Hali ya umeme yawa ya matumaini baada ya juhudi za Serikali pamoja na mvua kuanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini

Mimi ni mkulima. Naelewa vema. Ninapinga uingo wako kwamba mbolea imepungua hadi 70 elfu.

Kilichofanyika hapa ni kuongeza kodi kwenye huduma za jamii halafu mmeifanyia biashara ya kuuza mbolea kwa bei ya juu zaidi na kujifanya mmetoa ruzuku.

Hapa hakuna ruzuku, bei ni ileile isipokuwa mmechukua hela yangu mkanilipia halafu iliyobaki nipe mimi.

Huu ni mpango wa wizi mkubwa zaidi kuwahi kufanyika kwenye sekta ya kilimo.

Bei ya mbolea iko juu sana Tanzania.
 
Embu nijibu mbolea ya DAP ya Ruzuku inauzwa shillingi ngapi?
 
Namba za simu ni za nini sasa? Vijana mnajua kupambania fursa 🤣🤣🤣
 
Niliko Mimi Hali ya Umeme imeanza kurejea na kuwa ya Matumaini ,mfano kuanzia ijumaa umeme upo muda wote na hata hapa napoandika umeme upo na tunajiandaa kwenda kuangalia mpira baadaye
Sasa hapa ndo umedhihirisha una ugonjwa wa akili. km huko uliko kuna umeme ndo unakuja kusifia hapa hali imetengemaa kweli? Umefanya research ya maeneo mengine???? Hapa tanki bovu karibu na kambi ya jeshi umeme unakatika balaaaa hata jana ulikuwa umekatika siku nzima una mpya gani ya kueleza? Acha ujinga aseee
 
Ndio nimefanya utafiti ambao umenifanya nieleze hicho nilichokieleza
 
Fikra za mtanzania ni kushukuru baada ya kupigwa, fikra za kitumwa!
 
Ndio nimefanya utafiti ambao umenifanya nieleze hicho nilichokieleza
Utafiti wa kijijini kwenu ukatosha kugenerelize Tanzania nzima? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nyie ndo wapika data mpka zinaungua Acha ujinga
 
Utafiti wa kijijini kwenu ukatosha kugenerelize Tanzania nzima? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nyie ndo wapika data mpka zinaungua Acha ujinga
Kwani Tanzania I a vijiji vingapi? Hujuwi kuwa vipo zaidi ya elfu 16? Unafikiri Ni vichache hivyo hata ningekuwa nimefanyia kijijini pekee?
 
Acha kusema uongo.kwa sasa hali ya umeme ni mbaya sana.hapa tu dar kila Siku wanakata.Mradi wa umeme vijijini umekufa toka mzalendo afariki na IPTL imeingia mzigoni na muda si mrefu gharama za umeme zitaongezeka
 
Acha kusema uongo.kwa sasa hali ya umeme ni mbaya sana.hapa tu dar kila Siku wanakata.Mradi wa umeme vijijini umekufa toka mzalendo afariki na IPTL imeingia mzigoni na muda si mrefu gharama za umeme zitaongezeka
Acha uongo wako hapa hizo gharama utapandisha wewe au unafikiri zinapanda kiholela tu bila utaratibu
 
Kuna story moja ya manyani. Kila mvua ikinyesha usiku wakati yakiwa yamelala utayasikia yanaguna na kusema , mhuuu, kesho lazima tujenge nyumba, mhhhuuu kesho lazima tujenge nyumba. Kunapokucha, jua likitoka yanasahau na kuendelea na shughuli za kutafuta chakula. Yatasahau ajenda ya nyumba kabisa mpaka pale yatakaponyeshewa tena ndiyo yataanza tena kusema, kesho lazima tujenge nyumba. Na sisi tumekuwa hivyo. Tangu nikiwa mdogo mpaka sasa hivi matatizo ya umeme na maji hutokea kwa kujirudia na yanapotokea ndiyo tunakuja na plan mfu, yakiisha tunasahu. Kweli kesho kesho ni ya manyani.
 
Kwani unafikiri idadi ya watu ipo pale pale tangia unazaliwa? Jiulize kwenye familia yenu wakati unazaliwa mlikuwa wangapi na Sasa mpo wangapi? Jiulize tulipokuwa tunapata Uhuru tulikuwa wangapi na Sasa tupo wangapi? Kama watu tunaongezeja unafikiri Mahitaji yatabaki palepale?
 
Pole mkuu hata hivyo Hali kwa Sasa Ni ya Matumaini na faraja ukilinganisha na awali ,mgao siyo mjali Sana na naamini halini akwenda kuwa njema Sana siku chache zijazo kutokana na uwingi wa mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali

Mgao umekuwa mkali zaidi kuliko hapo mwanzo wakati mvua hazijaanza kunyesha...

Sasa hv mpaka saa sita usiku na ni mara mbili au tatu kwa wiki...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…