Hali ya uchumi ni mbaya mno, ni nini itakuwa tumaini la watanzania masikini

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,951
Reaction score
19,766
Habari wanajamvi.

Ukiwa unaishi Dar es salaam,halafu ukienda mikoani safari zako zinaishia mijini basi huwezi ukajua ya ndani kuhusu hali ya uchumi wa nchi hii.

Mimi shughuli zangu zinanifanya niwe natembelea sehemu za vijijini zaidi,basi ndugu zanguni maisha ni magumu na inatakiwa itolewe elimu Kwa watu wengi namna ya kukitumia kipato chao kidogo.

Lakini pia itolewe elimu kuhusu suala zima la uzazi wa mpango

Hebu fikiria mtu ana umri wa miaka 30 ,lakini tayari ana watoto 4 mpaka 5 hii imeniumiza,mtu huyu ana kibanda kilichoezekwa Kwa makuti (nyasi) halafu anavyoikatili familia yake ,bado kakopeshwa solar sets , yaani TV,na kafunga king'amuzi kabisa,ilhali watoto wake wanatembea uchi kabisa.

Huku miili yao ikiwa haina nuru wala afya,watoto wameongozana utadhani mapacha, imeniumiza Sana.

Lakini ukatili Kwa wanawake bado ni janga kubwa , mwanaume ni mtu wa kulewa , mwanamke ni mtu wa kwenda shamba , kuandaa chakula,kuwafulia watoto pamoja na kulazimishwa kutoa unyumba hata akiwa hayupo sawa,na ikitokea kafanya kosa hilo ni kipigo cha paka mwizi na pakushtaki hana.

Lakini pia suala la kujazana majengo ya zahanati ikiwa dawa na wauguzi hakuna,zahanati inakuwaje na muuguzi mmoja au wawili tu?
Ni hatari.

Kingine maji Safi na salama,hapa ni kitendawili ,nililazimika kusafiri zaidi ya 100 KM kufuata maji safi,yaani wanakijiji wanakunywa maji ya mtu ambako ng'ombe na watu wanaoga na kufua humohumo.

La mwisho ni umasikini kiujumla,

Jamani,Hali ni mbaya wengi Wana maisha magumu mno,tena mbaya zaidi wenyewe wameridhika ,
Mmmmh Mungu tusaidie
 
Attachments

  • downloadfile.jpg
    downloadfile.jpg
    96.2 KB · Views: 33
Tumaini lililobakia ki KUFA tu maana watawala hawataki kabisa kusikia tunalala njaa na mzunguko wa pesa ni mbovu balaa na biashara zimepigwa rungu na TRA na mamlaka zingine.....

Wananchi wakiongea na kuleta hoja basi WATAWALA wanatoa pesa kwa vijana wao wa FISIEM wanajivika mavazi kiraia na kusambaza taarifa za ajabu mitandaoni kuondoa sintofahamu.....

Ningeongea mengi ila MWANASHERIA wangu alifutiwa LESENI na sasa yupo JELA BUTIMBA.
 
ungetuambia upo mkoa gani, wilaya gani ingekuwa poa zaid
Ndani ya miezi sita kuanzia mwishoni mwa mwaka Jana mpaka sasa nimezunguka mikoa 18 Tanzania bara
Hali ya uchumi inafanana karibia mikoa yote haswa rural areas
 
Changamoto kijijin ni exposure,
Kijana ana miaka 20 ashaoa,
Vijana kupenda pombe na kutopenda kazi
 
na badoooooooooooooooooooooo mitano tena kwao, mkiambiwa mafisiemu ndio wameifikisha nchi hapo mnanuna, kuleni jeuri yenu makomandoo wa shida.
 
Vijana wenyewe hawajitumi mda wote ni vijiwe tu na story zisizo na msingi wao ilimrad wamekula na kulala
 
Habari wanajamvi.

Ukiwa unaishi Dar es salaam,halafu ukienda mikoani safari zako zinaishia mijini basi huwezi ukajua ya ndani kuhusu hali ya uchumi wa nchi hii.

Mimi shughuli zangu zinanifanya niwe natembelea sehemu za vijijini zaidi,basi ndugu zanguni maisha ni magumu na inatakiwa itolewe elimu Kwa watu wengi namna ya kukitumia kipato chao kidogo.

Lakini pia itolewe elimu kuhusu suala zima la uzazi wa mpango

Hebu fikiria mtu ana umri wa miaka 30 ,lakini tayari ana watoto 4 mpaka 5 hii imeniumiza,mtu huyu ana kibanda kilichoezekwa Kwa makuti (nyasi) halafu anavyoikatili familia yake ,bado kakopeshwa solar sets , yaani TV,na kafunga king'amuzi kabisa,ilhali watoto wake wanatembea uchi kabisa.

Huku miili yao ikiwa haina nuru wala afya,watoto wameongozana utadhani mapacha, imeniumiza Sana.

Lakini ukatili Kwa wanawake bado ni janga kubwa , mwanaume ni mtu wa kulewa , mwanamke ni mtu wa kwenda shamba , kuandaa chakula,kuwafulia watoto pamoja na kulazimishwa kutoa unyumba hata akiwa hayupo sawa,na ikitokea kafanya kosa hilo ni kipigo cha paka mwizi na pakushtaki hana.

Lakini pia suala la kujazana majengo ya zahanati ikiwa dawa na wauguzi hakuna,zahanati inakuwaje na muuguzi mmoja au wawili tu?
Ni hatari.

Kingine maji Safi na salama,hapa ni kitendawili ,nililazimika kusafiri zaidi ya 100 KM kufuata maji safi,yaani wanakijiji wanakunywa maji ya mtu ambako ng'ombe na watu wanaoga na kufua humohumo.

La mwisho ni umasikini kiujumla,

Jamani,Hali ni mbaya wengi Wana maisha magumu mno,tena mbaya zaidi wenyewe wameridhika ,
Mmmmh Mungu tusaidie
Lini maisha yalikua marahisi
 
Ndani ya miezi sita kuanzia mwishoni mwa mwaka Jana mpaka sasa nimezunguka mikoa 18 Tanzania bara
Hali ya uchumi inafanana karibia mikoa yote haswa rural areas
Hali ya umaskini nchi yetu ni mbaya na watu wameridhika.

Ila kuwa makini sana, kuna watu unakutana nao unawaona ni maskini kwa kuangalia mavazi yao au nyumba wanazoishi. Ila haohao wanamiliki mifugo, misitu ya miti n.k
 
Back
Top Bottom