...jpg


Toa maoni yako .


================================

WADAU WALALAMIKIA MIUNDOMBINU NA USAFI WA SOKO LA MABIBO

Soko la Mabibo ni moja ya masoko maarufu Mkoani Dar es Salaam hususan katika uuzaji wa ndizi mkoani humo hali inayofanya Wananchi wengi kwenda kupata huduma.

Kutokana na mvua zinazoendelea mkoani humo, hali ya miundombinu na mazingira ya soko hilo imekuwa sio nzuri kwa Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa ambapo tope maji hujaa sehemu kubwa ya soko.

Wadau wanaofanya ununuzi katika soko hilo wamelalamikia hali hiyo huku wakihoji ushuru wanaokatwa Wauzaji unatumika kufanyia nini iwapo soko lipo katika hali mbaya.

Hali ya soko hilo inaweza kusababisha mlipo wa magonjwa mengi ikiwemo Kipindupindu na kuleta athari si tu watumiaji wa soko bali Wananchi wote kwa ujumla.

Pia soma:

8cfb99f6-9541-4354-a2af-2aa320741d54.jpg

98a69a5c-8a2b-4dee-ab60-5a02b1ca3015.jpg

153ce067-6933-45dc-ae8f-0c8f5f47b547.jpg

a3046a21-e391-4e3a-8839-b34b310f5b77.jpg
 
Hili soko ni Maarufu kama Mahakama ya ndizi , liko Mabibo , Mkoa wa Dar es Salaam , Ushuru unaopatikana kwenye soko hili kwa mwaka ni zaidi ya hela ya madafu Bil 1.2

View attachment 2211524View attachment 2211526

Toa maoni yako .
Nimewahi kufika hapo kweli panapilika sana. Maoni yangu serikali ilifumuwe na kujenga mpya mana hela zinazoingia ni nyingi. Haifai kuimba maendeleo wakati soko lipo hovyo, watoto mashuleni wengine wakaa chini, maji na vyoo tatizo.
 
Si kweli, ukusema 1.2 bil maana yake wastani nu Tshs 100,000,000 kila mwezi sawa na Tshs 3,333,333.33 ni sahihi?
Tuache uchochezi.
 
Back
Top Bottom