Hali ya upatikanaji Maji Dar es Salaam ni shida. DAWASA iwajibike

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Ndugu Waziri wa maji,

Hali ya upatikanaji maji katika baadhi ya maeneo katika mkoa wa Dar imekuwa ni shida.

Majuzi DAWASA walitoa taarifa kuwa maji yangekatika kwa siku moja kupisha matengenezo, lakini leo tunakwenda siku ya tano hakuna maji, hivi mnataka sisi tuishije?

Wakati mwingine muwe mnaona aibu na muwe considerate katika maamuzi yenu katika hali ya kawaida chukulia mfano wa maeneo ya Sinza survey, hali imekuwa mbaya sana na DAWASA haitoi taarifa yoyote juu ya hali hiyo.

Ndugu waziri tunataka maji acheni longolongo, mbona wakati wa Magufuli haya mambo ya ajabuajabu yalikuwa hakuna, mnakwama wapi?
 
Kuna wakati Dar ilikua ukijenga nyumba unaanza kuchimba kisima kabisa cha maji. Unapata maji yenye chumvi lakini una uhakika nayo.
 
Lakini wana amani na raha.

Hii kukosa maji ni ujinga wenu.

Chimbeni visima
 
Kivuli cha Jpm kitaendelea kutesa !!
 
Mnataka maji ya Uhakika halafu wakija kwenye Kampeni Waseme wataleta nini mkiwa chagua shida ya Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla ni Je baada miaka 50 Uhuru kweli tulikuwa tayari kujitawala au Kuna Wajanja wachache tu Nia yao ilikuwa ni tusaidiane kumtoa Mkoloni weupe ili waje wao wakoloni weusi ambao kwangu binafsi ni wabaya zaidi ya Mkoloni mweupe...
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hatuna maji wala umeme ila maelfu ya viongozi kuanzia wilayani mpaka wizarani wanaendesha Toyota za milion 400 kila mtu, waafrica kichwani hakuna kitu mdomo tuu kutukana beberu ambaye analipa mishahara yao na kula rushwa ndio tunachojua
 
Kuna wakati Dar ilikua ukijenga nyumba unaanza kuchimba kisima kabisa cha maji. Unapata maji yenye chumvi lakini una uhakika nayo.
Kwahiyo nyumba nyingi dar zipo kama mboga, zina chumvi balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…