Hali ya Uchumi na kupanda kwa bei, Waziri Kijaji asema Bei za bidhaa za ndani ni himilivu. Waziri Mwigulu aahidi kupunguza bei mafuta ya kula na gari

Hizo % za tax zikishuka, si wamesha pitisha kwenye budget, wata recover vp ktk budget? Mm nashauri waache hivyo hivyo, sbb ukianza kushusha kodi kwenye vyakula vyote, mara mafuta ya gari, mara mbolea, mara sijui nn, budget itakuwa ngumu sana kutekelezeka..

Tuvumilie hivyo hivyo tu, Putin atamaliza vita muda si mrefu, within 6 months mbona mambo yatenda tu.
 
Kwani kodi wanayosema ipunguzwe hajaingizwa kwenye budget ijayo?.
 

Kwako wewe mambo yataenda tu kwakuwa kuna mahala unafyonza hawajakushitukia!!! Hiyo miezi sita unayojsema kwa hali ilivyo unadhani kutakuwa na usalama? Au mwenzetu unaishi MARS!!!!
 
Kwani sisi ndo wa mwisho hapa tanzania mpaka tuijenge iishe na kwa nn tujiteseeeee km hakuna kizazi kingine ambacho hawatakuja kuijenga tz.Unapo ona kuna shida sitisha mambo mengine punguza matumizi yasiyo lazima wananchi wapate ahueni ...mkuuu hali ni mbaya ama ww unakaa kwa shemeji yako.
 
Kwani Russia na Ukraine wameshaweka chini silaha zao?
 
Desperate times need desperate measures!
 
Huwezi zungumzia shusha mafuta ya kula tu, bila gusia shusha mafuta ya kuendesha mashine mbalimbali petrol deseal ,hapo ndo drive ya kula kitu,mmeweka matozo kibao alafu mwigulu anatwambia nini, alafu utasikia naye anayo malengo ya kuwa Rais,very shame
 
Inshu ya kupanda kwa bei wasitafute mchawi,mchawi ni Samia,alisikika zaidi ya mara mbili akisisitiza upandaji wa bei kwa vitu vyote!
 
Kama kuna kitu kinanishangaza nchi hii ni hili suala la kununua ngano na shayiri kutoka nje wakati kuna ardhi na hali ya hewa nzuri inayoruhusu ulimaji wake hapa nchini kutosheleza mahitaji ya ndani na kuuza nje ya nchi. Tuna mashamba ya Basotu, Mbeya na West Kilimanjaro yalikuwa yanatosheleza kabisa mahitaji ya ndani kwa chakula na shayiri kwa viwanda vyetu vya bia miaka iliyopita. Sijui hata kimetokea nini kiasi nimeshtuka kuwa eti tunaagiza tani kibao kutoka nje.

Ushauri wangu kwa waziri wa kilimo hebu fanya utafiti mdogo wa haraka haraka nini kimesababisha hii hali na nini kifanyike kwa haraka ili tujitosheleze kwa ngano hapa nchini. Na hii iwe chachu ili ukifanikiwa katika ngano uhamie kwenye mafuta ya kula na mazao mengine kwani naamini kabisa tukiwa "serious" hata mawese na alizeti yanaweza kabisa kuzalisha mafuta ya kulisha nchi nzima bila kuagiza nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…