Hali ya umeme ni mbaya sana Mkoa wa Mara, sijui ulipo hali ikoje?

Giltami

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,038
Reaction score
1,623
Jana nimeanza kutafuta Generator ,biashara yangu kwa mwezi sasa imekuwa na changamoto kubwa sana ya umeme nimepata hasara ambayo siwezi kui cover kirahisi kabisa Tanesco tatizo nini jamani?

Tunaomba basi Waziri zungumza na Taifa nini chanzo umeme kuwa tatizo?

Sifikirii 2023 kupata changamoto ya umeme naona ni kama uzembe sana TISS mko wapi haya mambo mbona madogo sana kwa mataifa yanayojua maendeleo ni nini?
 
Nnachojua mimi mkoa wa Mara pamoja na mikoa mingine Tanzania kuna maboresho ya miundombinu ya umeme msongo wa kati......yani medium voltage lines.

Maboresho haya yanafanywa mchana, umeme lazima ukatwe, na imeamuriwa umeme ukatwe siku 3 tu kwa week.

Huna haja ya kununua generator, hiyo hali itaisha ndani ya mwezi mmoja.
 
Na mkoa sehemu ambayo nimekwenda umeme ni tatizo ni Turiani wilaya ya Mvomero, umeme ni shida sana, Yani kwakweli Tanesco waliangalie hili.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Well said

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Hujui ulisemalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…