johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Wapi?Tutafika Tumechoka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapi?Tutafika Tumechoka
Acha mashaka waziri mchumi anazingatia yote hayo🤔Hizo tozo hazijapitishwa kwenye bajeti na bunge? Yasijetokea yale ya tozo za mafuta😂😂😂
Ni blind SII Kwa bahati mbaya ila Kwa sababu 😂Nchi ya blind viongozi blind
Peleka taarifa wewe chawa wao !! Tukiona wameacha kurusha CHOPPER na kuvurumisha maV* hovyo tutajua ujumble umefika. Wasidhani kwavile Samia anafunga basi hajui kinachoendelea!!!Serikali imekusikia!
Hizo % za tax zikishuka, si wamesha pitisha kwenye budget, wata recover vp ktk budget? Mm nashauri waache hivyo hivyo, sbb ukianza kusha kodi kwenye vyakula vyote, mara mafuta ya gari, mara mbolea, mara sijui nn, budget itakuwa ngumu sana kutekelezeka..
Tuvumilie hivyo hivyo tu, Putin atamaliza vita muda si mrefu, within 6 months mbona mambo yatenda tu.
Kwani kodi wanayosema ipunguzwe hajaingizwa kwenye budget ijayo?.
Kwani sisi ndo wa mwisho hapa tanzania mpaka tuijenge iishe na kwa nn tujiteseeeee km hakuna kizazi kingine ambacho hawatakuja kuijenga tz.Unapo ona kuna shida sitisha mambo mengine punguza matumizi yasiyo lazima wananchi wapate ahueni ...mkuuu hali ni mbaya ama ww unakaa kwa shemeji yako.Hizo % za tax zikishuka, si wamesha pitisha kwenye budget, wata recover vp ktk budget? Mm nashauri waache hivyo hivyo, sbb ukianza kusha kodi kwenye vyakula vyote, mara mafuta ya gari, mara mbolea, mara sijui nn, budget itakuwa ngumu sana kutekelezeka..
Tuvumilie hivyo hivyo tu, Putin atamaliza vita muda si mrefu, within 6 months mbona mambo yatenda tu.
Fafanua!
Kwani hilo budget haiwezi kuwa adjusted?
[/QUOTE
Hawana ubavu huo.
Desperate times need desperate measures!Hizo % za tax zikishuka, si wamesha pitisha kwenye budget, wata recover vp ktk budget? Mm nashauri waache hivyo hivyo, sbb ukianza kusha kodi kwenye vyakula vyote, mara mafuta ya gari, mara mbolea, mara sijui nn, budget itakuwa ngumu sana kutekelezeka..
Tuvumilie hivyo hivyo tu, Putin atamaliza vita muda si mrefu, within 6 months mbona mambo yatenda tu.
Inashangaza sanadah aisee ni shida tulikuwa tunajadili mahali hadi nikatamka bei ni humilietive
Mawaziri wawili wako ukumbi wa mikutano wa hazina, Dar es Salaam kubwa likiwa hali ya uchumi na kupanda kwa bei za bidhaa. Yupo waziri wa uwekezaji, Dkt. Asha Kijaji na waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba.
Zifuatazo ni nukuu muhimu
Dkt. Kijaji: Niliagiza mamlaka zinazosimamia mwenendo wa soko la bidhaa kuchukua hatua za kisheria pale ambapo chanzo cha kupanda kwa bidhaa hizo itathibitika kuwa ni michezo ya wafanyabiashara. Mamlaka haya tumepewa kisheria kupitia sheria ya ushindani.
=> Tathmini ya kina iliyofanyika inaonesha kwamba bei ya bidhaa nyingi zinazozalishwa hapa nchini bei yake ina uhimilivu yaani stable japo zipo bidhaa chache sana kama saruji na nondo ambazo bei zao zilikuwa zimepanda kwa viwango visivyohimilika wakati tunafanya tathmini hii.
=> Kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi yetu, tathmini imeonyesha bidhaa kuwa na bei zisizo na utulivu na zisizohimilika na ndio maana tuko na wazalishaji kutoka kwenye sekta mbalimbali, sekta ya mafuta ya kula, wanaotuuzia petroli, dizeli, tunao watu wa nondo, saruji ili kwa pamoja haya tuliyoyagundua tuyaseme wote kwa pamoja kwa watanzania na lipi watanzania tujiandae.
=▷Waziri Kijaji amesema visababishi walivyogundua upandaji wa bei ni janga la Uviko-19 ambapo chumi nyingi zimefungwa na upungufu wa bidhaa katika soko la dunia kutokana na kufungwa kwa viwanda baada ya watu kufungiwa kanuni ya 'demand and supply' kutumika kuamua bei.
=▷Pia Waziri Kijaji amesema vita ya Urusi na Ukraine imechangia ikiwemo Tanzania kuagiza bidhaa kutoka katika nchi husika.
=> Dkt. Kijaji: Kuna hoja kwamba ongezeko kubwa la bei za bidhaa hizi zitokapo nje ya viwanda, tulipoongea na wenye viwanda vya saruji walisema wao hawajapandisha bei kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.
KUPANDA KWA BEI YA NGANO
=> Dkt. Kijaji: Tunaagiza ngano tani laki nane kwa mwaka mmoja, sisi watanzania tunazalisha tani laki moja tu kwahiyo tunaweza tukaiona athari ilivyo kubwa, hapa tunapoagiza tani laki nane, asilimia 57 inatoka Urusi na Ukraine
MAFUTA YA KULA
=> Dkt. Kijaji: Tulishaathirika na janga la Uviko, bei ya kuagiza imeongeza hivyo bei ya uuzaji lazima kuongozeka, pia vita ya Urusi na Ukraine. Kwa wachumi wanafaahamu, hii tunaita imported inflation. Unaiingiza kutoka nje kuja kwenye nchi yako kwasababu huzalishi kiwango kinachohitajika.
=> Dkt. Kijaji: Uhitaji wa mafuta ndani ya Taifa letu kwa mwaka ni tani 650,000 huku uwezo wetu wa kuzalisha ikiwa ni tani 270,000 tu.
MBOLEA
Bei ya mbolea imeruka kabisa sio kupanda. Imeruka kwasababu ya janga la Uviko na vita. Uhitaji wa mbolea ndani ya Taifa letu ni tani laki saba kwa mwaka na sisi tuna uwezo wa kuzalisha tani elfu 30, tuna tofauti ya tani 630,000 ambayo yote tunaagiza kutoka nje.
=> Mwigulu Nchemba:
UCHUMI UMEPANDA
"Ukuaji wa uchumi kwa Tanzania ulishuka kutoka 7% hadi 4.8% na sasa uchumi umepanda hadi 4.9% huku nchi nyingine uchumi wake ulishuka hadi kufikia hasi, siwezi kuzitaja wka sababu za kidiplomasia
"Dira sahihi ya kututengenezea uchumi wetu ni kuendelea na kazi, hata itokee vita huko ulimwenguni au mawimbi ya ugonjwa wa Uviko-19, dira sahihi ni kuendelea kufanya kazi.
"Yanayotokea Urusi na Ukraine, yasitufanye tukaacha shughuli za uzalishaji na uchumi au uendelevu wa miradi ya maendeleo.
"Wenzetu wa Benki ya Dunia wanasema kama tukiendelea kuwa na uvumilivu huu uchumi unaweza kupata kwa asilimia 5.5. Pamoja na majanga, tuendelee na kazi, mambo hayatakuwa rahisi lakini hii ni dira sahihi licha ya yote yanayotokea, hata kama itatoea Covid tena.
KUHUSU BIDHAA KUPANDA BEI
"Bidhaa tunazosema zimepanda, ni bidhaa zinazonunuliwa na kusafirisha. Tunachotaka kufanya ni kupunguza makali, tukitaka kuondoa tatizo lote kabisa ni kutengeneza hatari kwa kuwa tunakabiliana na tatizo lililopo nchi nyingine lakini pia tusiruhusu uhaba wa bidhaa
SUKARI KUPUNGUZWA KODI
"Rais Samia Suluhu ameelekeza tuchukue hatua za muda mfupi na kisha tukiendelea kufanya tathimini ya yanayoendelea.
"Tutapunguza kodi ya sukari kwa kiwango si chini ya asilimia 10 kwa muda, baada ya hapo tutaangalia mwezi mmoja miwili. Tutakapokuwa tunapitisha sheria mpya ya kodi tutaangalia mambo yanaendaje
MAFUTA YA GARI, MAFUTA YA KUPIKIA TUTAANGALIA
"Kwa mafuta ya magari tutaangalia gharama zinazotuhusu kwenye mafuta tuone kiwango ambacho tutapunguza. Tutaangalia ni namna gani tunaweza kupunguza. Tutaangalia sisi taasisi ndani ya Serikali kitu gani tunaweza kupunguza.
"Timu yetu ya wataalam itakaa ndani ya wiki moja hivi inaweza kuwa wameshapata jibu kujua ndamba ili tuweze kuchukua hatua. Ukisema mafuta yameshapanda bei tuondoe fedha yote inayotengeneza barabara, itaathiri barabara ambazo zinatumia fedha hizo kutengeneza barabara.
"Kwenye mafuta ya kupikia tutaangalia namna ya kupunguza na kuja na viwango vipya vya kodi na hili tutakaa pamoja na sekta binafsi kuona tunakuja kiwango gani. Ndani ya mwezi mmoja na mwezi mmoja na nusu tutaweka viwango vipya.
Tunaangalia kwa muda huu, tutakuja na viwango vipya vya kodi, tutashirikiana na wenzetu wa sekta binafsi ili tuweze kupata kitu cha kumnufaisha mwananchi wa kawaida.
"Tutapunguza sehemu ya gharama ambayo ilikuwa inaongezeka katika vifaa vya usafiri, ili tukipunguza gharama kwenye mafuta na vifaa hivyo moja kwa moja tunaamini itashusha gharama na bei ya bidhaa nyingine.
TUFANYE KAZI HATA KAMA KUNA COVID
"Angalieni wakati wa kipindi cha ugonjwa wa Uviko-19 waliwafungia ndani, waliweza kuwalisha kwa wiki moja na zaidi ya watu 100 walifariki huku wengine wakiandamana kwa ajili ya chakula.
"Hakuna ambaye anajua Covid itaisha lini au mgogoro wa Ukraine na Urusi utaisha lini.
Inshu ya kupanda kwa bei wasitafute mchawi,mchawi ni Samia,alisikika zaidi ya mara mbili akisisitiza upandaji wa bei kwa vitu vyote!Samia ameishaambiwa mapungufu ya huyu waziri wake wa fedha lakini Katia Pamba maskioni . Hapa mnacheza na uhai wa watu na familia zao . Mishahara haipandi na kipato kimepungua lakini bei za mahitaji muhimu zimepanda hivyo kuumiza wananchi!!
Viongozi hamuwezi kuelewa machungu wanayopata wananchi kwasababu kipato chenu kikubwa!!
Haiwezekani na sio busara mawaziri kila siku kuimba tu sababu za kuwa na mfumuko wa bei, wananchi wanataka kuona hatua zinachukuliea zitakazopunguza makali ya mfumuko wa bei!
Njia moja serikali inaweza kusaidia ni kwa kuahilisha miradi isiyokuwa na kipaumbele kwa wakati huu. Serikali isimamishe ununuzi wa zile ndege za ATCL iilizoagiza kwani hivi sasa hali ya uchumi ni tete; nina hakika hao mlikoagiza hizo ndege watawaelewa. Punguzeni pia matumizi ya serikali ya siyo ya lazima kama hizi safari za maV8 kuja Dar. Toka Dodoma kila leo!!
Wananchi wanataka kuona hatua mathubuyu zinachukuliwa kuwapunguzia maumivu na sio kila leo vita ya Putin ndio kisingizio!
Mnataka waandamane ndio mtajua wanaumia?
OkayAiseh haya!!